Arusha: Watu 6 wanusurika baada ya nyumba ya Wageni kuwaka moto

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Watu sita akiwemo mmiliki wa nyumba ya kulala kulala wageni ya Australia Lodge wamenusurika baada ya nyumba hiyo ‘gesti’ iliyopo Maji ya Chai wilayani Arumeru mkoani Arusha kuteketea kwa moto wakiwa wamelala.

Moto huo uliotokea ghafla wakati watu hao wakiwa wamelala unadaiwa kusababishwa na mtu mmoja ambaye alitoweka baada ya moto huo ukiunguza gesti hiyo.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumapili Januari 16, 2022 mmiliki wa gesti hiyo ambaye ni miongoni mwa walionusurika, Silvester Masawe amesema tukio hilo limetokea Ijumaa alfajiri wakati yeye pamoja na wateja wake watano wakiwa wamelala.

[https://a24tv]

“Kwa kweli hakuna kilichookolewa kila kitu kimeteketea kwa moto zikiwemo nguo za wageni na thamani ya mali zilizoungua pamoja na jengo inafika milioni 100” amesema

Mmoja wa walionusurika, Mohammed Rashid amesema moto huo umeteketeza kila kitu ikiwamo Sh300, 000 na nguo zake zote.

Kwa upande wake balozi wa eneo hilo, Kundandumi Kanuya amesema kuwa moto huo ulizuka alfajiri baada ya wapita njia kuona ukitokea katika chumba kimoja wapo na kuteketeza Kila kitu huku wageni waliokuwa wamelala wakiokolewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtu mmoja anashikiliwa kwa mahojiano na ikibainika ni yeye hatua zaidi zitachukuliwa.

“Nikweli tukio hilo lipo na kikosi cha zima moto walifanikiwa kudhibiti moto huo usisambae eneo linguine na mtu mmoja anashikiliwa kwa mahojiano na kithibitisha ni yeye aliyeusababisha atachukuliwa hatua “amesema

IMG_20220116_095541_184.jpg
IMG_20220116_095623_147.jpg
IMG_20220116_103303_851.jpg
 
View attachment 2084074View attachment 2084076View attachment 2084079

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Aussie
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom