Masanja Umechemsha bro!!

Mlisema Lissu chaguo la Mungu? Huyo mungu wenu muongo mbona chaguo lake limepigwa chini? Shetani Sasa ameshajulikana maana mlisema shetani hawezi kumshinda Mungu, Sasa chaguo la shetani chali.
UMEMSAHAU YULE MAMA ALIESEMA USHINDI KWA CCM HAUNA MUNGU AKIPENDA, USHINDI WA CCM NI WA LAZIMA.
HALAFU UMESAHAU KUA UFALME WA DUNIA HII NI WA SHETANI?
 
Masanja Mkandamizaji ndo msanii aliyefanya kampeni kubwa , hasa akijikita kwenye kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya tano kupitia sanaa. Anakipenda Sana chama na nchi.
Maendeleo yapi? Kwani maendeleo ni Hisani za CCM? au pesa za walipa kodi?
 
Mbona nyinyi mlisema Lissu ni chaguo la Mungu kapigwa risasi 16 na hakufa, Mungu kamleta kuwa Rais wa Tanzania?
Nyie kina nani? hii dhana yako dhaifu kufikiria mtu mwenye mawazo tofauti ni Chadema.
 
Afu linaongea kwa kiingereza eti ili wageni walielewe bora lingemaliza kwa kiswahili tu
 
Akili za wenzangu wanasusiemu wachumia tumbo kama Masanja haziwezi kuwa na jambo la maana zaidi ya utopolo wa kutaka waonekane kwa Boss wao. As matter of fact, Jiwe hata kaa awe Mtakatifu kwa maneno yenu ya kumpongeza bali Kupitia Toba yake ya dhati na ndipo hizo siafa zitakuwa na faida.

Masanja anamsifia sana Mkuu, huenda akapewa ukurugenzi au uDC hata Uwaziri. Ilq kumpa Masanja wizara litakuwa kosa kubwa sana kwa Mkuu wetu wa Taifa. Masanja hana uwezo wa kujenga hoja zaidi ni kusifia sifia tu.
 
We nae hebu ficha ujinga wako.Masanja ni Mnyakyusa wa Ubaruku Mbeya kile kisukuma anaigiza tu.
Mpangwa wa Ludewa Ubaruku anafanyia shughuli za kilimo sio kwao.
 
Afu linaongea kwa kiingereza eti ili wageni walielewe bora lingemaliza kwa kiswahili tu
Kakingereza kake ni kale ka kuunga unga alikosoma miezi sita British council
 
Sijaona Kosa lolote Masanja kusema hivyo / hayo sana sana naona tu 'Chuki' zako kwa Mshindi Rais Magufuli na chama chake bora hadi Mbinguni.
Chuki? Kwa hiyo waliomkosoa yule aliyemfananisha YESU na JPM nao wanachuki? au yule aliyesema "MUNGU amshukuru sana JpM" watu wakamjia juu nao wana chuki na Rais?
 
Kila mtu anakula kwastyle yake, nayeye ndiyo kula yake ipo hapo.....ajira zenyewe hakuna,Rais kipaumbele ni kujenga uwanja mkubwa Dodoma.
 
Mimi pongezi za kwanza kwa kudhibiti CORONA nawapa watanzania wote ambao waliitikia kwa pamoja tahadhali zilizokuwa zinatolewa hasa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kutokusalimiana.

Nilishuhudia kila kona kuna sabuni na maji ya kunawa sambamba na kupunguza mikusanyiko. Hata kwenye nyumba za ibada mikati ya social distancing ilizingatiwa na watu walimlilia MUNGU hata kabla JPM hajatangaza siku tatu za maombi. Tangazo la JPM liliongezea hamasa lakini si kwamba ndilo lililo wafanya watu waanze kuomba.
 
Mkuu kila mtu uwa anasifia anakokula, ukiwa pembeni lazima upate hasira. We achana naye pambana tu nawe ipo siku utakuwa unasifia wengine wamekaa pembeni wanapta hasira wanakuona snitch tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…