Barua ya wazi kwa Rais: Mhesimiwa, Mungu ametusikia sasa na wewe tusikie

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Mheshimiwa Rais

Yesu anasema kuwa, kabla hamjaomba chochote kutoka kwa Baba yenu aliyeko mbinguni yeye ameshatambua mkitakacho!

Tulipofunga na kusali kwenye wimbi la kwanza la korona, Mungu alitusikia na alituonyesha kitu gani cha kufanya kwenye hili tatizo ili tunusurike.

Mheshimiwa Rais, kwenye wimbi la kwanza la Korona Taifa Zima na Serikali yao tulichukua tahadhari. Kwenye wimbi hilo serikali yako ilichukua hatua zifuatazo:

1. Ilifunga mashule kuwalinda watoto na pia kuzuis watoto kuusambaza ugonjwa kutokea mashuleni

2. Ilizuia michezo

3. Iliweka uraratibu wa vyombo vya usafiri kuwa na level seat

4. Serikali yako kwa tamko lako wewe binafsi ulitangaza kuviomba vyombo vya habari viwe wadau na vishiriki kuuleisha umma juu ya ugonjwa huu

5. Serikali yako ilihimiza watu kunawa, na wananchi wakaitikia kwa wingi kwa kuweka ndoo za maji kila kona ya nchi

6. Baada ya kelele nyingi za wananchi Serikali yako ilizuia ndege kuingia.

7. Serikali yako ikshimiza maombi kwa Mungu atusaidie

Mheshimiwa Rais, ukiangalia orodha hizo hapo juu utaona kuwa katika wimbi la kwanza Serikali yako ilifanya kitu, ilichukua hatua za msingi za kuzuia tatizo hili kusambaa na kwa kweli tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Rais, kwa bahati mbaya kwenye wimbi hili la pili la huu ugonjwa serikali yako inataka kujitoa katika wajibu wa kuhakikisha usalama wa wananchi katika maambukizi haya mapya!

Mheshimiwa Rais, kama serikali yako inachukua hatua:

1. Kwanini mpaka hivi sasa serikali haitamki Ugonjwa wa COVID-19 kwa uwazi kabisa na kwa jina lake?, Wananchi watajuaje kuwa kuna COVID-19 kama huo ugonjwa hamuutamki kwa jina lake?

2. Kwanini pamoja na kutambua kuwa Korona haijaisha duniani serikali yako iliendelea kuruhusu watalii kuja nchini tena wengine kutoka katika nchi ambazo zilikuwa zikiripoti kuwa korona imechachamaa mathalani nchi ya uingereza?

3. Kwanini mpaka hivi sasa serikali yako haichukui hatua, japo baadhi ya zile ilizochukua katika wimbi la kwanza ikiwemo kuzuia mashabiki kujazana michezoni, mbona katika nchi nyingine ambazo timu zetu zinakwenda kucheza mashabiki hawaingii uwanjani?

4. Kwanini viongozi wa serikali yako ukiwemo wewe mwenyewe ukiwa kwenye public hamuongozi kwa mfano ili wananchi waweze kuwa na kigezo kizuri kutoka kwenu, kwa mfano hamvai barakoa wala kuweka social distance, Je maneno yenu ya kuwaabia wananchi wachukue tahadhari yatatafsirika vipi kama nyie wenyewe hamuyaishi in public?

4. Mheshimiwa Rais Kwanini mara nyingi umesikika ukiipiga vijembe barakoa, au ukiwapongeza wasiozivaa in public. Je hatua yako hiyo inasaidiaje mapambano dhidi ya Korona?

Mheshimiwa Rais, Mtume Muhammad amefundisha kuwa, Mfunge Ngamia wako asikimbie kisha Muombe Mungu amlinde ili asikimbie, siyo umuache hivihivi kisha eti ukazane na maombi Mungu amlinde!

Mheshimiwa Rais, umeuliza kuhusu kurudi kwa wimbi hili la pili kuwa tumekosea wapi?

Tulipokosea ni kwamba tuliacha kuwa serious kwa kitu ambacho Mungu ameshatuonyesha ukweli wake. Tumekuwa tukikataa kuwa hakuna korona nchini wakati tunajua ipo. Tumekuwa tukikejeli njia za kujikinga kama vile kuzipiga vijembe barakoa, Tumekuwa hatutaki kuuita ugonjwa hata kwa jina lake halisi, Tumekuwa tukiruhusu wageni kutoka nchi zilizoathirika na ugonjwa kuingia nchini kisa tunataka fedha, Tumekuwa hatutaki kujenga awareness kwa kumobilize nguvu zote za serikali kuuelimsha umma kuhusu kuchukua tahadhari za ugonjwa huu.

Mheshimiwa Rais, Mungu anajua ayafanyayo, katupa bongo tuzitumie, katupa utashi wa maamuzi, katupa zawadi ya watalaamu miongoni mwetu baadhi yao ni madaktari, Sasa basi Kumuomba Mungu ni jambo jema lakini tunatska kuona unachukua hatua na uwajibikaji katika hili suala!

Mheshimiwa Rais, Unahoji kama tuna imani kwa Mungu au la, jibu ni naam Imani tunayo na tunamuomba alinde maboma yetu lakini tunafunga maboma yetu usiku kabla ya kulala, Sasa na wewe ndiye mkuu wa hili boma liitwalo Tanzania, wakati ukitaka kila mtu achukue hatua, Pia kumbuka na wewe unaowajibu kama mkuu wa boma hili la Tanzania kuchukua hatua za kulinda boma zima!

Mheshimiwa Rais, unasema kufa kupo, magonjwa yapo kwa hiyo tuondoe hofu!. Mheshimiwa hatuondoi hofu kwa sababu ya kuamini hayo magonjwa yapo, tunaondoa hofu tukiamini kuwa ipo serikali responsible itakayofanya kila inayoweza kutunusuru huku na sisi tuitimiza wajibu wetu kujinusuru. Bila ya kuona kuwa seriali inafanya vitu fulanifulani vya msingi kama nilivyoekeza huko juu tutaendelea kuwa na hofu, maana huwezi kupambana na ugonjwa wa halaiki wewe peke yako ni lazima nchi nzima muwe vitani. Sasa serikali itakwepaje wajibu wake hapo?

Mheshimiwa Rais, Mungu anafanya yake na kwa muda wake, sasa na wewe chukua hatua sahihi kulinda Taifa hili dhidi ya hili janga!
 
Walioweka lokidowni wote wamezifungua na bado tatizo lipo,mnapomsikiliza Raisi mengine naona yanawapita na mnachagua yale mliyotulia nayo,

Mnataka Raisi afanye au aseme kitu gani ? Akili zenu zipo wapi ? afunge mashule ? Afunge safari za kuingia na kutoka mkoa kwa mkoa,wilaya kwa wilaya kijiji kwa kijiji mtaa kwa mtaa ??

Kuna shemu mmekosea mliambiwa habari ya nyungu mmeachana nayo,mbona wimbi la mwanzo wanancho nyote mlikuwa mnapiga nyungu,mlipozoea na kuona mafanikio mkawacha,sasa Rais akisema yeye kila siku anapiga nyungu mtasemaje ? Na tunamuona anachanganyika na watu kila aina.
Nyungu ni zoezi endelevu.
 
Ujumbe kuntu! Tujilinde wenyewe. Tusisubiri kulindwa. Pole kwa waliopata maumivu ya kuondokewa Na wapendwa wao. Mwishoni wenye hekima ya kuongoza uchumi watakwisha tusipochukua tahadhari ya kuwalinda.
 
Walioweka lokidowni wote wamezifungua na bado tatizo lipo,mnapomsikiliza Raisi mengine naona yanawapita na mnachagua yale mliyotulia nayo,

Mnataka Raisi afanye au aseme kitu gani ? Akili zenu zipo wapi ? afunge mashule ? Afunge safari za kuingia na kutoka mkoa kwa mkoa,wilaya kwa wilaya kijiji kwa kijiji mtaa kwa mtaa ??

Kuna shemu mmekosea mliambiwa habari ya nyungu mmeachana nayo,mbona wimbi la mwanzo wanancho nyote mlikuwa mnapiga nyungu,mlipozoea na kuona mafanikio mkawacha,sasa Rais akisema yeye kila siku anapiga nyungu mtasemaje ? Na tunamuona anachanganyika na watu kila aina.
Nyungu ni zoezi
Hatuzungumzii lockdown, tunazungumzia measures za kawaida za serikali kudhibiti spread ya kirusi hiki
 
Kijazi yeye hakutumia nyungu?
 
Hatuzungumzii lockdown, tunazungumzia measures za kawaida za serikali kudhibiti spread ya kirusi hiki
Kwa Heshima yako tu nkuulize: Ni nchi gan imechukua measures izo unazoita "za kawaida" na ikafanikiwa kuidhibiti au kupunguza kasi ya Corona???

Mataifa makubwa yenye kila aina ya democracy yamejilockdown lakini bado corona imeendelea kuwatafuna, cha msingi ni kila mtu kujipambania na afya yake

Kingine kinachowaua waAFRICA wengi ni "IGNORANCE" ...Wabongo wengi tuna tabia ya kupuuzia, Measures ya kawaida raisi kashasema tupige NYUNGU iyo inatosha...sasa wewe sijui ulitaka measure gan mjomba
 
Wewe unafikiri kwa nini kwenye wimbi la kwanza serikali ilichukua hatua ilizozuchukua na kwa nini haichukui tena hatua zile?
 
Wewe unafikiri kwa nini kwenye wimbi la kwanza serikali ilichukua hatua ilizozuchukua na kwa nini haichukui tena hatua zile?
Embu zitaje hizo hatua ilizokachukua serikali na tukafanikiwa kuizima covid katika Corona Phase 1 na ambazo hamjaambiwa kuchukua kwenye Corona phase 2?
 
Embu zitaje hizo hatua ilizokachukua serikali na tukafanikiwa kuizima covid katika Corona Phase 1 na ambazo hamjaambiwa kuchukua kwenye Corona phase 2?
Rudia tena kusoma, kama huelewi hilo ni tatizo lako wewe binafsi.

Wewe mtu binafsi una uwezo wa kufunga mashule ili watoto wasiende huko wakaambukizana na kuuleta ugonjwa nyumbani?
 
Hatuzungumzii lockdown, tunazungumzia measures za kawaida za serikali kudhibiti spread ya kirusi hiki
Zakawaida zipi ??? Mheshimiwa misaili,labda uziweke hapa tuzitafakari na kila Mtanzanaia ataona Mheshimiwa usibanie unachokijua na kuona kitafaa labda serikali imeghafilika.
Angalizo :Siku serikali ikisema atakaekamatwa hajavaa barakoa atapigwa faini shilingi 50000/ mtarudi hapahapa na kusema serikali kandamizi
 
Back
Top Bottom