Masanja Mkandamizaji: Mimi ni mchungaji, lakini Mbinguni ng'o sitaki kwenda

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Emmanuel Mgaya, maarufu kama "Masanja Mkandamizaji" aliyejizoelea umaarufu katika fani yake ya uchekeshaji na kundi lake la "Ze Comedy" kwa sasa amegeukia kazi ya ushehereshaji na Uchungaji.

Katika moja ya Kazi yake hivi karibuni Masanja akiwa MC ktk tukio fulani alitoa mpya baada ya kuwashangaa waimbaji wa Kigali-Rwanda wa kwaya ya "AMBASSADOR OF CHRIST" ambao walipata ajali wakiwa wanatokea Tanzania.

Masanja anasema inakuwaje waliomba kifo kwa wimbo wao wa "KWETU PAZURI" lkn Mungu alipowachukuwa baadhi ya wenzao wale waliobaki wakaimba wimbo wa "KWANINI UMEYARUHUSU HAYA" yaani kwanini kawachukua wenzao?

Masanja anasema Kwanini washangae wakati wao ndio waliomba kwenda "kwao pazuri walipopakumbuka? Kwao hakuna malaria wala magonjwa".

Masanja anasema yeye hataki kabisa kwenda Mbinguni kwa sasa, bado yupoyupo.

Msikilize hapo;
 
Hii video ipo miaka mingi na sio habari mpya. Kwanza sijawai sikia wapi ambassadors of christ wameimba wanataka kufa.

Pili wimbo wa kwanini wengi waliu overlook meaning na kile waliimba kwa ujumla.

Mwisho hawa nao wameishiwa saizi hawana mpya mara 1000 futuhi
 
Emmanuel Mgaya, maarufu kama "Masanja Mkandamizaji" aliyejizoelea umaarufu katika fani yake ya uchekeshaji na kundi lake la "Ze Comedy" kwa sasa amegeukia kazi ya ushehereshaji na Uchungaji.

Katika moja ya Kazi yake hivi karibuni Masanja akiwa MC ktk tukio fulani alitoa mpya baada ya kuwashangaa waimbaji wa Kigali-Rwanda wa kwaya ya "AMBASSADOR OF CHRIST" ambao walipata ajali wakiwa wanatokea Tanzania.

Masanja anasema inakuwaje waliomba kifo kwa wimbo wao wa "KWETU PAZURI" lkn Mungu alipowachukuwa baadhi ya wenzao wale waliobaki wakaimba wimbo wa "KWANINI UMEYARUHUSU HAYA" yaani kwanini kawachukua wenzao?

Masanja anasema Kwanini washangae wakati wao ndio waliomba kwenda "kwao pazuri walipopakumbuka? Kwao hakuna malaria wala magonjwa".

Masanja anasema yeye hataki kabisa kwenda Mbinguni kwa sasa, bado yupoyupo.

Msikilize hapo;

Wee wachekeshe watacheka ila mwenye mbingu yake amekusikia na lbilisi kesha libeba hilo ukumbuke tu NENO LINAUMBA.
 
Hivi kile kipindi chao TBC nowdays hakipo au!? au Mzee wa hapa.kazi.tu kafanya mambo!? Siwasikii tena!
 
Frankly speaking sipendi jinsi ambavyo Masanja anatumia nafasi ya Uchungaji vibaya.

Ingekuwa sahihi kwake kuokoka na kubaki kuwa comedian lakini kujinasibu yeye ni Mchungaji hanibariki kabisa.

Mashabiki wa Masanja mwambieni madhara ya kutumia Ukuhani kufanya biashara ni anguko kubwa.
 
Masanja Mkandamizaji ni mchekeshaji.....nitawashangaa wanaoenda kusikiliza neno la Mungu kwake waongolewe badala ya kusikiliza vichekesho
 
Nyie wenzetu dini yenu ya mzaha sana yaani mpaka masanja ghafla kawa mchungaji lol
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom