Masanja acha kulitukanisha jina la Bwana Yesu kwenye majukwaa ya wamataifa

Jun 17, 2020
75
268
Habari wakuu!

Wokovu sio Bwana asifiwe, Wokovu ni maisha mapya! Ni mabadiliko anayoyapata Mtu baada ya kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake( Yohana 1:12)

Masanja mkandamizaji ww ni mchungaji kitendo cha ww kwenda kucheza jukwaa moja na wasanii wa bongo fleva na wengine! Bado humjui Yesu wewe upo kwa ajili ya tumbo! Mambo yafuatayo yanakuondoa kwenye Sifa ya kuitwa mchungaji wa kiroho:

1: Unapookoka unakuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya (wewe umerejea ya zamani)

2: Ukiamua kuwa baridi kuwa baridi na ukiamua kuwa moto kuwa moto (wewe upo potepote)

3: Ukiamua kumtumikia Mungu jikane nafsi yako (wewe bado hujajikana bado nafsi yako inapenda vya Misri)

4: Ukiwa mtumishi wa Mungu Yale yote yanayoonekana kuwa mazuri kwako inabidi uyahesabu kuwa ni hasara na mavi ili umpate Kristo (kwako hii ni tofauti)

4: Wewe ni mchungaji wa kundi la Mungu lenye itkadi za vyama vyote, unaposimama jukwaani kunadi chama kimoja wewe sio tena mtumishi wa Mungu Bali wewe ni mtumishi wa CCM.

5: Mtumishi wa Mungu ni kukemea maovu sio kuegemea kwenye chama kimoja! Unataka kutuambia kuwa CCM ndo chama ambacho hakina maovu? Na vyama vingine vina maovu.

6: Wale wasanii wote uliokuwa nao pale Dodoma wanamhitaji Mungu na wanahitaji mafundisho ya kuwabadilisha, ni kitu gani utakachowahubiria cha tofauti ikiwa mnakata mauno pamoja majukwaani?

6: Je, ni kweli kwamba upinzani wakikualika kwenye majukwaa yao utaenda? Maana ww ni mtumishi wa Mungu na Mungu ni wa wote! Kama hautaenda huoni kwamba ni double standard?

7: Unapokisifia chama kimoja jaribu pia kukemea waziwazi maovu yanayofanywa na chama hicho kwa sababu ww ni mtumishi wa Mungu!

8: Jua kwamba wewe una kazi kubwa ya kufanya kwenye Nyumba ya Mungu, najua unafanya vyote hivyo kwa sababu ya pesa (huwezi kumtumikia Mungu na huku unapenda dunia)

10: Huwezi kumtumikia Mungu na Mali ukiamua kutafuta pesa lazima utamuacha Mungu tu huo ndo ukweli (rejea mafundisho ya Yesu, ukiwa na mavazi na chakula ridhikeni na hivyo)

Note: Mbingu sio lele mama kama wengi wanavyofikiri, kuuona ufalme wa Mungu ni gharama inabidi hata kifo sio wachungaji wa sasaivi wanaotetea matumbo yao, hawapo tiyari kukemea na kuonya maovu ila wapo tiyari kupongeza tu!! Nawapa mifano michache ya watu waliokemea maovu hadharani kwa ajili ya ufalme wa Mungu hawakuogopa kifo wala hawakutaka heshima Kutoka kwa wakuu! (Yohna mbatizaji, Petro, Paul, Stefano, Mikaya, Yeremia, Daniel, Yusuph, moses, Yeremia, Samweli, nk) wachungaji wa sasa jipimeni kwa viwango vya hawa watu nyie mpo wapi? (Masanja acha kulitukanisha jina la Yesu kwenye majukwaa ya wamataifa)

NB: Nampongeza sana mbrakiwa Mwakipesile, ni moja ya wachungaji pekee hapa Tanzania wenye uthubuthu wa kukemea maovu kwa watawala! Haogopi cha nabii, mtume, mchungaji nk maadam unaenda kinyume na neno la Mungu!
 
Mama yangu mzazi huyu jamaa ni muongo zaidi ya shetani.

Janja janja hyu nyenganyenga.

JamiiForums-1793627352.jpg
 
Umeandika thread ndefu umepoteza muda wako kufanya mambo yako ya maana.
Kifupi huyo Masanja anawakilisha version mpya ya so called walokole wa kisasa.
Hayaeleweki yana mtangaza Yesu gani ,cha muhimu kwao ni wallets zao zitune bhasi.
 
Back
Top Bottom