Masalia yaliyobaki CHADEMA ni wapi?

scatter

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,615
2,000
Wakuu ni kwa wenye akili zao tu:

Tukiwa tunaelekea katika hatua ya kushindana katika kuchukua nchi hapo mbeleni LAKINI kwa moyo wa dhati kuna watu wanatakiwa kutoka na kuteua watu wengine zaidi ya waliosimamishwa kwani huenda wakarudi kwani sasa CHADEMA NI CHAMA CHA WANANCHI!
JE NI KINA NANI NA KWA SABABU GANI
 

mary mary

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
869
0
kuwa washindi katika uchaguzi si kazi ...kazi ni kuongoza nchi katika mustakabali wa maendeleo hapo kuna hitaji umakini kwa kweli!

Hao walioongoza wamefanya nini zaidi ya kudharau, kuwadidimiza wananchi na kuweka pesa nyingi mifukoni mwao? inabidi tujaribu tofauti hatuwezi kung'ang'ania kubaki sehemu moja miaka zaidi ya 50, huo ni umaskini, uwoga na ujinga unatakiwa kuondoshwa kwa nguvu. Watanzania acheni uwoga inabidi tuwafundishe vijana wetu ujasiri kwa faida ya Tanzania Ijayo iliyo Imara.
 

scatter

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,615
2,000
Hao walioongoza wamefanya nini zaidi ya kudharau, kuwadidimiza wananchi na kuweka pesa nyingi mifukoni mwao? inabidi tujaribu tofauti hatuwezi kung'ang'ania kubaki sehemu moja miaka zaidi ya 50, huo ni umaskini, uwoga na ujinga unatakiwa kuondoshwa kwa nguvu. Watanzania acheni uwoga inabidi tuwafundishe vijana wetu ujasiri kwa faida ya Tanzania Ijayo iliyo Imara.

uyasemayo ni kweli kwa hali ilivyo MABADILIKO NI MUHUMU lakini tuna uhakika wa kufika huko tuendapo bila kuchunguza wadhaifu na kuwatoa kwa manufaa ya taifa na chama pia kwani MIAKA MITANO KWA CHADEMA KUJA KUONGOZA NCHI NI MINGI
 

mary mary

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
869
0
uyasemayo ni kweli kwa hali ilivyo MABADILIKO NI MUHUMU lakini tuna uhakika wa kufika huko tuendapo bila kuchunguza wadhaifu na kuwatoa kwa manufaa ya taifa na chama pia kwani MIAKA MITANO KWA CHADEMA KUJA KUONGOZA NCHI NI MINGI

Kuchunguza madhaifu ni muhimu usiwaige CCM hao madhaifu yao yameoza ikitokea uka-scan hakuna atakayebaki...ili mgonjwa awe na afya njema inatakiwa dawa ya kudhibiti ugonjwa ule....huwezi kufanya kazi na wadhaifu mkafika salama. Inabidi waondolewe hata wakibaki wachache lkn mkiwa katika direction moja MABADILIKO yatatokea. Haitakiwi watu maelfu kukomboa nchi....
 

scatter

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,615
2,000
Kuchunguza madhaifu ni muhimu usiwaige CCM hao madhaifu yao yameoza ikitokea uka-scan hakuna atakayebaki...ili mgonjwa awe na afya njema inatakiwa dawa ya kudhibiti ugonjwa ule....huwezi kufanya kazi na wadhaifu mkafika salama. Inabidi waondolewe hata wakibaki wachache lkn mkiwa katika direction moja MABADILIKO yatatokea. Haitakiwi watu maelfu kukomboa nchi....

ok nadhani tupo pamoja
 

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Ukiangalia vituko na hekaya zinatotengenezwa na wanaMaCCM wakisaidiana na kundi la Masalia, Mabadiliko 2013 chini ya Jemedari wao mzee wa kuuwa panya, utaamini hii picha ilianzwa kuchezwa siku nyingi sana.

Timming ya CDM ndio pona yake. ZZK na kundi lake waliandaliwa waanzishe kasheshe ya kushikana mashati mwakani somewhere june, mpango huu chini ya Wassirra, Mwiguluu, Nchimbii, na baadhi ya vijana wa kazi ulisukwa kwa kutumia mambo kadhaa.

Mosi kuichafua CDM kwa ugaidi, udini, ukanda na ukabila. Pili kwa kuwatumia kina ZZK na kundi lake kutengeneza mitafaruku huku wakisaidiwa na Viongozi wa mikoa wa CCM kama inavyotokea leo huko Kigoma. Mipango hii ilivurugika kwasababu hata ndani ya MaCCM wengi hawapendi jinsi serikali inavyoendeshwa.

Wapo wanaCCM wenye akili timamu wanaelewa na wameona umuhimu wa uwepo wa CDM kwenye siasa za kizazi cha sasa. Check and balance imeasaidia sana kuokoa fedha nyingi za kodi zisipotee na walau watendaji kuanza kuhisi ile hali ya uwepo wa wapiga kura.

Leo hii kuvutisha vijana bangi na kuwalewesha gongo ili wakuteteee urudishiwe cheo au usichuliwe hatua kwa makosa uliyotenda, wakati umepewa muda na sehemu ya kujitetea ili haki itendeke ni uhayawani mkubwa sana.

Kwa yanaoyotokea sasa, CDM imejikuta kwenye three fronts line, wapambane na kundi linaloasisiwa na Zana za Kilimo na Masalia co. Pili Ipambane na MaCCM ambao wanaona karibu wanatoka roho, Tatu ipambane na serikali ambayo inatumia fedha za kodi chini ya usalama wa taifa kupambana na CDM. Makundi haya matatu yameungana kupambana na CDM ili kuidhoofisha kuelekea 2015.

Umuhimu wa 2015 naomba wananchi wajue sio wa kiongozi yeyote yule wa chama cha siasa bali sisi wananchi ambao ndio waathirika wakubwa sana wa mfumo huu uliopo. Mfumo unaoogopa kuwajibisha watu, mfumo mfu ndio maana leo pamoja na ZZK na kundi lake kukiri makosa yao na kuchukuliwa hatua bado wapo wanaona kaonewa, Kweli leo katiba ikifuatwa ni kuonea mtu? Uhuru bila mipaka ni fujo, cheo bila maadili ni ufisadi, kazi bila uwajibikaji ni uvuvi.

Ni lazima kuiondoa serikali iliyopo madarakani ili kutengeneza ushindani wa kweli na kujenga uwajibikaji chini ya sheria na katiba. Lazima kutoa umangimeza na usultani uliopo wa madaraka. Lazima kuwaondoa hawa ambao tayari wamelewa madaraka. Leo wanaoleta fujo CDM tayari wameshiba, wamekula fedha zetu, kodi zetu na uaminifu wetu. Kwanini wao hawataki nasi tukaiona Tanzania mpya? Sisi wananchi tunahitaji mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kimfumo.

Ili tuendelee lazima ushindani uwepo, na ushindani huu ni lazima tuuweke vipimo na uwezo wa kuwashindanisha watawala wetu wakijua kwamba wanaweza kupoteza nafasi zao wananchi wakiona hawafai.

Freeman Mbowe Mwkt wa CDM "tunapokaribia ikulu visa vitaongezeka, mateso yataongezeka, wasaliti watajikoze, serikali ya CCM itatumia fedha nyingi sana kujaribu kushinda, uaminifu wa wengi utakuwa-tested na wingi wa fedha chafu zitakazomwagwa kushawishi wale wote tishio kwa uwepo wa CCM madarakani, ni wale jasiri na uzalendo wa ukweli ndio watavuka hivi vizingiti." hiyo ni kauli kamanda wa anga mwaka na nusu uliopita. Leo yanatokea.

Kwa ushirikiano wa kila mpenda mabadiliko chanya tutashinda.

Chief Mkwawa
Mjerumani na vibaraka wake walishindwa kuniuwa-kakamatwa na adui ni unyonge-wote waliokamatwa kwa vipande vya fedha wamesaliti utu wao.
 

simbilisi

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
792
0
tatizo ni mbowe na si zito au masalia

apiseh wengine

haiwezekani chairman wa chama at the same time ni procurement officer
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom