Masalia ya Zitto yapukutishwa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masalia ya Zitto yapukutishwa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 6, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Alfred Lucas
  Imechapwa 01 June 2011
  CHANZO: Gazeti la MwanaHalisi

  KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ililazimika kujigeuza mahakama ili kusikiliza malalamiko dhidi ya wagombea nafasi ya uenyekiti wa baraza la vijana la chama hicho (BAVICHA).


  Katika kusikiliza malalamiko hayo, Kamati Kuu iliwateua wanasheria wake mashuhuri, Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari kuwa majaji wa kuendesha kesi ya Habibu Mchange aliyekuwa anawania nafasi ya mwenyekiti.


  Mchange ambaye anajitambulisha kuwa ni mfuasi wa naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe lilalamikiwa na mwenyekiti wa BAVICHA mkoani Mwanza, Liberatus Mlebele kukiuka maadili ya uchaguzi, ikiwamo kusafirisha wajumbe wa mkutano wa uchaguzi kutoka mikoani hadi Dar es Salaam.


  Ndani ya CC, Mchange alilazimika kujibu tuhuma moja baada ya nyingine ikiwamo malalamiko ya kushindwa kuwajibika yaliyofunguliwa na katibu wa BAVICHA jimbo la Kigamboni.


  Katibu huyo alimtuhumu Mchange kushindwa kutimiza wajibu wake kwa kile alichoeleza, "Tangu achaguliwe kushika nafasi ya mwenyekiti wa BAVICHA wilayani humo hajahudhuria vikao."


  Mjumbe mmoja wa CC amedokeza gazeti hili kuwa Mchange ambaye alionekana kuwa na wafuasi wengi, alikatwa kwa kuwa alishindwa kujitetea mbele ya mahakama ya CHADEMA.

  Kwa mfano, kati ya 20 Mei na 25 mwaka huu, Mchange alituma zaidi ya Sh. 2, 561,000 kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa vijana kutoka katika mikoa mbalimbali nchini. Fedha hizo zilitumwa na Mchange mwenyewe kupitia mtandao wa M-Pesa na Tigo Pesa.


  Namba ya Mchange iliyotumika kusambaza fedha hizo, ni 0658 178678. Alianza kutapakanya fedha kwa wajumbe 11 Mei 2011 saa 10:44.58 ambapo kiasi cha Sh. 28,500 zilitumwa kwa mmoja wa wajumbe wenye simu Na. 0659 374206.


  Baadaye saa 11:04.24 alituma Sh. 15,500 kwenda Na. 0659 374206 na kisha 20 Mei 2011 saa 14:03.04 alituma Sh. 19,000 kwa mwenye Na. 0713 866650.


  Tarehe 23 Mei 2011 saa 10:56.06, nyaraka zinaonyesa Mchange alituma Sh. 50,000 kwenda kwa mwenye Na. 0713 867745; tarehe 21Mei 2011 saa 11:54.47 alituma Sh. 40,000 kwenda kwa mwenye Na. 0717 268576 na saa 12:41.48 alituma Sh. 81,000 kwa mwenue Na. 0714 038536.


  Wengine waliotumiwa fedha na Mchange; ni wenye Na. 0712 511508 aliyetumiwa Sh. 26,000 na mwenye Na. 0713 606169 aliyetumiwa Sh. 10,000 ambaye alitumiwa fedha hizo, saa 22:24.31.

  Nyaraka za M-PESA zinamuonyesha Mchange akimtumia Peter Shiyo, mwenyekiti wa BAVICHA wilayani Maswa Sh. 50,000. Fedha hizo zilitumwa 23 Mei 2011 saa 16:39.

  Tarehe hiyo 23 Mei 2011 saa 18:48, Mchange alituma kiasi cha Sh. 30,000 mwenyekiti wa vijana wilaya ya Singida Mjini, Wilfred Kitundu.


  Aidha, siku hihiyo Mchange akitenda kama karani wa benki alituma Sh. 150,000 kwa mwenyekiti wa baraza hilo mkoani Mwanza, Liberatus Mlebele.


  Mara baada ya kupokea fedha hizo, Mlebele aliwasilisha malalamiko kwa katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa akimtuhumu Mchange kumshawishi kwa njia ya rushwa ili amchague kuwa mwenyekiti.


  Katika barua yake hiyo, Mlebele pamoja na mambo mengine alisema, "Ninakuandikia kwa nia njema kabisa ya kulinda hadhi ya chama chetu nikiomba maelekezo yako kama mtendaji mkuu wa chama."


  Anasema, "Tarehe 28 Mei 2011 Baraza la Vijana wa chama chetu litafanya uchaguzi wa viongozi wake wa kitaifa. Je, sisi wajumbe tumegharamiwa na chama ama wagombea kufika Dar es Salaam kwa ajili ya uchaguzi huu?


  Alisema, "Ninauliza hivi kwa sababu tayari mmoja wa wagombea ameshaniagiza kufika Dar es Salaam kwa gharama zake ili kukagua hoteli ambayo wajumbe wa mkoa wangu na kwingineko watafikia hali ambayo ninaihesabu kama rushwa."


  Mlebele alisema katika barua yake, "Niko tayari kutoa vielelezo sahihi juu ya kitendo hiki kama itabidi, ili kulinda hadhi ya chama chetu dhidi ya watu hatari kama hawa."


  Alisema, "Kwa kuwa mimi binafsi sipendi rushwa na siwezi kuvumilia vitendo vya rushwa na kwa kuwa natambua chama chetu kimekuwa kinara wa kupambana na rushwa nchini, ninaomba kamati kuu ichukue hatua stahiki dhidi ya mtu huyu ili kulinda hadhi ya baraza na chama chetu mbele ya wananchi."

  Ni maelezo hayo ya Mlebele yaliyozika ndoto za Mchange kuwa mwenyekiti wa BAVICHA. Taarifa zinasema Dk. Slaa aliwasilisha malalamiko yote mbele ya wajumbe wa CC. Barua ya Mabele iliwasilishwa kwa Dk. Slaa, 26 Mei 2011.


  Taarifa zinasema kabla ya CC kujigeuza mahakama ya kusikiliza shauri hilo, mjumbe mmoja alinukuliwa akimtetea Mchange. Hata hivyo, alizimwa na Dk. Slaa aliyesimama kidete kutaka chama chake kichunguze suala hilo na kichukue hatua.


  Katika barua yake, Mlebele anasema alifikia katika hoteli ya Bondeni One iliyoko Magomeni. Anamtaja Mchange kuwa ndiye aliyelipa fedha hizo. Alitoa nakala ya kitabu cha wageni kuthibitisha kuwa fedha hizo zililipwa na aliyemteja.


  Mchange alikiri mbele ya wajumbe wa CC kuwa ni kweli kwamba simu iliyotajwa kupeleka fedha ni yake; alimhonga Mlebele kiasi kilichotajwa, alilipia sehemu ya gharama za hoteli na alikiri kumuagiza akusanye wajumbe wa mkutano wa uchaguzi.


  Kamati kuu ya CHADEMA ilipitisha majina ya wagombea tisa katika nafasi ya mwenyekiti na kisha kukasimu madaraka yake kwa kamati ya wazee kwa hatua nyingine inazoona zinafaa.


  Ni kupitia kamati hiyo, ndiko wagombea wengine watatu walifyekwa. Waliopatwa na panga la kamati hiyo iliyokuwa chini ya Edwin Mtei, Bob Makani na mwanasheria wa chama hicho, Mabere Marando, ni Mtela Mwampamba, Bernard Saanane na Grayson Nyakarugu, huku John Heche akionywa na na kuelezwa ikibainika alifanya vitendo kinyume cha maandili, atavuliwa madaraka.

  Wote waliokatwa walipatikana na makosa ya rushwa, kutoaminika, kupanga matokeo, makundi na kutumiwa na watu wa kutoka nje ya baraza la vijana.

  Akifanya marejeo ya kilichofanyika Jumamosi katika uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa PTA Sabasaba, Temeke, jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa alisema chama chake kimeweza kunasua mitego yote ya rushwa iliyopandikizwa na CCM.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  khaaaa! Sasa CCM mambo kama haya hawawezi kuyafanya jamani? Why wanakosa ujasiri?
   
 3. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35

  Duh! hawa viongozi watarajiwa wananjaa kali namna hiyo? wote walimeza hizo ndogo ndongo kasoro yule wa Mwanza ambaye Heche alikuwa amempa nyingi zaidi ya hiyo kilo unusu ya Mchange.Hawa wakishika dola si watauza mpaka shule za kata hawa!!!!!!!!!!!
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  nngu007,

  Mkuu unajua waandishi wetu uchwara ni watu ambao hawakwenda shule kusomea habari, kwani huwezi kusema Uongozi wa Chadema umejifanya mahakama wakati swala linaloshughulikiwa ni la chama na uongozi wa Bavicha. Ni sawa na kusema JK hakuwa na mamlaka ya kubadilisha Sekretariet ya chama pasipo kupitia mahakamani..

  Swala la Takrima limechukuliwa kama ni rushwa na mgombea yeyote awe wa chama au Mbunge ktk hatua za mwanzo za uchaguzi anaweza enguliwa ktk uchaguzi huo kufikishwa mahakamani na tumewaona wengi tu ndani ya chaguzi za CCM na vyama vingine wakienguliwa ndani ya chama na hakuna mtu alodai watuhumiwa wafikishwe mahakamani ili HAKI - sijui ya nani ipatikane..

  Kisha ningependa sana kujua kwa nini Mchange anahusishwa sana kuwa mfuasi wa Zitto ili hali Zitto alijitoa mapema kabla ya uchaguzi na kusema hamshabikii mtu yeyote!..Iweje leo bado tu mnasema Mchange ni chaguo la Zitto ni kwa sababu zipi?

  Na vipi kama Chaguo la Zitto lilikuwa Seleman, Ben au Heche mwenyewe? najiuliza tena kama Mchange alikuwa chaguo la Zitto kabla ya uchaguzi, je huyo Heche ni chaguo la nani na kwa nini amechaguliwa?
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Mkuu ulienzisha hii thread huna kazi ya kufanya? Hii ni habari ya gazeti la mwanahalisi la jumatano iliyopita wewe unaileta hapa jamvini? watu hapa tuko up to date tunataka hot news na sio habari ambayo imeshaexpire.
  Au ndio unajifunza copy & paste?
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wataumbuka mmoja baada ya mwingine.
   
 7. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Wakuu;
  Nimepata kutambua kuwa CHADEMA hasa ni mali ya WACHAGA na ili ukubalike ni lazima uungwe mkono na mtu na mkwe wake..(MBOWE na MTEI) AMBAO WAKIKUTAA WATAKUUNGANISHIA KILA AINA YA SHUTUMA.
  Kwa mfano nimeipitia kwa karibu TAARIFA wanayosema MCHANGE amewatumia pesa wajumbe wa BAVICHA na kugundua ni uzushi umetaawala kwani Transaction inaonyesha MCHANGE ametumiwa pesa nyiongi kuliko kutuma na hata aliowatumia wengi wao ni ndugu zake japokuwa KUBENEA anataka kuulazimisha UMMA uamini kuwa MMCHANGE HAKUONEWA.
  Ukweli ni kwamba ilikuwa ni lazima mchange aenguliwe kwenye auchaguzi ULE KUTOKANA NA SABABU ZIFUATAZO.
  1.SIO MCHAGGA
  2.SIO MKATORIKI(yeye ni muislam)
  3.HABURUZIKI KIRAHISI
  4.ANA MSIMAMO MKALI
  5.ALISABABISHA KUSHINDWA KWA KWA KISHINDO na kura zao walizopata kwenye mabano KWA; GRACE KIHWELU(kura 3), REGIA MTEMA(kura 1), SUZAN LYOMO(kura 9), HALIMA MDEE(kura 7) NA WACHAGGA WENGINE kwenye uchaguzi wa viti maalum kwa kuwapigania wanawake masikini wa vijijni mpaka MBOWE AKAUFUTA akaenda kuwateua tena MABIBI ZAKE.
  KWA HIYO SASA;
  Ndio maana hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 wakati MCHANGE akigombea KIBAHA MJINI mchango pekee aliopewa na CHADEMA ni shilingi laki tano tu(500,000/=) tena siku tatu kabla ya kampeni kuisha huku wakitaka kutompeleka SLAA jimboni mwake mpaka walipogundua kuwa MCHANGE ana nafasi kubwa ya kushinda ndipo wakampeleka SLAA saa nne Asubuhi wakati jimboni kwa JOHN MREMA aliyepata ASILIMIA SITA ya kura zote SLAA alipelekwa vijiji vyote.
  Na hata alipofungua kesi ya uchaguzi kupinga matokea CHADEMA ilikataa kumchangia hata mia na kumwachia mwenyewe mzigo wote huku ikimlipia million 15 FRED MPENDAZOE.
  Katika hili sasa ilikuwa ni lazima mchange aenguluwe kwani USHAWISHI NA UFUASI WAKE NDANI YA CHAMA ni mkubwa mno kiasi kwamba dawa pekee ya kupatia HECHE ushindi ni kumuengua na ndio maana wakamuandaa MLOKOLE kutoka mwanza aliyejifanya anaomba msaada kuwa anauguliwa sana na mke wake hivyo anaomba msaada, hata baada ya kusaidiwa kwa namba nyingien akadai hakupata pesa mpaka akalazimisha atumiwe kwa namba yam change KUMBE ALIKUWA NA LAKE JAMBO.
  Cha kushangaza sasa kama kweli kuna rushwa basi wa kushtakiwa ni GODBLESS LEMA aliyemlipia TIKETI ya ndege huyo mlokole hadi DSM kuja kumchinja mchange na hata wakati mchange anaingia kuhojiwa na Kamati kuu MNYIKA lisikika akisema ‘’UNACHINJWA LEO’’ HII NI HATARI SANA.
  UIMARA wa MCHANGE ulidhihirika pale alipoamua kumuunga MKONO MTELA MWAMPAMBA kiasi cha kumfanya HECHE kufunga safari usiku usiku wa MANANE mpaka BILLCANAS kumlilia MBOWE kuwa bado kazi inaendelea sababu mchange kahamishia majeshi yake kwa MWAMPAMBA ndipo MBOWE akamwahidi kuwa atahakikisha anawaondoa wote ikiwezekana apite bila kupingwa.
  Ndio maana PADRI aliyefukuzwaDkt Slaa alipata aibu ya mwaka pale alipowaambia wajumbe kuwa MWAMPAMBA, GRAYSON, SAA NANE na HECHE wanamakosa ya rushwa na kupokea wageni na kufanya vikao isivyo halali mara tofauti tofauti lakini MWAMPAMBA, GRAYSON na SAANANE wanaenguliwa HECHE yeye anakwenda kujadiliwa kamati kuu; Hapa ndipo wajumbe wa vijana wakagundua kuwa sasa HECHE anabebwa na MBELEKO YA CHUMA.
  Nampongeza sana mchange kwa kuwa jasiri na kutokutetereka; MUNGU ATAWAUMBUA WOTE WANAOTUMIA MWAVULI WA RUSHWA KUFANYA DHURUMA DHIDI YA HAKI…
  USHAHIDI WA YOTE HAYA UPO NJIANI WAJA…
  MCHANGE WEWE NI SHUJAA;-KEEP IT UP.
   
 8. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Na bado mpaka mkome.... chama aanzishe Mtei na mkwewe Mbowe ninyi wa kuja Mchange, Zitto et al mje mchukue madaraka!. Mta enguliwa tu......
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu habari sio tarehe habari ni article yenyewe nyinyi labda mliiona Jumatano hakuona umuhimu wake, sisi kwa bahati mbaya hatupati habari muhimu kiurahisi sababu ya nchi yetu tunayoipenda haina technolojia ya kuweza kusambaza habari hama hizi duniani kote

  Bahati mbaya mimi siko TZ lakini baada ya kuona hii habari kwangu mimi naona ina umuhimu kwa jinsi chama fulani kinapinga ubwanyenye na ulafi wa madaraka wakati chama kingine kimekumbatia mantiki hiyo...
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mkandara

  As you know Journalism is Organized Gossip, junk is the evidence of a society that has got at least one thing right, that there should be nobody with the power to dictate where responsible journalism begins...

  To my Understanding Exaggeration of every kind is as essential to journalism as it is to dramatic art, for the object of journalism is to make events go as far as possible...   
 11. m

  ma'name New Member

  #11
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh hii ndo Sihasa
   
 12. Mkenazi

  Mkenazi Senior Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hizi habari za zamani, tunataka za 2012.
   
 13. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kuna watu wanataka kushusha hadhi ya JF, haiwezekani mtu anaibua vitu ambavyo vilitokea kitambo mno.
   
 14. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  dah kweli ruswa hizi eti cdm wapinga mafisadi kumbe wao ndo wako mstari wambele kuendekeza rushwa
   
 15. e

  ednjou Member

  #15
  Mar 27, 2013
  Joined: Mar 4, 2013
  Messages: 31
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Tujipange jamani ukombozi wa taifa sio kazi ndogo...
   
 16. A

  Adam Nkiko New Member

  #16
  Mar 27, 2013
  Joined: Mar 10, 2013
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa ndio wanaopinga ufisadi jamani
   
 17. Richard Mlangi

  Richard Mlangi JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2013
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 380
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Zitto ana mkakati gani ?
   
Loading...