Masaibu ya members wa JamiiForums

Masaibu ya members wa JamiiForums

Yaani miongoni mwa mitandao ya kijamii yenye impact kubwa kwenye jamii naweza kusema jamii forum ni no1.

Tatizo linaanzia kwa member wake..
Yani humu jamii forum bana kila mtu ana PHD.
Kila mtu ameshakwenda marekani Russia na Ukraine...

Yaani jamii forum kila mtu ana nyumba zaidi ya Moja na anaviwanja goba.

Yaani jamii forum kila mtu ana degree

Yani jamii forum kila mtu ana pesa Ila ajui afanye biashara Gani tena zaidi ya 100m

Yaani jamii forum kila mtu ni daktari na anajua kwa undani masuala ya afya

Kila mtu jamii forum ni mchambuzi wa kisiasa duniani

Yaani jamii forum kila mtu amewai kusafiri mikoa yote.

Kifupi jamii forum wajuaji ni wengi mtu unaweza kuhisi upo nyuma kimaendeleo kwa sababu watu wanaandika kama mabilionea.

Yani jamii forum kila mtu ni tajiri aisee..
Alafu jamii forum Tabaka la chini ni wahitumu wenye degree ndio wanaonekana mabwege

Aisee ni hatari sana.
Yani kuna watu wanasubiri uweke mada waje wajifanye waaguzi, ubishi, majitu ni majuaji🤣 mkute alipokaa na anaandika hiyo comment utachoka. Kuna mmoja niliwahi kukutana nae na mambo anayoandika humu ni aibu. Kuna siku nikaweka mada akaja kupinga.
Nikabaki nacheka kwasababu hali yake na anayoyapinga ni huruma🤣

Jamii forum mtupumzishe jamani na hapo bado hujakutana na wale wa kukatisha wenzao tamaa. Unakuta mtu anakwambia una milioni 30? Hakuna biashara ya kuanzisha hapo huwezi kutoboa🤣 unatamani umnase mtu kofi
 
Back
Top Bottom