GE2025 Masache Kasaka ashinda kwa kura 5,572 jimbo la Lupa, Chunya

GE2025 Masache Kasaka ashinda kwa kura 5,572 jimbo la Lupa, Chunya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428

MASACHE KASAKA ASHINDA KWA KURA 5,572 JIMBO LA LUPA, CHUNYA

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Lupa, Masache Njelu Kasaka ameibuka kidedea kwenye kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Lupa akipata kura 5,572 huku akiwaacha mbali washindani wake.

Masache amepata ushindi huo dhidi ya washindani wake watatu akiwamo Noel Ntangu aliyepata kura 2,821, Geoffrey Mwankenja (2,115) na Sarah Sampo (143).

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chunya, Charles Jockel ameeleza kwamba uchaguzi huo umekwenda vizuri katika Kata zote 10 zilizopo katika jimbo hilo.
 

Attachments

  • Screenshot 2025-08-06 at 15-55-55 Instagram.png
    Screenshot 2025-08-06 at 15-55-55 Instagram.png
    610.7 KB · Views: 15
Back
Top Bottom