Masaburi na idi simba nao ni magamba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masaburi na idi simba nao ni magamba?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mohamedi Mtoi, Aug 14, 2011.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kada maarufu wa CCM aliye wahi kuwa mbunge na waziri wa viwanda na biashara Mh Iddi Simba pamoja na kada ambae pia ni Mayor wa jiji la DsM Mh Didas Masaburi CcM wamejikuta wakianguka kwenye tope la kashfa ya ufisadi kwa kuuza shirika la usafiri Dar es salaam (UDA).

  Wakati hayo yakitokea chama chao kipo kwenye mkakati mzito uliobeba dhana ya kujizua gamba ili angalau kurejesha imani kwa wananchi dhidi ya chama hicho kilichogubikwa na kashfa lukuki za kifisadi ambazo zimelitikisa taifa. Taja Richmond, Epa, Kagoda, Meremeta, mikataba mibovu ya madini, Tangold na uhongaji kamati au wabunge ili kupitisha bajeti ya wizara zao.

  Viongozi kadhaa wa CcM akiwemo Nape Mnauye walishanadi kuwa wenye tuhuma za ufisadi lazima wajivue gamba lakini wakisema hayo huku macho yao yakiwakodolea mapacha watatu tu. Hapa ndio napata tabu, kama chama kimegubikwa na mifumo ya kifisadi je magamba ni mapacha watatu tu? Na vipi kuhusu hili sakata la UDA, wahusika nao ni miongoni mwa magamba ndani ya mifumo ya chama cha mapinduzi?
   
Loading...