Masaa 58 bila Umeme na bado tunasubiri

Biobenga

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
394
533
Naandika huu uzi kwa masikitiko makubwa. Nadhani kero zinazotokana na ukosefu wa umeme zinajulikana, hivyo nitaelezea tatizo kwa ufupi kadri nitakavyoweza.

Umeme ulikatika Jumamosi saa 12 asubuhi. Jioni niliwasiliana na kitengo cha dharura TANESCO nikapewa taarifa kuwa transfomer ya karibu imeibiwa mafuta lakini tatizo wanalishughulikia.

Jumamosi ikapita bila umeme na jana jumapili pia ikapita bila umeme. Leo Jumatatu alfajiri nikapiga simu tena nikajibiwa kuwa mafuta yamepatikana na yatawekwa asubuhi ya leo.

Mpaka hivi sasa saa kumi, hakuna dalili zozote.

Je, hii ni kawaida endapo mafuta ya transfomer yakiibiwa?

Nichukue hatua zipi? Au ukikosa umeme kwa muda wa siku tatu, utachukua hatua gani?

======

Umeme ulirudi muda mchache baada kuweka uzi huu.
 
Endelea kusubili mkuu, sanasana chukua glasi ya maji ya kisima unywe wakati ukisubiria!
 
Endelea kusubili mkuu, sanasana chukua glasi ya maji ya kisima unywe wakati ukisubiria!
Mkuu huwezi kuamini lakini umeme umerudi sasa hivi, sijui uzi wangu umefanya kazi au ilibidi niongeze subira kidogo.
 
Back
Top Bottom