Marufuku Kujadili Katiba Mtaani Huko Dodoma.

Marufuku Kujadili Katiba Mtaani Huko Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi amepiga marufuku mijadala yoyote inayohusu Katiba na rasimu yake katika maeneo na viunga vyote vya mji wa Dodoma.

Aidha amepiga marufuku mikutano ya hadhara au makongamano yoyote ya Katiba kwa maelezo kwamba vitendo hivyo vitawavuruga wabunge wa Bunge la Katiba linalotarajia kuanza kesho mkoani Dodoma.

Nimejiuliza sana kuhusu marufuku hii...hivi wabunge wetu kumbe hawana hoja na misimamo kiasi kwamba wanaweza kuvurugwa na mijadala ya nje ya bunge!

Inakuwaje dola kupitia kwa Mkuu wa Mkoa inawafunga midomo waTanzania kuongelea katiba,kisa makazi yao ni Dodoma?

Je kwa enzi na miongo hii,
marufuku hii ina impact anayotarajia Mkuu huyu wa Mkoa??
Chanzo: Taarifa ya Habari ITV usiku huu.

magamba wanahaha huku na huko baada ya mambo kuwaendea mrama. watahangaika sana safari hii.
 
Duh nimechemka kwa nguvu mpaka nikajishangaa. What!?
 
Kati ya wakuu wa mikoa wa ajabu kuwahi kuwasikia katika uso wa dunia hii, huyu ni mama moja. Si mara ya kwanza kusikia matamko yake ya kukataza mambo ambayo ni haki za msingi za wananchi. Sasa naelewa kwa vitendo kauli ya Prof Kabudi Jana kuhusu sifa za Wapumbavu.
La muhimu kwa huyu mama akumbuke ni nafasi na muda ndio vimempa hiyo nafasi aliyonayo.
 
Safi sana dodoma ni bunge tu ujinga mwingine marufuku.
Ona mtumwa wa fikra huyu naye! Mbona hamjiamini hivi? Pamoja na somo toka kwa Warioba na timu yake bado bongo zenu zimelala tuu?
Maneno ya Pro Kabudi yanajidhihirisha sasa.
 
haya ndio matatizo ya vyeo vya kipu.mbavu, vya kupeana, vya kulipana fadhila

Mzee apo umeongea. Huyo mama inawezekana anavunja sheria bila kujua ila tatizo watu wasiowa na profession yoyote hufanya lolote baada ya kupata kazi za kupewa kwasababu ujinga wowote haumuaribii kazi yake. Angekuwa mwanasheria, Accountant au daktari angekuwa na mipaka ya mambo yanayoweza kuaribu profession yake. Lakini vilaza kama hawa hawana chakupoteza.
 
Back
Top Bottom