Marufuku Kufukuza Wapangaji UK

Marufuku Kufukuza Wapangaji UK

Chibudee

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2016
Posts
1,775
Reaction score
2,408
Serikali ya Uingereza inatarajia kuwazuia wenye Nyumba kutowaondoa kwa miezi mitatu Wapangaji walioshindwa kulipa kodi ya pango kipindi hiki cha corona.
•
Serikali hiyo imesema kwamba inaelewa uchumi umeyumba kipindi hiki cha corona na kuna Watu hawafanyi kazi, wengine wamebaki nyumbani kulinda na kusaidia familia.
•
Kuhakikisha pia Wamiliki wa Nyumba hawakalii kuti kavu, wenye mikopo ya nyumba hawatoguswa kwa miezi hiyo mitatu.
FB_IMG_1584627557874.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku itakuwa ngumu sana kwa sababu bado watu wanakwenda kazini hivyo wanalipwa mishahara tofauti na huko ambako watu wanalipwa kwa saa ikimaanisha kuwa hujafanya kazi siku hiyo hakuna kulipwa.
Tunasubiri kwa hamu waziri mkuu wetu atoe tamko hili

God save us
 
Huku itakuwa ngumu sana kwa sababu bado watu wanakwenda kazini hivyo wanalipwa mishahara tofauti na huko ambako watu wanalipwa kwa saa ikimaanisha kuwa hujafanya kazi siku hiyo hakuna kulipwa.

God save us
Ikifika muda tukiambiwa hamna kutoka ndio tamko hilo tunalisubiri. Hata hapa tupo ambao tusipoenda kibaruani hatulipwi. Btw sio wote UK wanalipwa kwa saa, wapo wengi tu wanalipwa salary. Afanye masaa mawili au kumi mshahara wake ule ule.
 
Back
Top Bottom