Ibrahim K. Chiki
JF-Expert Member
- Apr 5, 2011
- 594
- 163
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), imepiga marufuku matumizi ya chupa za plastiki (vidumu) kuhifadhi au kubebea mafuta jamii ya petroli, kwa kuwa zina uwezo mkubwa wa kulipuka.
Pia imewataka wauzaji wa nishati hiyo katika vituo vyote vya mafuta nchini, kukataa kuhudumia wateja watakaohitaji petroli bila kuwa na magari yao vituoni kama njia ya kuwaelimisha juu ya athari za matumizi ya chupa au vidumu hivyo
Source: Habari leo
Maoni yangu
- Sisi tunaotumia magenereta kwenye biashara zetu na majumbani tufanye nini?
- Sheria hii inataka kutuaminisha kwamba mwenye gari akiishiwa mafuta ghafla basi ni mzembe. Tuchukulie mazingira kwamba umebakiwa na mafuta kidogo kwenye gari, lakini yanatosha kufika sheli iliyo umbali wa kama KM 25, then unafika na gari yako kwenye sheli hiyo, unakuta mafuta wameishiwa au hawa operate. The next sheli ni KM 25 zingine, uliskume gari mpaka huko?
Bila kuogopa naweza kusema kwamba waliotoa tamko ni wapumbavu na hawana uhalisia wa hali ya mtanzania wa kawaida.... itabidi sasa majenereta tuyabebe kwenye bajaji kuyapeleka petrol stations
hivi hawa watu wanafikiria kwa kutumia nini?
dira ya kigari chako cha mkopo haifanyi kazi, gari inakuzimikia kisa mafuta hakuna, unafungua buti, unatoa kidumu cha rita 5 haraka unaenda kituoni ili ununue mafuta safari iendelee, ghafla muuza mafuta anakwambia ni marukufu kuja na vidumu hapa, unamueleza hali ulitonayo kuwa gari imekuzimikia hivyo huna jinsi HATAKI KATUKATU. ghafla linakuja daldala limejaZa watu pomoni. anakuacha wewe pale unashangaa anakwenda kumuhudumia konda wa daladala. WANA JF nisaidieni hivi ile sheria ya kujaza mafuta huku gari likiwa na abiria imefutwa.....? NA HII YA KUTONUNUA MAFUTA KTK VIDUMU NDIO MBADALAAAAA..........?
huyu aliyetoa hilo wazo la kutokwenda na kigalon ni mpumbavu sana.......narudia......ni punguwani wa kutosha......mtu mzima huwezi fikiria upumbavu wa namna hiyo.......badala ya kutumia ubongo anatumia......nanihii (nimeihifadhi}.....$#^@@@*