Marufuku CD za Rogo, Uamsho na Ilunga

Marufuku CD za Rogo, Uamsho na Ilunga

Status
Not open for further replies.

Mzito Kabwela

Platinum Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,904
Reaction score
7,746
MARUFUKU CD ZA ROGO,UAMSHO NA ILUNGA.


Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar inayoongozwa na Dr Shein na Makamo wake Maalim Seif kupitia Jeshi la Polisi wamepiga marufuku rasmi cd zote za mawaidha ya Kiislam za UAMSHO,MUJAHID ABOUD ROGO na SHEIKH ILUNGA.

Hayo alisema ocd wazamani Murtad MKADAM ambae kwasasa yupo ofisi kuu ya polisi kitengo cha madawa ya kulevya Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif.

Alisema cd hizo za kiislam ni chanzo cha uvunifu wa amani hapa nchini na ndio zinazosababisha uchochezi baina ya dini ya ukiristo na uislam. Akifafanua alibainisha kuwa mpaka sasa washawakamata watu kadhaa wanaojihusisha kuuza cd hizo na kuwaonya wale wote ambao huweka kuzisikiliza watachukuliwa hatu kwani serikali ina mkono mrefu.

Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa kwamba waliowakamata hawawaoni kuwa wamewadhulumu kwa kufanya biashara halali ya uzaji cd. alijibu cd zile za mawaidha ni Haram wala sio rizki ya halali kwa upande wa serekali kwani zinapelekea uvunjifu wa Amani katika nchi.





Photo: SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA YA ZANZIBAR YAPIGA MARUFUKU CD ZA ROGO,UAMSHO NA ILUNGA.
 
Naona dola kule Zanzibar inaanza kuchukua hatua muafaka.
 
Umeambiwa CD ambazo zinachochea chuki ndio zimepigwa marufuku,sasa unaposema wadownload na kuweka kwenye simu unamaanisha kuwa unaunga mkno uchochezi na kusema kuwa Uislamu unakubali chuki na uchochezi?
 
Umeambiwa CD ambazo zinachochea chuki ndio zimepigwa marufuku,sasa unaposema wadownload na kuweka kwenye simu unamaanisha kuwa unaunga mkno uchochezi na kusema kuwa Uislamu unakubali chuki na uchochezi?

Sasa kama wanakataa kusikia tunafanyaje, tunawapa mbinu
 
Siku nikisikia masheikhe wengine pia wanapinga hizi cd ndipo nitakapo jua Uislam haufundishi kuua, hawa wanao pinga ni wanasiasa, sijasikia kiongozi yeyote wa dini/Mwislam kupinga hili, sijui na sina hakika, Mungu ameumba watu, halafu anawambia watu wengine wawaue ili wapate thawabu, inachanganya kweli kweli, sijui ni Mungu huyu huyu wa mbinguni au mwingine?
 
Jidanganye na akili yako mbovu,finyu,mbumbumbu,hakuna ki2 kibaya kama kumdharau m2 kwa imani yake,ucludie kumwita m2 kafiri,otherwise utafi...wa,kuwa makini unapo adrec wa2,popopopo.

"It is always more difficult to fight against faith than against knowledge" Adolf Hitler
 
Kiukweli namkubali sana dr shein,yaani ni mtu wa action...so objective... akitamka anamaanisha..
 
Hizi CD bado zipo na zinauzwa hadahrani kabisa, Hapa Arusha maeneo ya Cafe la Aziz kuna msikiti unaitwa "MASJID QUBA"
pale mlangoni kuna shelf limewekwa wanauza CD za uchochezi wa kidini muda wote. Jana nilipita hapo nikasikia kuna moja wameweka watu wanasikiliza, ilikuwa inazungumzia kuwa serikali imemtelekeza Aboud jumbe na kumficha huko mjimwema kigamboni kwa sababu ni muislamu.
 
Hizi CD bado zipo na zinauzwa hadahrani kabisa, Hapa Arusha maeneo ya Cafe la Aziz kuna msikiti unaitwa "MASJID QUBA"
pale mlangoni kuna shelf limewekwa wanauza CD za uchochezi wa kidini muda wote. Jana nilipita hapo nikasikia kuna moja wameweka watu wanasikiliza, ilikuwa inazungumzia kuwa serikali imemtelekeza Aboud jumbe na kumficha huko mjimwema kigamboni kwa sababu ni muislamu.

mi sometime huwa nabaki nacheka tu hizo mada zao mfu
 
Mi naona wasihangaike kuzipiga marufuku maana hayo mahubiri watu wenye akili timamu walishayapuuza, ni wajinga wahache sana wanaoweza kupotoshwa na hivyo vimahubiri, hata wakizipiga marufuku hawa wajinga wachache hayo mafundisho yameisha wakaa vichwani na nivigumu kuyafuta maana huo ndo uwezo wao na asiri yao, ndiyo haya matokeo tunayo yaona sasa, hapa Serikali ilishachelewa
 
Tusio waislamu tunaitwa kafiri.
LAKINI KUMBUKENI WOTE TUMETOKA KWA MUNGU.
Mnaweza kudhani nyinyi ni wamoja kumbe kuna SUNI NA SHIA.
JANA TU NIMEONA VIJANA WA KISLAMU WAKIJIANDIKISHA TUNISIA KWENDA KUPIGANA JIHADI SYRIA,lakini cha ajabu wote ni waislam na wanaenda kuwapiga wenzao waislamu kisa wao ni DHEHEBU TOFAUTI LA KIISLAM NA DHEHEBU LA RAISI ASAD.
madai yenu ya kuongoza nchi kwa sheria za kiislam tena kwa mabavu si jambo jema.
MIMI NAONA NI BORA MUENDESHE JUMUIYA ZENU ZOTE ZA KIISLAM KWA SHARIA LAKINI SIO NCHI.endesheni mambo yenu yote kwa sheria zenu lakini mambo ya wengine hayawahusu hata kidogo kama ambavyo sisi hayatuhusu mambo yenu.
NCHI HII HAINA HATI MILIKI YA KUENDESHWA KIKRISTO WALA KIISLAM.
wala hapakuwepo na hizi dini zinazotugombanisha.
KWANZA SEHEMU KUBWA YA WAUMINI WOTE WAMERITH DINI NA HAUKUWA UAMUZI WAO,mfano mimi leo ni mkristo kwa sababu nilizaliwa na wakristo,na ningekuwa muislamu kama ningezaliwa kwenye familia ya kiislamu.
HATA WEWE ULIYE MUISLAMU UNGEWEZA KUWA MKRISTO.
 
MARUFUKU CD ZA ROGO,UAMSHO NA ILUNGA.




Hii ndio hali tuliyofikiswa waislam na viongozi wanafiq ambao tuliwachagua eti tuliona uislam utakuja juu kumbe ndio wao wanaukandamiza bado waislam tumekuwa maiti hatutafakari ,hatuzinduki kuwabaini hawa wanasiasa niwanafiq.hawa wanailinda nidhamu yao sio uislam.

Tusipokuwa makini hata swala tutaambiwa tuswali majumbani kwani zinawakera makafiri.


Umesomeka mkuu, wengine tukisema CCM wameingia madarakani kupitia misikitini tunaambiwa waongo, wachochezi, tutoe ushahidi..... Aksante sana kwa kuwa muwazi. Kumbe mlichagua viongozi wa kisiasa ili waiweke dini yenu juu?
Salva Rweyemamu, bado dk Slaa ni Muongo?
Makinda bado unamtaka lema akuthibitishie ilihali hata nafsi yako inakusuta kuwa alichesema ni kweli?

 
Hizi CD bado zipo na zinauzwa hadahrani kabisa, Hapa Arusha maeneo ya Cafe la Aziz kuna msikiti unaitwa "MASJID QUBA"
pale mlangoni kuna shelf limewekwa wanauza CD za uchochezi wa kidini muda wote. Jana nilipita hapo nikasikia kuna moja wameweka watu wanasikiliza, ilikuwa inazungumzia kuwa serikali imemtelekeza Aboud jumbe na kumficha huko mjimwema kigamboni kwa sababu ni muislamu.
ukweli kwa upande wa kiislamu unaitwa uchochezi wa dini. ukweli kwa upande wa chadema unaitwa ugaidi.
 
ni wanafiki sana hao viongozi wa zenji, walikuwa wapi hadi wanakuja kuamuka leo kuzisimamisha wakati the whole msg has been delivered kwa wananchi? unafiki gani huo? kama wanaamini moyoni mwao kuwa ni kitu kibaya, kwanini siku ile ya kwanza tu walipoziona hawakuzisimamisha? si walizinunua wakaangalia na watoto wao, leo wanaona aibu kwasababu cd hizohizo ndizo zillizosababisha mapadri wawili zanzibar kupigwa risasi, mmoja akafa mwingine kabaki na ulemavu, na ndio hao hao waliosababisha bomb arusha....unafiki gani wa wazenji hawa, hivi wana faida gani kwa Tanzania?
 
Serikali kiziwi na kipofu!!!
Wanasubiri madhara yatokee ndipo wachukue hatua!!!!
 
Hizo cd ndo zilitumika kuhamasisha waumini wa dini yetu tukufu kumpigia kikwete kura na si kafiri! Nampongeza dr sheikhn kwa maamuzi yenye uzalendo kwa taifa letu!
 
Hamna lolote hapo walikua wapi,,,? Hizi cd zimetapakaa Congo,, south africa,,,zinauzwa ka babgum mpaka zimecross maborder mtawezaje kukzizuia nchini' ? Na mbaya mnazikamata kwa wamachinga badala ya kuzizuia kwa wazalishaji?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom