Martenity Leave | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Martenity Leave

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mercury, Jun 22, 2012.

 1. M

  Mercury Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wanaojua sheria naomba kujua maswala ya likizo za kinamama wanapojifungua. Mtu akijifungua huwa office ya serikali au binafsi zinampa likizo ya muda wa miezi mitatu. Na je hii likizo ikishaisha huwa kuna likizo ya nusu siku kwaajili ya kwenda kunyonyesha au la. Kwani watu wamekuwa wanaiongelea lakini aijulikani mtu anatakiwa apewe muda gani kwa wafanyakazi wa office binafsi na za serikali. Naomba nipewe ufananuzi na wataalamu wa haya mambo.
   
 2. B

  Bandio Senior Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sheria Ajira na Mahusiano Kazini, 2004 inatoa haki kwa mwanamke anapokuwa mjamzito kupata likizo ya uzazi yenye malipo (paid maternity leave) ya siku 84, au siku 100 kama utajifungua zaidi ya mtoto mmoja, ndani ya mzunguko mmoja wa likizo. Hata hivyo anaweza kupata siku nyingingine 84 ndani ya mzunguko mmoja endapo mtoto amekufa kabla ya kufikisha mwaka mmoja.

  Suala la mwanamke anayenyonyesha kupewa nusu siku sijawahi kulisikia, ila sheria ya kazi inamtaka mwajiri kumpa mwajiriwa anayenyonyesha muda usiozidi saa mbili kila siku ili aweze kumnyonyesha mtoto. Pia mwanamke anyenyonyesha hatakiwi kufanya kazi muda wa usiku kabla ya kutimia miezi miwili tangu alipojifungua.
   
 3. M

  Mercury Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Thank you
   
 4. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 3,058
  Trophy Points: 280
  Wanaruhusiwa pia kuwahi kuondoka..mfano hapa kwetu anaruhusiwa kuondoka saa 8 mchana..
   
 5. ram

  ram JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,224
  Likes Received: 918
  Trophy Points: 280
  Kuruhusiwa kuwahi kuondoka inategemea na makubaliano na muajiri, but kainachojulikana ni likizo ya uzazi siku 90 yenye malipo na masaa mawili ya kwenda kunyonyesha kwa muda wa miezi 6
   
 6. l

  lasix JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  ni kwa muda wa miezi 6 tangu kurudi kazini au hadi mtoto afikishe miezi 6?
   
Loading...