HUNIJUI SIKUJUI
JF-Expert Member
- Apr 4, 2015
- 1,335
- 1,639
nimesoma vitabu viwili vya ex- navy seals team six (DEVGRU) cha bwana Howard Wasdin na Mark Owen (alikua kwenye team iliyomuua osama bin laden infact yeye jamaa ndo alimuua na alikuepo kwenye mission ya kumuokoa captain philips pia)Hakuna Delta Force atakayetumwa kwenye mission inahusu undersea demolition wakamuacha Seal. Na pia kuna sehemu ambazo Delta wamebobea Seal hawaguswi
Mipaka ipo na ndio msingi mzima wa kuwa Spec Operator. Unabobea zaidi katika sehem zinazokuhusu, so inaundwa hivyo kwakua wanategemeana. Hakuna bora kuliko mwenzake ila wanakamilishana
Hata katika team moja kunakua na sniper mmoja,machine gunner mmoja,medic mmoja,k9 handler mmoja,radio guy na kiongozi kutaja kwa uchache. Na lengo ni kwamba ukifanye kitu hicho hicho mpaka unajua near perfect lakini sio kwamba wengine hawayawezi wanajua ila kuna specialization kubwa. Ndomaana ni gharama sana kutengeneza mmoja mpk kuwa tayari "kufanya majukumu" na akipungua pia kwa sababu yoyote ile no hasara sana kwakua inaharibu mizania.
Yes wanafanya mazoezi sana na marafiki zao. Mara ya mwisho niliwashuhudia kwenye mashindano yanaitwa SOFEX Qatar wakiwa na Jordans,SAS,Raiders Deltas nk
The most elite special forces kwa marekani ni delta na seal team six, Delta wao wako Army na Seals wako navy! Wote hao wako independent huwezi mkuta Navy seal kwenye mission za Delta au vice versa yaani wote hao wameiva kotekote, sio majini ardhini wala angani, hakuna mwenye weakness kokote yaani wote wapo sawa ,na kwenye mission hua wanagawana maeneo labda delta watakua wanaoparate kaskazini na seals kusini kamwe hawakutani, Kwanza navy seals na delta hawaivi pamoja kila mtu anajiona ni bora kuliko mwenzake
Wote ni makomando na wanajitosheleza ktk units zao, operator wa Delta yuko vizuri kokote ardhini,majini na angani, Navy seals nao ni hivyo hivo , sasa kwa hapa kwetu hakuna unit ambayo iko full???Maana uwanja wa vita hauchagua umespecialize wapi maana kama ni hivi maana yake makomandoo wetu wapo limited sana huyo wa majini ukimleta nchi kavu hana kitu, na huyu wa nchi kavu ukimpeleka majini hana kitu