Mark My Words: Serikali hii haina ujasiri wa kuhamisha machinga barabarani, inawaogopa sana

Tumemsikia Rais Samia akisema kwa lugha ya kujihami kuwa machinga wapangwe

Katumia lugha ya wapangwe badala ya waondolewe sababu anaogopa, anaogopa kuwa hawana mbadala wa sera ya kupunguza watu wasiwe machinga na pia aliyewaweka ni Magufuli ambaye naye alikuwa sehemu ya utawala wake ila akafeli kumshauri kuruhusu machinga ku operate freely

Pia Serikali inaogopa kwa kuwa haina sera za maana za kushawishi watu wala kujitetea kwa lolote kuhusu matatizo ya ajira na mengineyo na sana sana ipo madarakani kwa mabavu na ulaghai

So haitathubutu kwa kuwa itawapandisha hasira wananchi hawa, maana haina excuse yoyote ya kuwaambia na inahisi wataleta machafuko na kuwasogeza wananchi hao karibu na upinzani ambao inajaribu kila njia kuwazama

Tumesikia mbunge mmoja akithibitisha haya kwa kuishauri Serikali kuwa ikiwaondoa machinga watakuwa wanawaunga mkono upinzani na hivyo kuleta tishio kwa CCM

So CCM lazima iwaache machinga mtaani ili kuilinda, maana ikiwatoa haina cha kuwaeleza, itakuwa very unpopular

Mark my Thread..
Yes, I'll "mark your thread", because what you have expressed is the truth, the whole truth and nothing else!

Kiongozi mzima anaogopa kusema jambo bayana, anafumbafumba tu, "wapangeni"!

Watapangwa vipi bila ya kuendelea kuwa tatizo?
 
Tumemsikia Rais Samia akisema kwa lugha ya kujihami kuwa machinga wapangwe

Katumia lugha ya wapangwe badala ya waondolewe sababu anaogopa, anaogopa kuwa hawana mbadala wa sera ya kupunguza watu wasiwe machinga na pia aliyewaweka ni Magufuli ambaye naye alikuwa sehemu ya utawala wake ila akafeli kumshauri kuruhusu machinga ku operate freely

Pia Serikali inaogopa kwa kuwa haina sera za maana za kushawishi watu wala kujitetea kwa lolote kuhusu matatizo ya ajira na mengineyo na sana sana ipo madarakani kwa mabavu na ulaghai

So haitathubutu kwa kuwa itawapandisha hasira wananchi hawa, maana haina excuse yoyote ya kuwaambia na inahisi wataleta machafuko na kuwasogeza wananchi hao karibu na upinzani ambao inajaribu kila njia kuwazama

Tumesikia mbunge mmoja akithibitisha haya kwa kuishauri Serikali kuwa ikiwaondoa machinga watakuwa wanawaunga mkono upinzani na hivyo kuleta tishio kwa CCM

So CCM lazima iwaache machinga mtaani ili kuilinda, maana ikiwatoa haina cha kuwaeleza, itakuwa very unpopular

Mark my Thread..
Kwani Magu anasemaje!?!
 
Labda kitu ambacho hamjuwi CCM inaogopa tume huru ya uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama baasi na uhuru wa vyama vya upinzani.lakini wapiga kura nchi hii hawana maamuzi kwenye uchaguzi.
Pamoja na kukubaliana na wewe hapa....
Kwani CCM inategemea kura za wamachinga kushinda uchaguzi? Usijidanganye hao wachuuzi wanaweza kuhamishwa na CCM ikajitangaza kushinda kwa asilimia miamoja 100% na hakuna kima yeyote ataongea. Hii nchi bado tuna safari ndefu.
Sikubaliani nawe hapo juu!

Naona unajisahaulisha kitu wanachokiona cha hatari CCM, wewe unadhani wao hawana akili ya kujuwa hatari yao ipo wapi.

Machinga kwa umoja wao wakisema hakuna uchaguzi bila ya uwepo wa Tume Huru ya uchaguzi; uchaguzi hauwezi kufanyika popote nchi hii.
 
Hivi hata ukiwahamisha unawapeleka wapi?

Poor management and leadership ya CCM kwa miaka 60 ndio imepelekea yote haya.

Hawa machinga unawatoa mjini uwapeleke wapi, hakuna maeneo ya wazi, yote ccm iliuza na kujigawia, mji hauna open space. Hii yote ni uongozi na utawala wa hovyo wa ccm.

Kwa mfano, unawatoa kariakoo unawapeleka wapi hapa mjini?

Mimi ningeunga mkono waondolewe kama kungekua na maeneo maalum ya wazi yametengwa kwa ajili yao, hakuna, hakuna kabisa.

Kwa hiyo tuwaache wauze wanapotaka maana haya ccm imeyataka yenyewe.
And kwa nini yatengwe maeneo ya wazi kwa ajili yao? Wana uspecial gani? Kila kundi likitaka lifanyiwe vile wanataka wao then hamna sababu ya kuwa na serikali! Kuna masoko, waende huko, wakikosa nafasi watafute namna nyingine ya kujipatia kipato. Ila ni ukweli ulichoongea hapo mwanzo, upuuzi wa CCM ndiyo umezalisha hii kitu inaitwa machinga
 
🤣🤣🤣🤣🤣 unadhani kwanini hawataki Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi kama maccm yanapendwa na hivyo kushinda chaguzi kihalali?
Kila mtu anataka katiba mpya, ile ya kwanza kipindi cha JK ndiyo ilikuwa pa kuanzia, tatizo likaja wapinzani walitaka matakwa yao yote yatimizwe katika ile katiba, bila kucompromise kwenye baadhi ya vitu hatuwezi kufika popote
 
And kwa nini yatengwe maeneo ya wazi kwa ajili yao? Wana uspecial gani? Kila kundi likitaka lifanyiwe vile wanataka wao then hamna sababu ya kuwa na serikali! Kuna masoko, waende huko, wakikosa nafasi watafute namna nyingine ya kujipatia kipato. Ila ni ukweli ulichoongea hapo mwanzo, upuuzi wa CCM ndiyo umezalisha hii kitu inaitwa machinga
Wao kama wanachi wengine, wanahitaji maeneo ya kufanyia biashara. Wao ni wafanya biashara ila wenye mtaji mdogo hivyo wanahitaji maeneo ya kufanyia shughuli zao. Maeneo hayo ama mazingira hayo yanatengenezwa na serikali.

Kwa mfano kwa hapa Dar, naomba unisaidie kujua masoko ambayo machinga wanaweza kwenda kufanya shughuli zao bila shida ama wakapata nafasi za wazi na kuweka biashara zao, naomba unitajie.

Tatizo lako ni kuwaona machinga kama watu wasio na maana, sio sahihi. Hawa ni wananchi wafanyabishara wenye mitaji midogo na pia wana wateja wa bidhaa zao.

Kwa miji mikubwa wanalazimika kufanya biashara zao maeneo yasiyo rasmi kwa sababu hakuna maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili yao wakafanyie. shughuli zao huko.

Hawa watu wanafanya shughuli rasmi ila kwa mtaji mdogo, lazima wataftiwe maeneo maalumu ya kufanya shughuli zao. Hawa wote wakiwa hawana kazi wakaanza kupiga roba mtaani utapona wewe na kiduka chako??
 
Tangu lini Warioba amekuwa mpinzani? Unajua jinsi Kikwete alimvyodhalilisha Warioba na wajumbe wengine wa ile Tume ili tu kuonyesha rasimu ile haikubali?

Unadhani ni kwanini Butiku na Warioba wanataka mjadala wa Katiba mpya utumie rasimu ya Warioba ile ambayo HAIKUCHAKACHULIWA na maccm?
Kila mtu anataka katiba mpya, ile ya kwanza kipindi cha JK ndiyo ilikuwa pa kuanzia, tatizo likaja wapinzani walitaka matakwa yao yote yatimizwe katika ile katiba, bila kucompromise kwenye baadhi ya vitu hatuwezi kufika popote
 
Wao kama wanachi wengine, wanahitaji maeneo ya kufanyia biashara. Wao ni wafanya biashara ila wenye mtaji mdogo hivyo wanahitaji maeneo ya kufanyia shughuli zao. Maeneo hayo ama mazingira hayo yanatengenezwa na serikali.
Umeongea vizuri, ila definition ya machinga zamani ilikuwa ni watu wa kutembeza biashara ndogo ndogo barabarani, kwa sasa imebadilika! Machinga hawa wapya wengine wana mitaji hadi ya mil.100! Na wanavunja sheria za biashara, mipango miji waziwazi! Ila hili lawama zote ziende kwa CCM, wamelikoroga na walinywe sasa
 
Tangu lini Warioba amekuwa mpinzani? Unajua jinsi Kikwete alimvyodhalilisha Warioba na wajumbe wengine wa ile Tume ili tu kuonyesha rasimu ile haikubali?

Unadhani ni kwanini Butiku na Warioba wanataka mjadala wa Katiba mpya utumie rasimu ya Warioba ile ambayo HAIKUCHAKACHULIWA na maccm?
Hawakuichakachua yote Mkuu, Kikwete alikataa serikali 3 (Nadhani sababu ya hilo unajua) pamoja na kuweka ukomo kwa wabunge, mengine yote alikubaliana nayo ikiwemo kuwatoa wakuu wa mikoa na wilaya, tungeanza naye hapo
 
Back
Top Bottom