N-handsome
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,453
- 556
Sidhani kama kuna cha kubisha hapo.
Marine Hassan = CCM
TBC1 = CCM
Msajili wa vyama vya siasa = CCM
Mkuu wa Majeshi = CCM
Jaji Mkuu = CCM
IGP = CCM
Kamishna wa Magereza = CCM
Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi = CCM
........................... = CCM
Ukijumlisha vyote hapo utakuta JMK = CCM = Rais wa JMT 2010-2015.
Halafu eti mnataka nipoteze muda wangu kupiga kura? Siku hiyo nitashinda baa!
hayo ni mapenzi yako ndugu na wala kura yako moja haitamnyima Dr. (kwa maana ya dokta na si dokta wa kupewa) ushindi. ila nakushuari uende ukapige kura tu kama utakuwa na mudaHalafu eti mnataka nipoteze muda wangu kupiga kura? Siku hiyo nitashinda baa!
Katika hali kushangaza mtangazaji wa TBC1 Marine Hassan Marine wakati anamalizia kipindi chake cha jambo leo asubuhi ametangaza kuwa Kikwete ndio mshindi wa urais na Dr. Slaa na Prof. Lipumba watakuwa wanashindana nani apate kura nyingi. Hivi hii TBC inamwakilisha nani? ni ya taifa au ya CCM? kweli safari yetu ndefu na NEC watakaa kimya kwa hili pia
Lakini hebu tuwe realistic. Katika hao wapinzani wa Kikwete, nani anaweza kupata japo robo ya kura za Kikwete? Tusibweteke tukadhani kuna upinzani hapa Tz. Hamasa tuliyo nayo sisi huku mtandaoni ingefika kwa watu wa kawaida mitaani na vijijini ndipo tungeona upinzani kweli wa hoja/sera badala ya kupambanisha watu. Kwa hali iliyoko sasa, ni wazi kabisa kuwa atakayeshinda ni Kikwete, mazingira ya kisiasa yako upande wake kabisa. Sisemi kwa ushabiki wa kutaka iwe hivyo, ila ni kwa masikitiko makubwa kuwa hali hii haibadilishiki kwa wakati huu.
Ndiyo maana sijafurahishwa hata kidogo na uamuzi wa kumpeleka Dr Slaa kupoteza muda wake kugombea urais ambao hataupata na kuachia ubunge ambao angeupata. CHADEMA wamefanya kosa kubwa kujipunguzia wabunge bungeni.
Aspirin, mate wangu wa Arusha,
Unafanya makosa sana kusema hivyo. Ningelishauri au ukae kimya (siyo kwamba nakwambia shut-up ya Kihaya, USINIELEWE HIVYO TAFADHALI) au basi jiandikishe ukapige kura na umchague KIKWETE. Ndiyo makosa wengi huwa wanafanya. Kumbuka kuwa hata Mungu humsaidia mtu anayejisaidia.
Kuna siku naangalia formula 1. Jamaa wa RED BULLS walikuwa wakifukuzana na Hamilton akiwafuata bila wasiwasi. Hawa jamaa wakiwa wanagombea namba 1 na wakavaana na kutoka nje ya barabara. Hamilton aliishia kuwa namba 1. Kama angelikata tamaa na kujikalia pembeni, basi au mwingine angelishinda au jamaa wangelirudi na kushinda tena.
Kijana wangu, kama ungeliona Ubabe wa Wakoministi miaka hiyo, basi usingeliamini kuwa hawa jamaa wangeliweza kuangushwa. Ungeliona ubabe wa Hitler na askari wake wa SS, basi ungeliamini milele hawataweza kupigwa. Ungeliona........... iko mifano mingi na kwa Tanzania ni cha mtoto saaana. Ungelikuwa wa kukata tamaa, hata kwa Lugundi usingemaliza.
Acha hiyo kijana wangu. Wewe jiandikishe na ukampigie kura Slaa. Tukiwa na mtu Ikulu basi mambo mengi sana yatabadilika.
Kama Tido ana busara basi ni vyema kesho katika kipindi hicho hicho cha jambo leo huyu marine awaombe watanzania radhi kwa kujichukulia madaraka ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na kutangaza matokeo kabla ya uchaguzi! nakumbuka ule uchaguzi wa mwanzo kabisa wa vyama vingi kuna kituo kimoja cha televisheni kilitangaza matokeo ya uchaguzi Zanzibar na kusema Maalim seif alikuwa ameshinda, kilipata kasheshe hicho ni balaa! basi na iwe hivyo kwa huyu kibaraka wa CCM Marine Hassan Marine!
Lakini hebu tuwe realistic. Katika hao wapinzani wa Kikwete, nani anaweza kupata japo robo ya kura za Kikwete? Tusibweteke tukadhani kuna upinzani hapa Tz. Hamasa tuliyo nayo sisi huku mtandaoni ingefika kwa watu wa kawaida mitaani na vijijini ndipo tungeona upinzani kweli wa hoja/sera badala ya kupambanisha watu. Kwa hali iliyoko sasa, ni wazi kabisa kuwa atakayeshinda ni Kikwete, mazingira ya kisiasa yako upande wake kabisa. Sisemi kwa ushabiki wa kutaka iwe hivyo, ila ni kwa masikitiko makubwa kuwa hali hii haibadilishiki kwa wakati huu.
Ndiyo maana sijafurahishwa hata kidogo na uamuzi wa kumpeleka Dr Slaa kupoteza muda wake kugombea urais ambao hataupata na kuachia ubunge ambao angeupata. CHADEMA wamefanya kosa kubwa kujipunguzia wabunge bungeni.
Ndugu yangu inakatisha tamaa sana,
Kwa jinsi navyoona mwenendo wa chaguzi zetu upinzani kushinda kiti cha uraisi ni kama ndoto za alinacha. Kura zinavyoibiwa, mawakala wa vyama wanavyogeuka mamluki wa CCM na vitu kama hivi huwa inanikatisha tamaa sana. Unaweza kupiga kura kwa Slaa kumbe kura yako inahesabiwa kwa JK na kuzidi kumwongezea pasenti kwenye ushindi wake. Sasa skuli meti, si ni heri nisipige kura ili nipunguze pasenti ya ushindi wa JK?
Naungana na wengine, Slaa kugombea urais wapinzani wamepunguza sauti yao bungeni. Na hili ni kosa kubwa sana. Kwa gharama yoyote ile JK atashinda. Iwe kihalali au kilanguzi au hata kiubabe.
Mbona kuna majimbo WAPINZANI walishinda? Yaani CCM ni wezi kiasi hicho ila kuna sehemu wanaamua kuachia kidogo? Mie sidhani kama hali ni mbaya kiasi hicho. Kama watu wote tukisimama wima na kwenda kupiga kura kwa wingi na kusimamia kura wakati wa uchaguzi kuwa hakiibwi kitu, basi amini kwamba hawataiba. Na hata wakifanya hivyo basi si kwa asilimia kubwa sana.
CHDADEMA kama chama kinaweza kuweka karibu kila sehemu mtu mwenye computer na Internet LIVE wakati wanahesabu. Na wakimaliza, matokea yanatangazwa palepale. Hata kama si LIVE, watu wanaweza kuwa wanarekodi kwenye simu/Camera zao na kuwa na kumbukumbu.
Wakati wa UCHAGUZI nchi kama za Czech, Bulgaria, Rumunia, Hungury nk Wakoministi walikuwa wametawala kila sehemu na kuweka watu wao. Maadamu watu walikuwa wamechoka, WALIBANANA hadi kikaeleweka.
Inasikitika sisi kukata tamaa mapema namna hiyo.
Moto wenu VIJANA uwe "SLAA FOR PRESIDENT 2010"
Mengine haya wala MSITISHWE kihivyo. Mbona Slaa alishinda? Zitto, Wangwe, ....... na wengine wengi? CCM kweli iliruhusu? Kuiba kura imekuwa ni LUGHA inayotumika na UPINZANI mara wakishindwa kwa uzembe wao. Kama sasa hivi tukiwa NGANGARI na tulivalie njuga hili swala, TUTASHINDA.
JENDA KAJIANDIKISHE na siku ikifika, wewe, familia yako, Wapwa na Washikaji mnamchagua SLAA.
Ila kama kwako wewe, kuwepo kwa CCM unafaidi, basi hapo hakuna cha kujadili. Labda na mie ningelikuwa mtoto wa FISADI/Kigogo wa CCM au mtu wa karibu na Kikwete, basi ningelipinga Usiku na Mchana maana imesemwa "Aisifiaye Mvua........."