Maridhiano ya kweli kati ya vyama vya upinzani na chama tawala yanajumuisha nini?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Hivi karibuni, tume shuhudia viongozi mbali mbali wa vyama vya upinzani wakifanya mazungumzo na Rais Samia katika mchakato mzima utakao hakikisha kwamba kuna maridhiano kati ya chama tawala na vyama vya upinzani.

Je maridhiano ya kweli yakoje?. Kwanza kabisa ni vyama vya siasa kuhusishwa zaidi katika maamuzi yanayofanywa na serikali. Hii ina maanisha kwamba tofauti zote kati ya chama tawala na wapinzani ziwekwe pembeni na wote waweze kushiriki pamoja katika shughuli zote za kiserikali kwa manufaa ya wananchi.

Pili, tumejionea wenyewe jinsi ambavyo vyama vya upinzani vina chakarika kudai katiba mpya na tume huru. Picha tu hazitoshi katika kuhakikisha kwamba vyama vyote vinashiriki kikamilifu katika chaguzi zijazo. Nina amini kwamba maridhiano yanaenda sambamba na kuhakikisha kwamba madai hayo yanapatiwa suluhisho.
 
Nchi haina vyama vya upinzani, wote vibaraka na walamba asali wa Chama dola. Ukiwaona wanavyofoka na kutoa povu ujue hawajapata mgao wao ila wakishiba wanakuwa mazezeta yasiyojua mbele wala nyuma. Nonsense
 
Back
Top Bottom