Maria Sarungi: Mkopo wa WB wa elimu una masharti ya mtoto lazima arudi shule baada ya kujifungua, si Ombi ni lazima. Serikali kwanini inaficha ukweli?

Nitakuwa wa mwisho kukubaliana na hili..! Ukiniambia tuwekeze kuzuia mimba nitakuelewa si katika kurusu ujinga wa hawa watoto wabebe tu na watarudi shule.

Wanaharakati tukikosa kutumia hekima badala yake tukabeba mihemko ni ujinga, mnamfikiria mtoto mama vipi mtoto mjukuu, atalelewa na nani..??

Ukisha zaa wewe si mtoto ni mzazi tayari. Kwanini hamuoni pia mtoto kumlea mtoto ni ajira za utotoni tena zisizo na malipo ya moja kwa moja..?? Iweje mtetee mtoto anayeomba kufanya kazi za ndani ambazo kimsingi ni kama hizo za kulea mtoto afu huyu muone bora azae na akalee, binafsi sikubaliani kabisa, kikubwa tupambane kuzuia mimba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisingeweza formulate vizuri namna hiyo kama wewe ulivyo fanya. Respect! Wewe ni mhasibu nini mkuu? Safi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati huo mimi naandaa jina la taasisi mbili moja nitaiita ng'wakiliambiti na nyingine niite ng'washitolyo
 
Wewe

Wewe unajua mamaako alifanywa nini akiwa shule ya Msingi????
Mimi nadhani, kosa lilikuwa kutangaza kuwa WENYE MIMBA MARUFUKU. Maanatulikuwa na utaratibu wetu wa kimyakimya na ulitufaa.
Kwa bahati mbaya mama yangu hakuliona darasa
 
You are very wrong thinking that you know much about what happens out there
 
Muuu,sawa nadhani MAFARISAYO WANAFIKI wamekuelewa bila chenga,wapiga mimba wakubwa.
 
Samahani mkuu, unaweza Ku-highlight hiyo sheria kisha ukatuma humu na sisi tuweze kuona?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwongozo wa Wizara ya Elimu, hivi ndivyo unavyosema:-

KIFUNGU CHA 2.0 kinasema:-
Kumbe Mwongozo umetowa majukumu kwa washika dau wote, na hapa nataja wadau wakuu wawili:-

KIFUNGU CHA 2.3- Mwongozo kwa Wazazi/ Walazi


KIFUNGU CHA 2.6 ni Mwongozo kwa serikali:
-


Haya, weka hapa hiyo sheria unayosema "Sheria ya Elimu inatamka wazi kuwa binti kuwa na ujauzito ANAFUKUZWA shule."

Angalizo ni kwamba, huo mwongozo hapo juu ni wa April, 2009... kwahiyo tuwekee hapa sheria iliyokuja baada ya huo mwongozo!!
 
Wewe akili zako hazimo au hazikutoshi! Wazazi hawajazuiliwa kuendelea na shule baada ya kujifungua! Kilichozuiwa ni kutokana na Mira na desturi kama nchi! Nchi yoyote ina Mira na desturi yake ikiwa ni pamoja na wazazi kutochangamana na watoto katika shule za secondary! Wazazi kamwe hawawezi kuchanganywa na watoto wa secondary! Watasoma katika mfumo wa VETA na QT au vyuo vingine chini ya NECTA! Usipotoshe wazazi kamwe hawawezi kuchanganywa na watoto watiitu waliojitenga na ngono!
 
Mawazo yako ni mazuri isipokuwa msingi wa hoja tetezi wa Sarungi hujauelewa vizuri.
 
Unachotetea ni mufilisi na unachopinga ni mufilisi.
 

Kufikiri kwamba uliyemtaja angeweza kugombea uraisi, ni moja ya makosa makubwa uliyopata kufanya. Bila shaka umekwisha jisamehe.
 

Mataga mna shida nyie! Umesoma financing agreement yenyewe? Ni bora ukauliza ili uelimishwe kuliko kujifanya unajua operation za IDA. Hiyo sio loan ndugu, ni CREDIT. Hizo terms kwenye operations za World Bank zina maana na treatment tofauti mno.
Badala ya kumshambulia personally Maria ingependeza zaidi kuthibitisha uongo au uzushi wake kwa facts zilizopo kwenye financing agreement zikiwa na maana tofauti na hicho alichoandika Maria.

Kati ya vitu serikali hii ya jiwe inavyoviogopa ni UKWELI kuwekwa hadharani. Ni serikali inayodhani propaganda zinaweza kuficha ukweli. Hilo halitatokea aslani. Matusi yote hayo uliyomtukana Maria yanaashiria jambo moja tu:
Anaongea ukweli msiotaka ujulikane. Live with it dude, this is 21st century and it is the era whereby information is more freely available. Unamkumbuka alietamka hadharani kuwa anatamani "malaika ashuke na kuzima mitandao yote"?

Tell him that won't happen, even in his wildest dreams. Eti tunaelekea kwenye uchumi wa kati!
Uchumi wa kati my foot!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…