Maria Sarungi: Katika Siasa hakuna Malaika wala Shetani

Maria Sarungi: Katika Siasa hakuna Malaika wala Shetani

Status
Not open for further replies.
Naam... pengine kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tumempata mwanasiasa "malaika". Mwanasiasa huyu asiye na mawaa ni mwerevu kupita wanasiasa wote ndani ya chama chake na Taifa kwa ujumla wake. Mwanasiasa huyu ni kijana na mara zote amekuwa kwenye migogoro na wenzie chamani kutokana na kuonewa wivu.

Ndioo... anaonewa wivu kwakuwa ni mwerevu sana na kamwe hajawahi KUKOSEA. Huwezi mfananisha na yeyote aliyewahi kutangulia, hata yule tuliyemuita Baba wa Taifa si ashawahi kukiri kufanya makosa..? hata pamoja na jitihada zetu za kumpa "Utakatifu"..!? Malaika huyu niwa kipekee yeye amevuka hata Utakatifu wenyewe...!

Kwa mujibu wa walio karibu yake wanatueleza kuwa hii ndio nafasi yetu pekee ya ukombozi kupitia malaika huyu asiye na doa na bila yeye hakuna litakalofanikiwa Tanzania. Ni mara nyingi malaika huyu amejaribu kukamata usukani lakini wenye wivu wamekuwa wakimzuia.

Malaika huyu yawezekana kabisa akafanania na yule aliyetuahidi "maisha bora kwa kila mtanzania" kwenye nchi yenye neema tele ya asali na maziwa, ndiye yule tuliyeaminishwa ni "chaguo la Mungu" na wala hujakosea..!
cc:ZITTO ZUBERI KABWE
 
Huwezi fananisha mazingira ya siasa za TZ na USA! Kule hakuna kununuliwa kwa watu wala wagombea.Kama zipo taarifa tena zenye ushahidi wa Zitto kushawishi wagombea wa chama chake wakubali kununuliwa na kujitoa katika kugombea baada ya wapinzani wao kuongeza dau,Je mleta mada anadhani ni mwendawazimu gani anayeweza kumwanini Zitto na kumkabidhi chama? KUONGOZA CHAMA CHA UPINZANI KATIKA MAZINGIRA YA TZ SI LELEMAMA,MTU MWENYE TUHUMA ZA USALITI HAWEZI KUAMINIWA KAMWE NA KAMA YEYE NI MALAIKA SI AANZISHE CHAKE? HUKO USA ULISHAWAHI KUSIKIA VIONGOZI WAANDAMIZI WA SERIKALI WAKIAPA KUUA CHAMA CHA UPINZANI?
 
Ni matusi mazito kufananisha Mkakati wa David Plauffe na Mkakati wa MM,M1 &Co katika hili.Ni wapi uliona akina Plouffe wakiwatukana na kuwachafua viongozi wa juu au kusimika uongozi wao ambao ni parallel na kusababisha mgawanyiko ndani ya Democrats?
 
Anachokisema Maria Sarungi kwa mtazamo wangu ni kwamba yeye na wana CCM la kwao ni moja. Hiki anachokisema ndicho ambacho kimelifanya hili Taifa kuwa masikini na kuwa na kundi kubwa la WEZI wa mali za UMMA. kwamba ukiiba tukuvumilie, tukubebe kwa vile tunafahamiana. UIKIBAKA KWA VILE WEWE NI KIGOGO Usichukuliwe hatua.

Huu utaratibu wa watu wanafanya makosa halafu akina maria sarungi wanasema usichukuliwe hatua ndio unaopelekea kuwa na ORGANIZED CRIME hapa nchini na ndio maana unaona kuna wezi wengi sana ndani ya serikali na kila fedha inayopelekwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ZINALIWA NA WAJANJA kisha akina maria sarungi wanasema tusiwafukuze.

Akina maria sarungi wanasema hawa walio ua raia wasio na hatia kwenye operation tokomeza raia wasichukiliwe hatua eti kwa sababu wao ni wakubwa na serikali itatikisika

Ngoja nimpe mfano sarungi. ndani ya huu mwezi wa 12 Raisi wa korea ya kusini alisaini shemeji yake anyongwe kwa sababu ya kula rushwa na unyanyasaji wa kijinsia.

Maria sarungi wewe unamtetea zitto yawezekana wewe ni mmoja wa wafaidika na fedha za zitto. Kama zitto ni kiongozi ndani ya chama hafanyi lolote kukisaidia chama lakini akitoka nje anasema chama ni kibaya, akiwa ndani kwenye vikao anasema chama ni kizuri. MAMA yake zitto kupitia gazeti la mwananchi alisema Zitto ana watu wake wanaoweza kuzuia chadema iisifanye mikutano na kweli hawa watu wake wa CCm walifanikiwa kutekeleza maagizo ya mama yake zitto ya kuzuia mikutano ya chadema. Zitto akiwa kwenye mikutano hasema kwamba hana tatizo na viongozi wake lakini akiwa kwenye mitandao anasema mengine mengi

Ninaamini maria sarungi wewe ni msomi na kama msomi uliingia kwenye chama kumfuata mtu basi elimu yako haijakukomboa. THINK AGAIN
 
Ni matusi mazito kufananisha Mkakati wa David Plauffe na Mkakati wa MM,M1 &Co katika hili.Ni wapi uliona akina Plouffe wakiwatukana na kuwachafua viongozi wa juu au kusimika uongozi wao ambao ni parallel na kusababisha mgawanyiko ndani ya Democrats?

Kaka mimi nakuelewa kwa nini huwaelewi wenzako wa upande wa pili. Ukweli ni kwamba sio rahisi kuwaelewa unless you change your paradigm...the way you see things. in short kuna miwani umevaa.

Jamaa akina Kitila & Zitto wana uwezo wa kuona mbali unless na wewe uwe na huo uwezo huwezi ona hata kidogo.


So mimi nakubaliana na muono
wako!

Remember: Kitila ndio president wa DARUSO wa kwanza ambaye kipindi
chake ali-achieve a lot bila UDSM kufungwa. This tells uwezo wa ku-convince anao bila kupeleka watu
barabarani.
 
Sijaona hao wapinzani wa ndani wa democrats kama waliandaliwa mikutano na republic, nafikiri pamoja na kutaka uongozi hao wenzetu huwa vitu wanavyotaka kusimamia,
Na kwa hakika huwa hawana mpango wa kudhoofisha vyama vyao hii ndio tofauti ya upinzani wa ndani ya chadema na huo wa democrats
 
A kaleidoscopic Kubangos through a Kalahari of ideas, blooming bulbs by cacophonous coherence and overwrought obeisance to some almost ancient Uncle Sam antidotes.

I am not sure which is more disturbibg, the fact that such prominent members of society and supposed advocates for change would declare publicly that the sole purpose of political organization is winning or the contradiction of upholding transparency and hailing Zitto.
 
Mleta mada napata mashaka kuwa unajenga hoja c kwa lengo jema, bali kutimiza nia ovu ya kutuaminisha kuwa uasi ndani ya chama ni kitu chema. Kinachofanywa na Zitto hakitokubalika kamwe hata ungekuja na mfano gani hapa jamvini. Haiwezekani utuaminishe ati kuchukua fedha toka chama tawala kwa lengo la kuua chama chako uite ni jambo la kawaida, eti ni ushindani. Kukwepa kuhudhuria vikao vya chama eti ni ushindani. Kuenda tofauti na maagizo ya chama na kupinga wazi wazi kauli za viongozi wa chama chako eti ni ushindani. Kuwanunua wagombea na madiwani wa chama chako ili kukidhoofisha chama ni ushindani? Huu ni usaliti. Hakuna lugha nyingine mbadala, ni usaliti. Chama ni kikundi chenye malengo sawa, kama unadhani malengo yako hayatimii ndani ya cdm c uhame ama kuanzisha chama chako? Usiwapotoshe wanajamvi kwa kutoa mifano ya USA ambayo wala haiendani na kilichofanywa na Zitto. Acha siasa nyepesi kwa masuala mazito kama ya Zitto. Usilinganishe mazingira ya demokrasia ya USA na TZ, wenzetu wako hatua ya juu ya maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Hivyo mitazamo imehama kutoka kujiangalia wao binafsi na kuitazama jamii iliyowapa uongozi.
Usimlaumu Nyerere, alilazimika kubinya wigo wa mawazo mbadala kutokana na uchanga wa Taifa letu. Angeruhusu hicho unachoita demokrasia wengine wangenunuliwa kama Zitto na kuja na mawazo ya kubomoa taifa. Halafu nani kakwambia hiyo demokrasia ni universal? Usitupotoshe, Kitila na Zitto ni wasaliti, wangekuwa na nia njema wangefuata taratibu na miongozo ya chama.
 
there is no permanent enemy or friend in politics
 
Nimejaribu kupitia uzi wa maria sarungi,kwangu mimi naona kuna mahala kachanganya mambo mawili yasiyoendana kama ifuatavyo,
1.moja amejaribu kueleza umuhimu wa mtandao kwenye uchaguzi ikiwa ni pamoja nakutumia mbinu za uzushi na ujasusi ikibidi.katika hali ya kawaida uchaguzi wa ndani ya chama nitofauti kabisa na uchaguzi wa kushindanisha vyama vyenye sera na misimamo tofauti.maana kuna vyama katika chaguzi kuna vyama vingine utegemea sana ushawishi wa fedha badala ya sera vingine hutegemea sana ushawishi wa sera,vingine utegemea mgongo wa dini nk.
2.upande wa pili kuna uchaguzi wa ndani ya chama chenyewe kupata mtu wakukiongoza au kukiwakilisha katika chaguzi mbalimbali kama vile,urais,ubunge,udiwani na uwenyekiti wa mtaa.katika nafasi nilizotaja kila chama kinavigezo vyake vinavyotumika kumpata mtu anaefaa kwenye nafasi husika kwamfano,
MWENYEKITI.katika vyama safi kabisa kigezo cha kwanza ni uadilifu na sio elimu,kwa sababu mtu mwadilifu anashaurika,ni mwaminifu,nimpenda watu nk.na katika kampeni ya uchaguzi wa ndani ukitumia ujasusi au uzushi ni dhambi,kwa sababu ndani ya chama nyie ni wa moja unapotumia ujasusi na uzushi unafaidika wewe uku chama kikibomoka kwa hiyo kwa faida ya chama tunafanya kampeni za wazi zenye maono chanya ju ya mustakabali wa chama na sio mgombea maana mgombea anaweza kuhama lakini chama kina baki.mwisho ju ya suala la chadema kweli chadema ndio chama kina cho wapa matumaini wa tanzania yakuwa chama mbadala ya ccm kwenye kushika dola.na kama hivyo ndivyoilivyo chadema haitakiwi kiwe na makundi kama ilivyo kwa ccm ambayo wana ccm wenyewe wamekiri hadharani.pia kuwa mwenyekiti au mgombea wa chadema ni lazima mtu uwe msafi kwa maana ya kuwa muadilifu usiye na chembe ya uzushi, majivuno,muongo,mbinafsi au mwenye tamaa.hapo ndipo tatizo lakina zitto lilipo anzia zitto yy binafsi amekuwa akituhumiwa kuwa anatumika na ccm kutaka kusambaratisha cdm.
 
Kaka mimi nakuelewa kwa nini huwaelewi wenzako wa upande wa pili. Ukweli ni kwamba sio rahisi kuwaelewa unless you change your paradigm...the way you see things. in short kuna miwani umevaa.

Jamaa akina Kitila & Zitto wana uwezo wa kuona mbali unless na wewe uwe na huo uwezo huwezi ona hata kidogo.


So mimi nakubaliana na muono
wako!

Remember: Kitila ndio president wa DARUSO wa kwanza ambaye kipindi
chake ali-achieve a lot bila UDSM kufungwa. This tells uwezo wa ku-convince anao bila kupeleka watu
barabarani.

Mkuu na wewe pia yawezekana umevaa miwani. Unapofanya mikakati ya ushindi bila kuharibu chama usitukane viongozi waliokutangulia ili wewe uonekane msafi! Acha natural process ichukue nafasi yake. Kwa nini utukane viongozi wenzako kwa kujificha? Ni upumbavu na tamaa ya madaraka ndo inayosababisha watu wafanye haya. Umesingiziwa sawa, kwa nini usifuate taratibu kutafuta justice? Anachofanya zito sasa hivi kina utofauti gani na hao unaowaita viongozi wa DARUSO waliogoma
 
Kusingekuwa na haja ya kuwa na vyama kama mawazo ya Maria yangekuwa valid. Maana ya vyama ni kwamba watu wa chama fulani wanakuwa na common goals na hata kama wanakuwa na tofauti bado ni ndogo sana.

Na hapa ukisoma vyema uzi wa Maria unagundua kabisa yuko in favor kwa upande anaotuhumuwa kuusaidia kufanya maasi. Watanzania wanajua mambo siku hizi Dada yangu na sio rahisi kuwadanganya.

Mifano uliyotoa pale juu ni tofauti sana na kinachoendelea hapa kwetu. Mtu anasaidia chama kingine wazi wazi ili hali wenzie wanahangaika usiku na mchana na wengine wanawekwa hata kolokoloni katika kupromote chama chao kisha uje uclaim uongozi wa juu from no where kweli inawezekana? Kwa hapa nitabaki kuwa tofauti na mawazo ya Dada yangu Maria tuliekulia pale Ghana Mwanza wote. We ni mjanja usikubali kutumiwa Sister.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kuna wakati huwa najidharau kuwa mtu mweusi! 7bu tunaongea nakufanya mambo yakijinga sana! Ktk mambo wanayofanya wazungu tumeona hilo2 lakutofukuzana! Mbona hatuigi na mengine ili tuwe km wao!
 
Naomba nisimame upande wa Mzee Mwanakijiji kuwa Nidhamu ni Msingi mkuu wa mafanikio... Mkakati wowote ambao huonndoa nidhamu huleta madhara... Ukosefu wa Nidhamu hupelekea Usaliti kama ambavyo Zitto alivyoamua kukisaliti CDM kwa tama ya madaraka na mali...Aliona ni bora atafute usaidizi nje ya CHAMA, hata kama wasaidizi ni mahasimu wa CDM... Je, Ukosefu huu wa Nidhamu kwa Zitto et al umekijenga chama ama unakidhoofisha? kushirikiana na akina Zoka, Nchimbi, Nchemba ilikuwa bahati mbaya ama ni urafiki wa kawaida tu?...Mavi hayapuliziwi manukato! Bado yataendelea kuwa mavi tu!!!!
 
Maria umeandika makala nzuri sana na mie nakubaliana na wewe kuwa hivyo ndivyo inatakiwa kuwa.

Ila ukweli ni kwamba kwa wenzetu kama USA au UK, Vyombo vya usalama huwa vinafuatilia vyanzo vya mapato vya hawa Wagombea ili isije ikatokea kanunuliwa na Matajiri wa nje. Tuliona UK wakila sahani moja na PM Tony Blair kuwa alipokea laki kadhaa kutoka kwa wale Wahindi Ndugu (Mittal Brothers), matajiri wakubwa duniani. Tuliona German, Chancellor Helmet Kohl akiondolewa madarakani kwa kosa la kupokea fedha kutoka kampuni la mafuta la Wafaransa ELF kwa aiili ya chama chake.

Tatizo kubwa lililopo kwetu Tanzania ni kuwa unakuta kiongozi wa upinzani anafedha chafu na hakuna anayeuliza kazitoa wapi huku kipato chake kikiwa duni sana. Hawa watu huwa wanarubiniwa na kuanza kusaka madaraka kwa nguvu kwenye chama. Na kwa sababu Waafrica tuna tamaa sana ya hela (ona Kenya walivyonunuliwa kwa urahisi na El-Shabaab) basi huwa tupo tayari kumkaribisha nyoka kwenye nyumba.

Tuseme leo hii Zitto Kabwe na kitila Mkumbo waingie na kuwa Mwenyekiti na Katibu wake na huku Mwigamba akiwa sijui mtu wa habari. Umoja wa vijana wa Chadema warudishwe Juliana Shonza na Mwipamba na Davidi Kafulila arudi na kuchukua sijui nafasi ya Mnyika (ninaamni wataweka watu wao), je Chadema atabaki nani? Si kitakuwa kama CUF au NCCR kwa kuitwa Mke mdogo wa CCM? Je Zitto kama Mwenyekiti wa upinzani, ataendelea kuwa na uhusiano mzuri na chama tawala? Huo utakuwa upinzani kweli au mtu na shoga yake?

Kwa hali ilivyo sasa, kitendo cha Zitto kuwa Mwenyekiti, ndiyo utakuwa mwisho wa Chadema. Labda siku CCM ikija kuwa chama cha upinzani, Zitto anaweza kuchukua hicho cheo na kuwa kiongozi mzuri, labda waje sasa Wachina wamnunue.

Umeandika with very very low mind, yaani kwa akili zako haukutakiwa hata kidogo kujibu hoja za maria, amekuacha mbali sana

yaani kwa akili zako, huwezi ukawa rafiki na CCM, upinzani ni uadui

nilifikiri nyie mliojiunga siku nyingi JF mna weza kufikiri, kwa bandiko lako hilo umenifanya niwe cautiously

uliachoandika ni mwendelezo wa siasa chafu kabisa
 
Hivi siku kina ZZK na Kitila wakiingia madarakani watakuwa tayari kufanyiwa hichi kitu wanachofanya wao kwa viongozi wao ?

ZZK akumbuke 2010 alikuwa anampigia kampeni Kafulila badala ya mgombea wa CDM, kama huu si usaliti ni nini ?

Dada umeandika maandishi mengi sana lakini maudhui yake ni hali ya chini. Mawazo yako yangefaa kwa CCM zaidi kuliko kwa vyama vilngine. Kwa CCM ni kawaida kuwa na makundi ya kimmaslahi.
 
Maria na washauri wote wa zzk,mnafananisha USA na TZ.sawa

kwa vyombo vya usalama vya America,milele Zitto asingekuwa Rais wa nchi
Acha Urais huko ni mbali bali nafasi yeyote ya maamuzi isingewezekana. Only in Tanzania ndio mtu anaweza kugundulika ghiliba zake na bado akafikiriwa kupewa uongozi.
Mie nasema hata ile nafasi ya naibu katibu mkuu haikuwa stahili yake hata kama hangefanya makosa aloyofanya. Jamaa sifa za uongozi ( wa ukweli) hana kwa maana ya kiongozi makini. Uongozi ni wa kuunganisha watu sio kutafuta sifa binafsi.
 
Umeandika with very very low mind, yaani kwa akili zako haukutakiwa hata kidogo kujibu hoja za maria, amekuacha mbali sana

yaani kwa akili zako, huwezi ukawa rafiki na CCM, upinzani ni uadui

nilifikiri nyie mliojiunga siku nyingi JF mna weza kufikiri, kwa bandiko lako hilo umenifanya niwe cautiously

uliachoandika ni mwendelezo wa siasa chafu kabisa

Wewe ndio una akili ndogo kuliko mwenzako.

Kuwa na urafiki na CCM ni sawa na urafiki kati ya Simba na swala.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom