Maria Sarungi: Independent Candidate?

Ni raia wa TZ au Ethiopia maana hatuna uraia wa nchi mbili mleta mada utakuwa wala hujui.Nikikuuliza ndoa ilikuwa lini na wapi utakuwa hujui unachojua anafaa uraisi.Urais sio picha za kubandika ofisini
 
she is a big thinker na anauwezo wa kutetea point.Aende Rorya akarudishe jimbo la mzee wake.
 

..duh!!

..by the time nimegundua kuwa mtoa mada anataka huyu dada awe Raisi it was too late to change my post.

..lakini kwa kifupi ni kwamba demokrasia ya Tanzania bado ni changa mno kuweza kuwa na independent candidates hata ktk nafasi za ubunge, achilia mbali uraisi.

..mimi kwa kiasi fulani napenda siasa za Kenya ambapo haraka haraka wanaweza kuunda coalition za ushindi. nadhani kwa mfumo huo kuweza kufanya kazi hapa Tanzania itabidi kwanza CCM ivunjike au idhoofike kwa kiasi kikubwa.

..mimi ndoto yangu ktk siasa za Tanzania ni MUNGU atujaalie tupate BUNGE ambalo hakuna chama chenye CLEAR MAJORITY.
 
Mzalendo gani ameolewa na mkimbizi hana lolote sarungi amepata hasara ya mtoto
 
Wabongo kwa kushadadia,sasa ukichwa wake upo wapi mbona hata hatumsikii,naona anashinda fb tu na Zito wake,fb yake inatuhamasisha vp sisi huku Iramba ndani ndani,watu kama Halima Mdee,Bulaya ndo madem wa kuwapa vichwa
 

Mwalimu nimeisoma Post yako na majibu mengi ya hii Post.Ni kweli Maria amejitokeza kuwa Mtanzania anayetetea maslahi ya wengi bila Uoga wala kuegemea upande mmoja (Itikadi za vyama).Maria ni Mwanaharakati wa kutetea haki sawa kwa wote.Mimi binafsi nina Imani kubwa na huyu Dada kama ataingia kwenye ulingo wa Siasa.Uwana harakati wake haumzuii kuingia kwenye Siasa.Ana upeo mkubwa wa uelewa wa mambo na ni rahisi kutolea maelezo wakati wowote.Maria hana Chama cha Siasa, na wala hatetei Status Qou,anaamini katika Utanzania na si Itikadi za vyama.Wapo hapa wanaomuhusisha siasa zake na Urafiki na Mh.Kabwe.Maria ni Mtu huru,huwezi kumchagulia rafiki eti kwa sababu tu rafiki huyo yupo upande wa pili wa Itikadi yako? Mbona hamuujadili Urafiki wa Maria na Dr.Kingwangwalla, Januari Makamba,John Mnyika, Halima Mdee au Ismail Jusa? Imekuwa Zito Kabwe tu? Kabwe kama Maria ni Watanzania zaidi kuliko Itikadi za Vyama,Urafiki wao unaweza kuwa umejikita kwenye hilo zaidi.

Kwa Mtazamo wangu Sikubaliani nawe Maria kuwania nafasi ya Urais,Nafasi hiyo ni kubwa sana kwake.Itakuwa vyema Maria aanzie (aingie) kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge kwanza.Ana nafasi nzuri kama atakwenda kwenye Ubunge katika Jimbo analotoka Baba yake au Majimbo yanayozunguka DAR kwa sababu tu ni sehemu anayoishi,na aliyokulia ana ufahamu zaidi na eneo hilo.Nawashangaa sana wanao-question uwezo wa Maria.Watu hawa watakuwa hawamfahamu huyu Dada au wanaleta ubishi kwa sababu zao binafsi.Maria toka Utoto wake ni mtu mpenda Nchi na mwenye Juhudi kwenye masuala ya Akademia (shule).Kwa maelezo yake mwenyewe "Anakinzana na Baba yake Dr.Sarungi kwa masuala mengi yanayohusu Utumishi wa Umma." Ni mtu mwenye mawazo huru na anayesimamia maamuzi yake!

Ni Mtanzania mwenzetu,Ametoka kwenye familia yenye uzoefu na public service,Tumpe ushirikiano atafute Jimbo ili awatumikie Watanzania wenzake.Siasa haina mwenyewe,huko Bungeni wapo wanasheria,walimu,wapiga disco,wanafunzi,wanaharakati,mabongoflava mpaka waganga wa kienyezi,wanaweza kuwawakilisha watu wao vizuri,Itakuja kuwa Maria ambaye kipindi kifupi cha Bunge la Katiba ameonyesha Umahiri na Ukomavu wake kisiasa? Tusimwage matusi na kujadili maisha yake Binafsi,Tumjadili Maria kutokana na mawazo yake kisiasa ktk Bunge la Katiba,Makongamano,Tweets,Instagram au Facebook.Tusijenge Hulka ya kuwakatisha Tamaa wenzetu ambao wameonyesha utashi wa kutaka kuwatumikia Watanzania wenzao..
 
Mtaanza nyie bootlickers, empty headed!!!
Watu msio na dira wala upeo!!!

Hao wanaowatuma wakisoma hapa wanajua na ujumbe wanaupata!!!
mbona povu limekutoka kama unataka kufa kweli
 
Mzalendo gani ameolewa na mkimbizi hana lolote sarungi amepata hasara ya mtoto
jambo usilolijua ni kama usiku wa giza maria sarungi elimu aliyokuwa nayo kwenye ukoo wenu hakuna mwenye hiyo elimu ndo la kwanza hilo.
 
Na ni mhudhuriaji mzuri wa masomo ya Jaji Warioba.
Ni jembe sn,alikataa kurudi bungeni kwenye upuuzi wa Sitta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…