Marekebisho JF

Marekebisho JF

GY

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
1,279
Reaction score
126
Tumeona namna JF ilivyoboreshwa na kuwa na mambo mengi zaidi. Lakini mimi kuna kitu huwa bado naona kama kinapunguza sana ladha ya JF

Mosi: Mtu anaruhusiwa kupost thread nyingi atakavyo na wakati mwingine unakuta zote zinazungumzia kitu kimoja...INACHOSHA

Pili: Kuna mijadala ambayo huwa ni mizuri sana ila huwa inaharibiwa na watu hasa pale wanapoanza kuichukulia ni personal badala ya kuiendeleza kama ambavyo muanzishaji alivyolenga: INAKATISHA TAMAA

Tatu: Ingawa ndio kwenye msafara wa mamba hata kenge wamo, ila kenge wakizidi inakuwa ni msafara wa kenge wenye mamba....pumba zimekuwa nyingi kuliko mchele sa sijui hiki ni chakula cha kuku ama binadamu: INAUDHI

Nne: Bado upo ubaguzi sana kwenye nani anaruhusiwa kupost thread yake wapi...mfano jukwaa kuu ambalo ni jukwaa la siasa (uone namna watanzania wanavyopenda blaablaa) huwa linatumiwa zaidi na watu fulani hata kama walichokipost hakihusiani na siasa: HAIHUU

Tano: Ingawa slogan ya JF ni "where we dare to talk openly", ukitazama kwa makini utaona kuwa slogan hii ingepaswa kuwa (kama nilivyopata kusema huko nyuma) "where we dare to talk crazily": INATIA AIBU

Sita: .............ongezea na wewe uliyoyaona

All in all, moderators mnajitahidi sana, hasa kwenye ku-ban watu sikuizi.....na huenda kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi, mtani-ban na mimi kwa niliyoyasema

I am responsible for that!
 
Mimi nilidhani unazungumzia marekebisho ya system, kumbe unazungumzia mabandiko?! Weka heading vizuri.
 
As far as you understand what I mean, its enough
 
Mkuu unataka tuendeleze vipi wakati hayo ni mawazo na utafiti wako ulioufanya! Labda ungetoa pia mawazo mbadala kwenye moja ya thread zako jinsi ambavyo wewe umekuwa muadilifu kwa hili.
 
Mkuu unataka tuendeleze vipi wakati hayo ni mawazo na utafiti wako ulioufanya! Labda ungetoa pia mawazo mbadala kwenye moja ya thread zako jinsi ambavyo wewe umekuwa muadilifu kwa hili.

Tayari yaleyale ya kuchukulia vitu personal..soma namba mbili hapo juu
 
mimi naona acha mambo yaendelee kama yalivyo,tuko wengi sana hapa JF kila mtu na akili zake.Pale unapokuta PUMBA,vumilia...chapchap tafuta ulipomchele ufaidi.Mods wanajitahidi sana sana na siku zote nashangaa wazimuduje kazi zote hizi mathread kibaoooo kila siku.
 
Nakubaliana na wewe to some extent!...Japokuwa unaposema pumba zimekuwa nyingi sielewi its from what point of view!, maana wewe unazoona ni pumba wenzio ndo wanaona ishu, na ishu zako watu wengine wanaweza kuona PUMBA, labda unge'cite live examples za hizo pumba ili tuzichambue kwa pamoja na tuone zinaangukia zaidi wapi!....

Na je unaposema JUKWAA KUU ni lile la SIASA, Hii imetangazwa lini, au mimi niko nyuma ya wakati?...Hivi kuna majukwaa madogo hapa, au yapo yanayokosa wachangiaji, ndo ukayaita madogo!..Anyway, u r entitled to all what you said, na sioni kwanini unahofia MODS kukukamata mapembe, hujamtukana mtu mkuu!
 
Naweza kuanza ku-justfy baadhi ya niliyoyasema...mfano wa hoja namba nne hapo juu ni kama ifuatavyo: ukienda kwenye jukwaa la siasa hivi sasa utakuta thread iliyowekwa jana na somebody TRACE yenye kichwa cha habari: "Startrimes ipo nyuma ya nani?".....sasa hili linahusiana vipi na siasa..hata nilipoisoma haikuwa na uhusiano wowote na masuala ya siasa
 
Kwanza ni sahihi kabisa uliyosema kuhusu jukwaa kuu,,,kunradhi kwa kutosema hapo awali kuwa hiyo ni kwa mtazamo wangu hasa baada ya kulifuatilia kwa muda sasa na kwa kutazama vigezo fulani kama idadi ya viewers, threads na posts,,,,pia namna ambavyo limekuwa likitumiwa na mods toka huko nyuma kwa matangazo mbalimbali...but well linaweza kuwa lisiwe hivyo kwa wengine

Hilo la pumba aaa sidhani kama linahitaji sana justfication....unaweza kupitia threads mbalimbali ukajionea mwenyewe...na hata kwenye hii niliyoianzisha utaona sasaivi pumba zitaanza kuja,,,and as u said huenda hata haya yangu ni pumba tu,,,so pumba kwa pumba unapata nini sijui
 
mimi naona acha mambo yaendelee kama yalivyo,tuko wengi sana hapa JF kila mtu na akili zake.Pale unapokuta PUMBA,vumilia...chapchap tafuta ulipomchele ufaidi.Mods wanajitahidi sana sana na siku zote nashangaa wazimuduje kazi zote hizi mathread kibaoooo kila siku.
Huyu bwana anataka kulazimisha akili zake tuzichanganye na za kwetu!!
 
Naweza kuanza ku-justfy baadhi ya niliyoyasema...mfano wa hoja namba nne hapo juu ni kama ifuatavyo: ukienda kwenye jukwaa la siasa hivi sasa utakuta thread iliyowekwa jana na somebody TRACE yenye kichwa cha habari: "Startrimes ipo nyuma ya nani?".....sasa hili linahusiana vipi na siasa..hata nilipoisoma haikuwa na uhusiano wowote na masuala ya siasa
Nafikiri hii siyo ishu wakati mwingine mtu hupost topic kwenye jukwaa lisilohusika lakini baada ya Muda MODs huipeleka kwenye jukwaa husika maana siyo ishu ya kusema uifungulie topic na siyo kosa mtu kupost topic kwenye Jukwaa lisilohusika wengine bado wachanga wa ving'amuzi.

Hata ya kwako kutokana na uliyoandika ungeipeleka kwenye Jukwaa la complain na siyo kwenye Hoja Mchanganyiko kama kweli uko 'smart':dance: ila pengine na wewe ni mmojawapo uliyeshindwa kujua hii post yako inafaa Jukwaa gani.
 
We need an orientation for that....kwangu mimi hii sio complain..ni hoja tu

Na ndo ninayoyasema hayo, badala utazame kilichoandikwa, unakimbilia kumu-attack mtu personally

Na yoooote niliyoandika hapo juu nimesema yanapunguza ladha tu ya JF sikwamba yanaondoa maana na kazi nzuri inayofanywa na MODs na wachangiaji...ebu soma tena iyo thread yangu, na kwakuwa unaonekana mkongwe utaelewa yapo yenye maana yakufanyiwa kazi
 
Back
Top Bottom