Vikwazo vipya dhidi ya Iran? Baada ya vita kali? Hiyo nchi imepigwa vikwazo vikali na Marekani, EU na marafiki zao tangu 1979 lakini haipigiki. Haisalimu amri.
Marekani waliifadhili Iraq chini ya Saddam Hussein kushambulia Iran kwa vita iliyochukua miaka 8 tangu 1980 hadi 1988 na kuua wapiganaji na raia wa Iran karibia 1m wengine kwa mabomu ya sumu Marekani na Israel wakihusika.
Marekani na Israel wameua viongozi wa kidini na kijeshi wa Iran na kuangamiza jeshi lake la maji, anga na vituo vya kurushia makombora kwa kuvizia katikati ya mazungumzo ya awali ya amani ya mwanzo kabisa katika hii vita ya sasa. Lakini Iran imegoma kujisalimisha. Na sasa vikwazo vipya! Sijui kama vitasaidia kitu.
Iran imechakazwa sana na mabomu ya Marekani na Israel. Uchumi wake umepigika kweli kweli kwa miaka 40. Lakini ni no surrender tena sasa wanaendelea kumfanyia dhihaka Donald Trump wakitumia AI.
Marekani ina majeshi yenye silaha nzito na teknolojia kubwa. Ina pesa kubwa na uchumi mkubwa. Inadhibiti sehemu kubwa ya uchumi wa dunia. Lakini wameshindwa kuisalimisha Iran. You know why? jeshi lake halina SPIRIT (nafsi) ya mapigano. Kupigania pesa na mabilionea ni tofauti na kupigania uhai wa nchi yako.
Uongozi wa Marekani hasa wa sasa hautumii akili, una kiburi kingi, jeuri nyingi wala hauna mikakati ya maana katika hizi vita zake za uvamizi wa nchi "nyonge". Inachukulia nchi zote zina viongozi duni kama Venezuela. Kwenye list bado wana Cuba, Greenland, Amerika ya Kusini yote, n.k. Sasa wanataka kutawala dunia wakishirikiana na Urusi, China na Israel. Israel wao wanataka kutawala eneo lote la Middle East (chini ya Abrahamic Accords).