let the caged bird sings
JF-Expert Member
- Sep 19, 2020
- 4,179
- 9,750
Inasikitisha sana kuona kuna watu wanaupa kisogo ukweli mchungu kuhusu watawala wa Africa.Unawalaumu wazungu wakati viongozi wetu ndio chanzo cha haya yote yanayotokea.
Mugabe aliwatimua wazungu akatuaminisha waafrika kuwa mashamba watapewa wananchi wakaida, kinyume na matarajio yale mashamba waliyopokonywa wazungu walipeana viongozi wa serikali na chama(Zanu pf) tu na kama hiyo haitoshi Grace Mugabe amehusika kwenye uporaji wa ardhi za wananchi zilizokuwa zinatumika kwenye kilimo. Mashamba yote waliyopeana hakuna alieyaendeleza ijapokuwa vifaa walikuwa navyo ila maarifa na utayari haukuwepo. Mugabe huyohuyo baada ya kufanya yote hayo bado akataka kumuachia nchi mke wake hadi jeshi lilipoingilia kati na kutolewa madarakani.
Al Bashir alikuwa dikteta aliewageuza aliewageuza wananchi wake kuwa wafungwa wa nje. Kaongoza muda mrefu nchi ikiwa na vikwazo na ilikuwa wazi asingweza kuiletea mabadiliko yoyote chanya, busara ilikuwa kuondoka lakini akawa muuaji wa wanaomkosoa.
Gadaffi alikuwa dikteta aliewasupport madikteta wenzake kama Iddi Amini, mminyaji wa haki na demokrasia nchini kwake(alikuwa anawaua wapinzani wake kwa kuwanyonga mbele ya halaiki bila kwenda mahakamani na wengine walipotea tu)lakini kuna mabadiliko kadhaa aliyaleta pia.
Hao wote walitolewa na wazungu kwa kwenda kinyume nao lakini pia wananchi wa hizo nchi waliwachoka pia sababu ya ubinafsi na roho mbaya zao.
Na Unaposema Afrika hatuhitaji kuvushwa stage na demokrasia ya Marekani unamaanisha nini hasa? changamoto ulizotaja hapo zinaweza kutatuliwa kwa njia gani?
Et Mugabe nae ni shujaa!!! 😢😢