Third test si uliiona, kwanini unataja second attempt iliyofeli wakati third attempt iliyokuwa successful ipo. Marekani ina makampuni zaidi ya matano yanatengeza hypersonic missiles, nyinyi wajamaa hamjui dunia inaendaje. Urusi ina makampuni ya serikali ndio yanaunda, China ina institutes za serikali ila Marekani haina kampuni yoyote ya silaha inayomilikiwa na serikali badala yake ina DARPA ambayo ni taasisi ya tafiti za kijeshi tu na huwa haiundi silaha inatoa demo na kuwapa private contractors waunde.
Ndio maana SpaceX ya Elon Musk inafanya vitu Urusi nzima haiwezi. Waambie ROSCOSMOS pale Urusi watengeneze reusable spaceship uone. SpaceX ina rocket inaenda nje kisha inarudi na kutua chini inakuja kutumika tena. Warusi wataipata lini? Na hiyo sio kazi ya NASA bali wamechangia funds na utaalamu.
Boeing wana hypersonic missile program yao
View attachment 2607411
Lockheed Martin wana ya kwao ndio unayosema ilifeli
View attachment 2607413
Na bado makampuni mengine yanazo programu zao kama mabingwa wa makombora Raytheon Technologies.
Marekani ikitengeneza silaha haifyatuki na kuchagua kampuni moja, inaita tender ya wazi kila anayejiona anaweza aende. Hata mbongo kama una kampuni ya silaha unaweza weka bid Marekani. Kila silaha unayoona Marekani ujue nyuma yake kuna silaha nzuri ziliachwa ikachaguliwa nzuri zaidi. F-16 ilikuwa na competitor, F-22 ilikuwa nae, B-2 ilikuwa nae ila B-21 imeendelezwa kutoka B-2 hivyo walitumia single source. Future lift program ambayo Sikorsky walishinda mwaka jana mwaka huu Boeing amefungua kesi award irudiwe. Bell ndio ilishinda.
Mwaka jana standard rifle ya US Army wameshinda kampuni ya Ujerumani au Uholanzi kama sikosei na kampuni ya Marekani imeachwa ila bunduki yake ina teknolojia ya kisasa labda tutakuja iona miaka ijayo.
In short, Marekani itakuwa na kampuni zisizopungua mbili zenye hypersonic missiles tofautitofauti kama air launched na ship launched