Marekani yamuweka Magufuli njiapanda

Marekani yamuweka Magufuli njiapanda

Hiyo trillion moja tumekwisha kuipata kwenye makontena yaliyotoroshwa. Na bado tukibana mianya yote ya ukwepaji kodi na ufisadi hatuhitaji misaada yenye masharti ya kipuuzi. Mbona Mugabe amewatolea nje na bado anadunda!
Waulize wananchi wake mateso wanayopata, mkate tu ni sh 1mln na Mpaka sasa wanatumia sarafu ya A.kusini na marekani
 
Shida yoote hii ni ccm kutaka kubaki madarakani milele na milele au hadi kiama. Mdudu ccm ni hatari kwa ustawi wa jamii, hata Pombe analijua hilo.
 
Tutaelekea kwa marafiki zetu wa China, watupe misaada kwa mashariti nafuu.
Tukiwaambia tunataka pesa kwa ajili ya jambo fulani wanatoa tu, zipo hawana gozigozi.

By Mkwere wa Msoga.
 
Ni porojo tu, fedha zipo pale pale na hawana uwezo wa kuzizuwia.

Wanachotazama ni fedha zilizotolewa awali zimefanya nini na kama hizi zitatolewa zitafanya nini.

Ninajuwa fedha zitapatikana lakini kwa dhati kabisa ninatamani tusizichukuwe na tuwadhihirishie kuwa tuna uwezo wa kujiendesha wenyewe bila fedha za masharti.
 
China ipo wataleta hata trilion 3 bila masharti
 
Leo hainafaida ila ,kipindi cha mkwere mlikuwa mnaisifia sana alikuwa anaenda kuiomba...trilion moja sio mchezo.....umeme vijijini utakuwa ndo mwisho kwa Tanzania bila huu msaada

mkwere alikuwa ombaomba sana
 
Hawa sitaki hata kuwasikia na misaada yao. Wanajifanya kujipendekeza na misaada kumbe wana lao jambo. Wakae nayo, hatuitaki, naomba Magufuli awe nunda kwa hili
 
Hivi tunaangalia misaada tu au tunaangalia Future ya ndugu zetu wa Zanzibar? Hivi hatuna upeo zaidi ya pesa? Yaaani Wamarekani wanashinikiza ili ndugu zetu wasiingie kwenye machafuko halafu sisi tunashangalia eti pesa zenyewe trilioni moja tu? Kweli kuna watu uwezo wao wa kuona mambo ni mdogo sana.

Ishu sio pesa hapa ishu ni hatima ya maisha ya Wazinzabari ambao ni ndugu zetu, ambao haki yao ya kuchagua mtu wanayempenda imeporwa!
 
Majizi ya Kura yanataka kutuletea Balaa hapa.

Leo hainafaida ila ,kipindi cha mkwere mlikuwa mnaisifia sana alikuwa anaenda kuiomba...trilion moja sio mchezo.....umeme vijijini utakuwa ndo mwisho kwa Tanzania bila huu msaada

kodi ya trilioni moja kwa yale makontena labda kama yalikuwa yamebeba dhahabu! acheni kukuza mambo

Hizi ndizo comment positive tu, the rest wameongea utumbo! Mungu awabariki kwa kuona mbali, maana kinachozungumziwa hapa sio pesa bali haki ya kuchagua Rais wanayempenda wazanzibar. Tukiwa na hizo pesa sijui za makontena halafu Zanzibar kukawa na vita bado hatutabakia salama! Hatuweza kusogea mbele. Asanteni mmewaza mbali hao wanaona pesa za makontena ngoja wasubiri na makontena mengine kama yatakuepo. Hata hivyo kodi yenyewe ya makontena haijulikani ni bei gani.... kila mtu anakuja na hesabu zake za kichwani tu
 
Kwa maoni yangu, naomba deadline waliyoitoa(wanayofikiria kuiweka) ifike kabla hatua ya utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar wanayotaka wao iwe haijafikiwa halafu tuone nini kitafuata. Nasema hivyo nikiwa naamini kwamba hakuna cha MCC wala msaada wowote kutoka IMF,World Bank marekani na washirika wao ambao huwa hauna manufaa kwao. Kama wamefanya analysis zao na kujiridhisha kwamba utoaji wa fedha hizo kwa Tanzania una manufaa kwao watazitoa tu hata kama matokeo ya uchaguzi Zanzibar yatatangazwa mwezi June 2016(provided kwamba kuna hali ya utulivu kama ilivyo sasa)
Mtazamo wangu mwingine juu ya hili suala ni kwamba, watanzania na waafrika kwa ujumla ifike mahali tuwe na uhuru wa fikra,tujiamini na tufanye maamuzi yenye manufaa kwetu na nchi zetu bila kuingiliwa na mataifa ya kigeni. Ni kweli kuna utata ulioibuka juu ya uchaguzi Zanzibar, kila upande ukijiona kuwa unataka kudhulumiwa haki yake. Kwenye sintofahamu kama hiyo busara ndiyo hutumika,kuna msemo ambao umeanza kuzoeleka sana siku hizi "matatizo ya Zanzibar yatamalizwa na wanzanzibar wenyewe" . Japokuwa linaweza lisiwe na ladha nzuri katika muktadha wa muunguno lakini ukweli unabaki kuwa wanzanzibar ndio watakaokuwa front line kulimaliza hili. Ndio maana limeundwa jopo likiwahusisha Ali Hassan Mwinyi,Abeid Karume ,Sharif Hamad na Mohamed Shein. Mazungumzo yakiwa yanaendelea anajitokeza marekani na kisingizio cha MCC ku-pressurize. Nilidhani hizi nchi wahisani ziache kuchochea migogoro kwa visingizio vya misaada,na sisi waafrika tusiingize ushabiki kwenye suala nyeti kama hili. Tuwaache wenye dhamana ya kushiriki mazungumzo wazungumze ili muafaka upatikane
 
Wachina ni waangalifu sana hawatoi mikopo kipuuzi. Wakitoa mikopo wanahakikisha sehemu kubwa ya hiyo hela inarudi kwao kwa njia ya ajira na vifaa toka china.
 
Katika suala la misaada kutoka mataifa Tajiri kwa nchi za Africa alikwepeki.

Hata kama wakikitoza kodi hadi pesa zako zote zilizomo kwenye kibubu chako bado huna ujanja wa kutotegemea misaada ya nje.

Muulize Mugabe atakwambia
Hii ni imani potofu; ni matokeo ya kuzowea matumzi yaliyo nje ya uwezo wetu. Angalia eti sherehe za uhuru zinapangiwa bajeti ya mabilioni ilihali tunajua hatuna uwezo huo mpaka tupewe misaada. Kinachotakiwa ni kupanga bajeti inayoendana na uwezo wa Taifa. Hakuna haja ya kuwa na sherehe, semina makongamano, posho na gharama nyingine kubwa ambazo hatuna uwezo nazo.
 
I think its unfair to magufuli... Muungano kwa kiasi kikubwa una mambo makubwa kuliko yeye
Alipochukua fomu ya kugombea "Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zimbabwe hakulijua hilo?

Muungano hauna makubwa yoyote, ni unafiki na usanii tu.

Magufuli amewezaje kumteua Lukuvi katika Serikali anayoiongoza baada ya Lukuvi "kuharisha kule kwa Kanisa"?

Hili nalo ni kubwa kuliko Magufuli? Lukuvi ni jambo kubwa kuliko Magufuli?

Katika hutuba alipofungua bunge la "mipasho na ubabe" alisema ataulinda Muungano. Kama Muungano una mambo makubwa ni kweli ataweza kuulinda?

Mambo makubwa yepi hayo?





Na Katiba Mpya ya wananchi pia utasema ina mambo makubwa kuliko Magufuli.

Ndio sababu , tunasema ni unafiki na usanii tu.

Muungano ni kiinimacho cha CCM cha kuweza kuendelea kuwatawala wadanganyika tu.

Hoja yako ni hoja ya hovyo tu kama hoja za Lukuvi.
 
Last edited by a moderator:
APEWE MAALIM SEIF TU,KWANI TATIZO LIPO WAPI,TUACHE WOGA WA KIJINGA.
SOTE TUNAJENGA TANZANIA YETU
TATIZO LIPO WAPI?
ii
 
Hiyo trillion moja tumekwisha kuipata kwenye makontena yaliyotoroshwa. Na bado tukibana mianya yote ya ukwepaji kodi na ufisadi hatuhitaji misaada yenye masharti ya kipuuzi. Mbona Mugabe amewatolea nje na bado anadunda!
Kwa hiyo tukose trillion moja na nusu kwa sababu CCM hawataki kushindwa? We ni juha nini?
 
Back
Top Bottom