Marekani imeiweka njiapanda Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, baada ya Bodi ya shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) kuamua kukutana kesho kujadili masuala kadhaa ya utoaji wa misaada kwa nchi zinazoendelea huku angalizo lake kwa serikali ya Tanzania kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar likiwa bado halijapatiwa ufumbuzi.
Tofauti na fedha zinazotolewa na wafadhili wengi duniani, fedha za MCC hazitakiwi kurudishwa na nchi inayopewa fedha hizo na pia nchi husika hupewa uhuru wa kuchagua aina ya miradi ya maendeleo ambayo inataka igharimiwe na fedha hizo.
Katika fedha za awamu ya kwanza za MCC, Tanzania ilipata dola za Marekani milioni 698 (Sh.trilioni 1.46), ambazo tayari zimesaidia kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya barabara na usambazaji wa umeme vijijini
CHANZO: NIPASHE