Marekani yajitoa rasmi WHO

Sasa huoni kuwa kujitoa kwa USA ndio wanazidi kujiweka katika wakati mbaya zaidi

Maana WHO ni shirika ambalo linachangia kuzisaidia nchi nyingi kiafya ulimwengu ..endapo china ataweza kumudu kulipa shirika hilo pesa nyingi za kujiendesha halafu shirika hilo likawa linaendelea kutoa misaada katika nchi wanachama bila ya kutetereka ..bila shaka china itafanikiwa kuongeza ushawishi wa kisiasa katika mataifa mengi duniani hivyo basi itaifanya china kuzidi kupaa kiuchumi na kuogopeka zaidi kauli ya china itakuwa ni amri kwa hayo mataifa wanachama kama ilivyo kuwa USA kwa mataifa mengi miaka kadhaa iliyopita
 
Imejitenga au imetangaza nia ya kujitenga?

Hayo ni mambo mawili tofauti kama kutangaza nia ya kuwa mbunge na kuwa mbunge.
 
Hapana, huo ni uamuzi wa Trump tu; bunge halikuhisiki. Rais pekee ndiye ana mamlaka ya kuamua mambo yote ya nje ya nchi.

Watanzania tuna ugonjwa wa kuamini kuwa Tanzania ndio tunaofanya hovyo tu mpaka tunajitungia mambo ya kuhalalisha ugonjwa huo.
 
Hapana, huo ni uamuzi wa Trump tu; bunge halikuhisiki. Rais pekee ndiye ana mamlaka ya kuamua mambo yote ya nje ya nchi.

Watanzania tuna ugonjwa wa kuamini kuwa Tanzania ndio tunaofanya hovyo tu mpaka tunajitungia mambo ya kuhalalisha ugonjwa huo.
Sio kweli, acha upotoshaji, labda unaiongea Russia, China, Tanzania au nchi zingine sampuli hiyo.

Marekani uamuzi wa Congress unaweza ku-overule uamuzi wowote wa rais. Marekani uamuzi wa mtu mmoja hauwezi ukaamua hatima ya nchi. Marekani sio Banana Republic.
 
China itoe pesa kuziba nafasi ya Marekani?? Wewe huijui China na hata huo uwezo hawana.

Umesikia wenyewe China wamekiri wazi kuwa kuondoka kwa Marekani WHO itakuwa ni pigo kubwa kwa nchi maskini duniani. Unafikiri ni kwa nini wamekiri hivyo.
 
Kwamba Trump yeye toka angeingia ni kulaumu tu hajafanya chochote. Kwamba toka corona imeingia Marekani Trump hajafanya chochote?

Haya umeyaona au kuyasikia wapi?

Ni ukweli usiopingika kua WHO imeshirikiana na China kuihadaa Dunia. Sasa China atoe hela.

Wabunge wa Republican wamesema hawawezi kutoa hela kufadhili shirika ambalo limeshindwa au limeshirikiana na China kudanganya kuhusu corona.

Toka corona imeanza WHO wamekua wanatoa kauli zinazopingana kama wanasiasa balada ya kua chombo cha kisayansi na kitaalam. Leo wanasema hivi kesho wanasema vile.

WHO walishindwa hata kukemea ubaguzi ukiotokea China dhidi ya watu weusi kwa sababu ya corona.

Ni kiongozi taahira tu ataendelea kufadhili ujinga kama huo.
 
China itoe pesa kuziba nafasi ya Marekani?? Wewe huijui China na hata huo uwezo hawana.
China ikifika kwenye kuchangia inajiweka third world ila kwenye masuala ya biashara inajiweka first world..

Kwenye hili suala la Corona WHO walikosea kupanga namna ya kupambana na Virusi matokeo vikasambaa dunia nzima.Acha Marekani akae pembeni tuone ukubwa wa China.
 
Bila ushahidi kuhusiana na UCHINA zitakua nitetenasi tu kama mingine.....
 
Mimi ninakaa hapa Marekani kwa miaka 26 sasa kwa hiyo ninaijua vizuri kuliko unavyodhani. Congress haina sauti na maamuzi yanayohusu mambo ya nje; Congress inaweza ku-overule veto ya rais kwenye miswada ya sheria tu, tena kwa supermajority, lakini siyo mambo ya foregn policy. Trump aliposema anafungia watislamu kuja Marekani, Congress haikukubaliana naye lakini haikuwa na la kufanya kwani hiyo ilikuwa ni foregn policy ambayo haiko kwenye power zake. Soma katiba ya Marekan Article 2 uonde madaraka ya rais.
 
Kuna mengi huyajui kuhusu WHO kushiriakana na China na vile vile hujui kazi za WHO. Hao siyo bwana afya au hospitali ya kulaumu wakati magonjwa yanapotokea; majuukumu yao nimyaweka hapa. Taarifa za Ugonjwa zilianza zamani sana, ingawa haikuwa inajulikana namna unavyosambaa. WHO ilitoa taarifa zote kulingana na information iliyokuwepo wakati huo. Ukisoma katiba ya WHO utakuja majukumu yake ni haya,
  1. To act as the directing and coordinating authority on international health work;
  2. To establish and maintain effective collaboration with the United Nations, specialized agencies, governmental health administrations, professional groups and such other organizations as may be deemed appropriate;
  3. To assist Governments, upon request, in strengthening health services;
  4. To furnish appropriate technical assistance and, in emergencies, necessary aid upon the request or acceptance of Governments;
  5. To provide or assist in providing, upon the request of the United Nations, health services and facilities to special groups, such as the peoples of trust territories;
  6. To establish and maintain such administrative and technical services as may be required, including epidemiological and statistical services;
  7. To stimulate and advance work to eradicate epidemic, endemic and other diseases;
  8. To promote, in co-operation with other specialized agencies where necessary, the prevention of accidental injuries;
  9. To promote, in co-operation with other specialized agencies where necessary, the improvement of nutrition, housing, sanitation, recreation, economic or working conditions and other aspects of environmental hygiene;
  10. To promote co-operation among scientific and professional groups which contribute to the advancement of health;
  11. To propose conventions, agreements and regulations, and make recommendations with respect to international health matters and to perform

Trump aliambiwa Ugonjwa wa corona tangu mwezi wa 11 na wala hakujiandaa kukabiliana nao. Mara nyingi Marekani ilikuwa inadhibiti usambaaji wa magonjwa kwa kuyadhibiti kabla hayajaingia, ilishindwa Ukimwi tu kwa vile ulianzia hapa hapa. Makini magonjwa kama Ebola, Evian flu na swine flu ya aina zote yalidhibitiwa kabla hayajaingia ndani. Trump alipoambiwa kuwa kuna Corona virua huko China, yeye hakufanya lolote kuudhibiti ungali haujaingia ndani; msikilize hapa.


Sasa anaona ameelewa ndiyo anatafuta wa kualaumu na kwake yeye WHO ni target nzuri sana kwa sababu mojawapo ni kwa director wake ni mtu mweusi wa kutoka "shithole countries"

Kwake yeye manbo yakienda vizuri, anadai credit, na yakienda hovyo, anatafuta kisingizo cha kulaumu.
 
Basi Marekani ana haki ya kujitoa. Ameshajitoa. WHO aendelee na ushirikiano wake na China ambao hatuujui kama unavyosema, kwani shida iko wapi? China achukue nafasi ya USA mambo yaishe.
 
Basi Marekani ana haki ya kujitoa. Ameshajitoa. WHO aendelee na ushirikiano wake na China ambao hatuujui kama unavyosema, kwani shida iko wapi? China achukue nafasi ya USA mambo yaishe.
CHINA hakuwahi kusema kma anaitaka nafasi ya US ila kama ataweza kuchukua pia sio mbaya

US kaishajitoa kwa WHO awache kulia lia sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…