Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,607
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo amesema Marekani itajitoa kwenye mkataba huo Februari 2, akiongeza kuwa ikiwa Urusi haitarudi katika njia ya kuheshimu utekelezwaji wa mkataba huo, basi utavunjika.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo ametangaza kuwa Marekani inajitoa kwenye mkataba kati ya Marekani na Urusi wa kuzuia urundikiaji wa silaha tangu kumalizika kwa Vita Baridi.
Kujiondoa kwa Marekani kumekuwa kukitarajiwa kwa miezi kadhaa. Hatua hiyo imetokana na mzozo ambao haujasuluhishwa kwa miaka mingi wa madai kuwa Urusi imekuwa ikikiuka mkataba huo ulioafikiwa mwaka 1987 ambao unapiga marufuku baadhi ya makombora ya kufyatuliwa ardhini. Urusi imekana madai ya kukiuka mkataba huo.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo amesema Marekani itajitoa kwenye mkataba huo kesho Jumamosi, akiongeza kuwa ikiwa Urusi haitarudi katika njia ya kuheshimu utekelezwaji wa mkataba huo, basi utavunjika. Pompeo ameeleza kuwa:
''Tuliipa Urusi muda wa kutosha wa kurekebisha mienendo yake na kujitolea kikamilifu kuheshimu mkataba wa INF. Muda huo unamalizika kesho lakini Urusi imekataa kuchukua hatua yoyote ya kurejesha hali halisi na inayoweza kuthibitishwa ya kuheshimu mkataba katika kipindi cha siku 60 tulizoipa. Kwa hivyo kuanzia kesho, Jumamosi, Marekani itajiondoa kwenye mkataba huo''
DW