Marekani yaitumia Islamic State Kuivamia Philippines

Bowie

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
4,373
Reaction score
6,084
Rais wa Philippines Duertete amesema serikali ya Marekani kupitia magaidi wa Islamic State wamevamia jimbo la mindanao na kuuteka mji Mkuu wake Marawi. Vita katika mji huo mkuu umechukua wiki 3 na mpaka sasa majeshi ya Philippines yameshindwa kuwaondoa wapiganaji ISIS. Raia na wanajeshi wengi wamepoteza maisha yao.
Toka Rais Duertete aingie madarakani ameonyesha chuki kubwa kwa nchi za magharibi mpaka ilifikia hatua kumwita aliyekuwa Rais wa Marekani Barrack Obama mwanaharamu, uhusiano wa nchi hiyo na marekani umezorota sana kiasi ambacho Rais Duertete aliamuru majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo. Hawa magaidi wa ISIS wanapigana huko Syria na Iraq kwa msaada wa serikali ya Marekani kupitia shirika lake la ujasusi CIA
Imebidi kwa Rais Duertete kuipigia magoti Marekani ili imsaidie vita hivyo. Kwa miaka mingi nchi ya Philippines ilikuwa na vita na kikundi cha kigaidi Abusayaf lakini haikuwa kutokea vita vikubwa kama zilizotokea wiki 3 zilizopita.
 
Ukiambiwa ni marekani wako nyuma ya hii kitu unaweza usibishe maana jamaa kafukuza US Army kutoka Philipines, ISIS tunaaminishwa wana bif na marekani hawana sababu ya kuvamia nchi ambayo imewafukuza wamarekani.
 
Bahati mbaya sana Dunia inapambaa na kitu wasichokijua, kwani stage ya kwanza kupambana na kitu chochote kwanza ni kukijua kuanzia mienendo yake na wao ni kina nani kutofautisha na wengine, cha kushangaza mpaka leo DUNIANI hakuna tafasiri moja inayoelezea Gaidi ni nani zipo zaidi ya tafasiri 15 ambazo zinaelezea gaidi ni nani lakini wataalamu wa maswala ya matukio ya mashambulizi ya kustukiza na yenye kuleta hofu wameshindwa kukubaliana maana sahihi ya UGAIDI na GAIDI ni nani na wanaposhindana ni vigezo vipi vinatumika kumuita mtu gaidi? au ni vigezo gani vinatumika kumtoa mtu kuitwa gaidi? mfano wapigania Uhuru wote (freedom fighter) walikuwa wanaitwa magaidi mfano Mandela lakini kwa waafrica tulikuwa tunamwona kama mpigania uhuru na haki za waafrica weusi nchini South Africa lakini makaburu na wazungu walikuwa wanamuona ni Gaidi na aliwekwa mpaka kwenye list ya Magaidi Duniani amekuja kufutwa kwenye list tena mmoja wa viongozi wakuu Duniani Margaret Thatcher aliwai kumuita Mandela na ANC kuwa ni “typical terrorist" haya kuna nchi duniani zinavamia nchi zingine na kufanya mauaji ya kinyama mfano Israel wanavyofanya kwa watoto wa kiparestna je hule ni nini?

Leo kundi la (ISIS) inasemekana wanapata ufadhiri kutoka US sasa unajiuliza hawa magaidi na hawa wapinga ugaidi wana mpango gani tena? nadhani ni wakati sahihi ktk kupambana na ugaidi na magaidi duniani siku wapambana na ugaidi wakiwa serious kupambana na ugaidi tutapata tafasiri moja ya ugaidi ni nini na gaidi ni nani na wote tutajua tunapambana na nani na nina uhakika ugaidi utakuwa history kama ilivyokuwa ucominist
 
ISIS ni kikundi cha kigaidi kinachotumiwa na Marekani na kikundi hiki huwa hakuna ugomvi na Marekani.
Urusi ndio waliweza kukipiga kikundi hiki huko Syria mpaka nguvu ya kikundi hiki kikapungua.
 
Bahati mbaya sana Dunia inapambaa na kitu wasichokijua, kwani stage ya kwanza kupambana na kitu chochote kwanza ni kukijua kuanzia mienendo yake na wao ni kina nani kutofautisha na wengine, cha kushangaza mpaka leo DUNIANI hakuna tafasiri moja inayoelezea Gaidi ni nani zipo zaidi ya tafasiri 15 ambazo zinaelezea gaidi ni nani lakini wataalamu wa maswala ya matukio ya mashambulizi ya kustukiza na yenye kuleta hofu wameshindwa kukubaliana maana sahihi ya UGAIDI na GAIDI ni nani na wanaposhindana ni vigezo vipi vinatumika kumuita mtu gaidi? au ni vigezo gani vinatumika kumtoa mtu kuitwa gaidi? mfano wapigania Uhuru wote (freedom fighter) walikuwa wanaitwa magaidi mfano Mandela lakini kwa waafrica tulikuwa tunamwona kama mpigania uhuru na haki za waafrica weusi nchini South Africa lakini makaburu na wazungu walikuwa wanamuona ni Gaidi na aliwekwa mpaka kwenye list ya Magaidi Duniani amekuja kufutwa kwenye list tena mmoja wa viongozi wakuu Duniani Margaret Thatcher aliwai kumuita Mandela na ANC kuwa ni “typical terrorist" haya kuna nchi duniani zinavamia nchi zingine na kufanya mauaji ya kinyama mfano Israel wanavyofanya kwa watoto wa kiparestna je hule ni nini?

Leo kundi la (ISIS) inasemekana wanapata ufadhiri kutoka US sasa unajiuliza hawa magaidi na hawa wapinga ugaidi wana mpango gani tena? nadhani ni wakati sahihi ktk kupambana na ugaidi na magaidi duniani siku wapambana na ugaidi wakiwa serious kupambana na ugaidi tutapata tafasiri moja ya ugaidi ni nini na gaidi ni nani na wote tutajua tunapambana na nani na nina uhakika ugaidi utakuwa history kama ilivyokuwa ucominist
Kwasasa magaidi wamekuwa tools za nchi za magharibi katika kutetea maslahi yao. Nitakupa mfano Seif Islam aliyekuwa mtoto wa Ghadaffy aliachiwa na magaidi huko Libya baada ya kukaa jela miaka sita leo ICC badala ya kuwakamata walioanzisha vita vya Libya sasa wametangaza seif islam akamatwe apelekwee the Hague kushitakiwa. Rais Sisi wa Misri aliyepindua serikali ya kidemokrasia na kuua maelfu ya watu yuko huru.
Hiyo ndio sura 2 za nchi za magharibi.
 
Ila hii habari tumelishwa matango pori, kwa mujibu wa Dairy Mirror la uk, usa wameenda Marawi kumsaidia Durtete kupambana na isis
 
Back
Top Bottom