ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,418
- 9,599
Ikulu ya Marekani siku ya jumatatu imeeleza kwamba imepata ushahidi madhubuti kwamba Syria inajiandaa kufanya shambulizi lingine la silaha za kemikali, imeonya kwamba kama Syria itafanya hivyo bhasi italipia gharama kubwa sana kama itatekeleza shambulio hilo.
White House statement on Syria
Marekani imesema kwamba ina ushahidi wa kwamba Syria chini ya serikali ya Asaad imekua kwenye maandalizi mazito ya kufanya shambulizi lingine la kemikali ambalo litapelekea mauaji makubwa ya raia pamoja na watoto wasio na hatia yoyote.
Tweet ya balozi wa Marekani UN kuhusu shambulio hilo
Kwenye taarifa hiyo ikulu ya Marekani imeeleza kwamba iwapo Assad atafanya tena shambulio baya la kemikali bhasi yeye pamoja na jeshi lake watalipia gharama kubwa.
Meli ya Marekani (USS Porter) ikirusha makombora ya Tomahawk toka bahari ya Mediterranean kuelekea Syria baada ya shambulio la kemikali lililofanyika April