Marekani yaituhumu Syria kupanga shambulizi lingine la kemikali,yaonya kwamba italipia gharama kubwa

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
6,743
2,000
Ikulu ya Marekani siku ya jumatatu imeeleza kwamba imepata ushahidi madhubuti kwamba Syria inajiandaa kufanya shambulizi lingine la silaha za kemikali, imeonya kwamba kama Syria itafanya hivyo bhasi italipia gharama kubwa sana kama itatekeleza shambulio hilo.
4a64471d492342a926438ab8ccbaa4f5.jpg
White House statement on Syria

Marekani imesema kwamba ina ushahidi wa kwamba Syria chini ya serikali ya Asaad imekua kwenye maandalizi mazito ya kufanya shambulizi lingine la kemikali ambalo litapelekea mauaji makubwa ya raia pamoja na watoto wasio na hatia yoyote.

4b1eaf7f1aed433c3ddc51f4be59cd06.jpg
Tweet ya balozi wa Marekani UN kuhusu shambulio hilo

Kwenye taarifa hiyo ikulu ya Marekani imeeleza kwamba iwapo Assad atafanya tena shambulio baya la kemikali bhasi yeye pamoja na jeshi lake watalipia gharama kubwa.
acfc3514954a890a502327ddd50d43c0.jpg
Meli ya Marekani (USS Porter) ikirusha makombora ya Tomahawk toka bahari ya Mediterranean kuelekea Syria baada ya shambulio la kemikali lililofanyika April
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,165
2,000
DDP8IYMWAAEOU1O.jpg:small
.

Marekani kwanini hawaishi kulalama lalama .

Au bado hawajaridhika kuwa wameshamshindwa assad,kila mbinu inagonga mwamba leo mwaka 6 ,lengo halijatimia
 

The Proudly African

Senior Member
Jun 22, 2017
139
250
Tukumbushane tu, Tuhuma kama hizi ilipewa Iraq, baadae kwa maneno matatu tu blair aliushangaza ulimwengu WE WERE WRONG.. nini gharama ya waliouawa...
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
38,803
2,000
Syria haitaweza fanya huvyo na kama ikifanya basi ni kichwa ngumu
 

error term

JF-Expert Member
Jan 29, 2017
388
1,000
Huyo mbabe wa dunia kwa North Korea kimemkimbiza nin, kabweka kama mbwa koko saiz kimya anamuomba china aongee nae wamalize kikubwa baaba ya stori zake zakudanganya wapenda mapicha kufail.
Ye ubabe wa dunia anauonyesha kwa nchi zilizo dhaifu ila zile ngum anapita pemben, siku akitokeza anakuja na propaganda za NASA, wapenda mapicha hapo wanaona Marekan kamaliza kila kitu.
Mnajidanganya sana sana
(Mtu unamshabikia marekan anauwezo kwakuwa anawekeza sana kwenye utafit wa sayansi vita sawa, lakin mkumbuke gharama ya labor marekan ni kubwa sana, kaz moja inayo fanyika china na marekan, kwa ufanisi sawa mwajiri wa marekan atatumia pesa nyingi kulipa mshahara kuliko china kwa kitu hicho hicho) ndio maana makampun mengi ya marekan yamewekeza nje kukwepa gharama. Kama wangeweza na techinologia ya jeshi kufanya nje ya marekan gharama ingepungua zaid.

Lakin nchi kana russia, china nk wote labor cost ipo chini sana na technologia inakuwa kwa kasi maana imekuwa cheep kwao, hilo marekan anajua na analiogopa pia.
Mogogoro wa syra US na Russia wanapigana in indirect way maana ngumi kuwahi, lazima kila mmoja atafute sababu za pemben ndio aweze kufanya tukio, ila wakisha ingia mazima us awezi baki hapo hata iweje.

Nchi ikisha jiingiza ktk migogoro vitu inaathirika sana ktk soko la mitaji na kuuwa uchimi wake. Umtakumbuka world economic crisis ya 2008 ilisabibishwa na nin, japo wanajitetea kutokana na failure ya financial market ila vita ya iraq ilichangia kwa kiwango kikubwa.

Mtazo wa dunia ya sasa umebadilika sana na mataifa mengi yameanza kujitegemea hasa kitechnologia ikiwa na china
Ndio maana china kazuia google na bado anasonga mbele kwa kasi sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom