Marekani, Ulaya Wasusia Kuapishwa Dr. Shein

Marekani, Ulaya Wasusia Kuapishwa Dr. Shein

Mabalozi kutoka Marekani na Nchi za Umoja wa Ulaya, wameendelea kuonyesha msimamo wao wa kutoridhishwa na uchaguzi wa marudio Zanzibar baada ya jana kususia mwaliko wa kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.

Wanadiplomaasia hao walipewa mwaliko rasmi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), lakini waliiambia kuwa hawatashiriki sherehe hizo.

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje Zanzibar, Silima Kombo Haji, aliliambia Nipashe kuwa serikali ilitoa mwaliko rasmi kwa Mabalozi wote wa nchi za Afrika na Ulaya kuhudhuria sherehe hizo, lakini Mabalozi wa Umoja wa Ulaya na Marekani walijibu kuwa hawatahudhuria bila kutoa sababu zozote.

“Tumewaalika na mialiko imewafikia na kutujibu kuwa hawatahudhuria. Hatukuwa na sababu ya kuwang’ang’ania,” alisema Haji.

Hata hivyo, alisema licha ya Mabalozi wa Marekani na Umoja wa Ulaya kutohudhuria sherehe hizo, Mabalozi wa nchi nyingine walioalikwa walihudhuria sherehe hizo na wengine kutuma wawakilishi wao.

Aliwataja Mabalozi wa nchi waliohudhuria sherehe hizo ambao wengi ni kutoka nchi za Afrika kuwa ni Balozi wa Cuba, Zimbabwe, DRC, Indonesia, Iran, Kenya, Kuwait, Malawi, Msumbiji na Oman.

Wengine ni Palestina, Ruwanda, Algeria, Angola, Burundi, China, Japan, Libia, Pakistan, Umoja wa Nchi za Kiarabu, India, Uganda, Uturuki, Urusi na Mratibu Mkaazi wa UN.

Nipashe lilipomuuliza Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer, endapo walipata mwaliko huo na sababu za kutohudhuria sherehe hizo, alisema ushirika wao usingeakisi dhamira ya tamko lililotolewa na Balozi mbalimbali nchini Machi 21, mwaka huu.

Tamko hilo lilitolewa na Mabalozi na Wawakilishi wa nchi za Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Hispania, Sweden, Switzerland, Uingereza na Marekani.

“Tumesikitishwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) wa kuendesha marudio ya uchaguzi uliofanyika 25 Oktoba 2015, bila kuwapo makubaliano ya pamoja baina ya pande kinzani na ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani humo uliotokana na majadilino baina ya pande husika.

“Ili uwe wa kuaminika na kukubalika ni lazima mchakato wa uchaguzi uwe jumuishi na unaowakilisha kwa dhati matakwa ya watu,” lilisema tamko lao la awali na kuongeza:

“Tunarejea wito wetu kwa Serikali ya Tanzania kuonyesha na kuchukua uongozi katika suala la Zanzibar na kujielekeza katika kupatikana kwa ufumbuzi wa mgogoro huu kwa kupitia mazungumzo baina ya pande husika kwa lengo la kudumisha amani na umoja.”

Mabalozi wamekuwa na msuguano na Serikali ya Zanzibar kwa kupinga kitendo cha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kufuta uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kwa kile wanachodai kuwa haukuwa na kasoro yoyote na kwamba ulikuwa huru na haki.

Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salim Jecha, Oktoba 28, mwaka jana, alifuta uchaguzi mkuu kwa madai kuwa haukuwa huru na haki, lakini waangalizi wa kimataifa wakisema kuwa ulikuwa huru na haki.

Wanadiplomasia hao hawakufurahishwa na kitendo cha Mwenyekiti huyo wa Zec kufuta uchaguzi, hivyo kutounga mkono uamuzi wa Zec kurudia uchaguzi ambao ulifanyika Machi 20, mwaka huu na Dk. Shein kushinda kwa kura 299,982 sawa na asilimia 91.4.
Waache hao wazungu ni malofa.
 
Mwakilishi wa UN alihudhuria!
Kwa hiyo nchi wanachama wote wa UN walihudhuria kwa kuwakilishwa!
 
....eti wenyewe wanadai hawababaishwi na chochote watakula hata nyasi....te te te , kwani wao wataumia basi ?/ maumivu kwa WANYONGE, wao ni tambarare...../ ULAFI NA UBABE WA VIONGOZI WA AFRICA.
 
Kwenye jumuiya za kimataifa kama Umoja wa mataifa,Umoja wa nchi huru za Afrika nk nchi inayotambuliwa ni ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.Mabalozi kwa kutambua hilo walihudhuria kuapishwa kwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania lakini hawakwenda Zanzibar kuhudhuria kuapishwa kwa Dr.SHEIN kwa sababu Zanzibar si nchi mwanachama wa umoja wa mataifa,jumuiya ya madola wala umoja wa Afrika,wala jumuiya ya madola.

Walifanya sawa nawapongeza hao mabalozi kwa kuligundua hilo na waendelee hivyo hivyo wasije kanyaga kuapishwa kwa raisi wa Zanzibar.
 
ujinga ni pale unapomsahau mwenyezi Mungu na kuwasujudia binadamu wenzako.. Huu ni msiba mkubwa sana..
 
Malofa nini wale wanaosherekea msiba
Ni kweli mkuu lofa ni yule asiyejua kuwa bajeti yetu ya mwaka huwa haitoshi hadi wazungu wachangie au anadhani hayo makusanyo ya trilioni moja na nusu ya mwezi yatatosha hadi Zanzibar??
 
mkuu YEHODAYA watu hawalitambui hilo. Fikra na mitizamo yao wameijenga kwa kuamini kuwa wazungu ni muhimu kuliko wao.. Wanaposusa mabalozi wa uingereza, marekani na wenginewe hakumaanishi kwamba wapo wao tu. Kuhudhuria kwa Mabalozi wa Nchi nyingine ikiwemo Urusi ni kuonyesha hawataki kuwa wapumbavu kama mleta Andishi hili hapa Jukwaani
 
Hao waliosusia (Ulaya na Marekani) ndiyo wenye dunia. Wakikukataa utabaki na sharubu zako tu! Zanzibar ni msiba jamani.
 
Kaka upo? Nipo zigua mwenzio nawaona wazigua walivyoamka bado wewe kaka yangu
mimi nilishaamka kabla ya hao unawaona ndio maana tumeamua kujiondoa kwenye kusujudia binadamu wenzetu. Kazi kwenu wamiliki wa saccos ya Ufipa.. Ipo siku mwenyekiti atahitaji na hamtakataa
 
Lakini dunia inawashanga
Yaani kwako dunia ni hako ka-europe + ka-usa! Yaani hawa waliotufanya koloni lao tangia 1888 walipogombania kuligawana bara letu! Na hadi leo hawataki kuliachia. Wanaendelea kutunyonya rasilimali zetu, yaani hadi tumbili zetu wanachukuwa!! Huto mnatotuita misaada kwetu ni peanut ya wanayopora kwetu! Halafu wewe na akili yako unaamini kuwa hatuwezi kuishi bila misaada ya watu hawa! You must be ashamed of yourself. Do you think we need them to continue reuting our resources so as to get peanut OR is it them who need us at any cost for survival??
Jamani Waafrika tuamkeni. Hawa wazungu si watu wema na wala si ndugu zetu. Tujivunie bara letu. Ndugu zetu ni watu wa Cuba, Arabia, India, China, Urusi, bara Asia, Amerika ya kusini nk. Hawa tuna vitu vingi tunafanana, na wote tulishaonja au tunaendelea kuonja machungu ya hawa europe + usa. Mr. Trump ametupatia siri ya dira vision ya watu hawa ambayo ni kutufanya kuwa makoloni yao tena ya waziwazi. Sasa hivi sisi ni makoloni yao kwa njia za vificho!

Nadhani umenielewa.
 
Back
Top Bottom