Marekani Kuupiga Mabomu Mwezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekani Kuupiga Mabomu Mwezi

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Oct 7, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Jinsi mwezi utakavyolipuliwa

  October 07, 2009

  Marekani ina mpango wa kupeleka chombo chake angani ambacho kitaupiga mabomu mwezi ikiwa ni mojawapo ya hatua ya utafiti unaoendelea wa kugundua kama kuna maji kwenye mwezi. Shirika la utafiti wa anga la Marekani (NASA) linajiandaa kuzindua mpango wake unaoitwa LCROSS (Lunar CRater Observing and Sensing Satellite) ambapo mwezi utapigwa mabomu katika harakati za NASA kugundua kama kuna maji angani.

  Katika mpango huo kombora linaloitwa Centaur ambalo linaenda spidi mara mbili ya spidi ya risasi litatumika kuulipua mwezi ili kutengeneza shimo kwenye mwezi.

  Wanasayansi wa NASA wanasema kwamba mlipuko utakaotokea utakuwa mkubwa sana kiasi cha kwamba vipande vikubwa vya vifusi toka kwenye ardhi ya mwezi vitaweza kuonekana kutokea duniani kwa kutumia darubini kubwa.

  Mabomu hayo yamepangwa kulipuliwa kwenye mhimili wa kusini wa mwezi ambako wanasayansi wanaamini mabilioni ya barafu zilizoganda yanapatikana mita kadhaa chini ya ardhi ya mwezi.

  Chembe chembe za vumbi la mwezi zitafanyiwa uchunguzi ili kugundua kama kuna dalili ya kuwepo kwa maji yaliyoganda au mvuke.

  Kugundulika kwa maji kwenye mwezi kutasaidia sana safari za baadae za utafiti wa anga.

  "Kusafirisha maji na vifaa vingine kutoka duniani hadi kwenye uso wa mwezi ni gharama sana" NASA lilisema na kuongeza "Kupatikana kwa maji au barafu kwenye mwezi kutasaidia kupunguza gharama za safari za kwenda mwezini".
   
 2. Robweme

  Robweme Senior Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mmmm!!!, tunakoelekea sasa, tutajimaliza wenyewe na tutatengeneza Sodoma wenyewe bila hata kuletwa na Mwenyezi Mungu, haya ngo tuone.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Du ...kweli sasa hali imefika kubaya...lakini anyway, ni utafiti tu...kwani maendeleo yote ya sasa ya kisayansi yalianza kwa kuthubutu kama hivyo!

  Vitu vya hatari sana kama madini ya Uranium, ambavyo kutokana na Teknolojia tu inatumika kuzalisha umeme wa Nyuklia vingelaumiwa sana na sisi maskini endapo tungekuwa consulted kutoa maamuzi ya whether vitumike ama la!.

  Acha bana wajaribu!
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wamepata kichaa hawajui wanaharibu vilivyotengenezwa na muumba wao na wao watapewa kichapo ohooo.....
   
 5. f

  fungamesa Senior Member

  #5
  Oct 7, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hawa Jamaa wameona Asubuhi ya saa 3 mwezi utakuwa kwetu kwa hiyo madhara yoyote yatakuwa Africa kama kutatokea mwezi kumwaga vifusi:confused:
   
 6. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  hizi ishu zingine siyo, kuripua bila kujua kitatokea nn! mbona ni mbinu mbovu sana, kwa nini wasingedrill kiustaarabu, gharama itakuwa kubwa sana lakini wataepusha kuharibu mazingira ya mwezi. vijukuu wao watawawajibisha!

  naipenda tanzania
   
Loading...