Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 169
- 287
Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni ametangaza mpango wa kutoza ushuru wa asilimia 100 kwa filamu zinazotengenezwa katika nchi za kigeni na kuoneshwa nchini Marekani. Hatua hii ni sehemu ya juhudi zake kuimarisha biashara ya ndani na kukabiliana na kile alichokiita “kufa kwa kasi” kwa sekta ya filamu ya Marekani.
Trump amesema nchi nyingine zinatoa motisha mbalimbali ili kuwahamasisha watengenezaji filamu na studio za Marekani kuondoka Marekani. Matamshi hayo yanaendana na wazo lake kwamba nchi nyingine zinaiba vitu vya Marekani, hivyo ni lazima achukue ushuru wa forodha kama silaha. Lakini ukweli ni upi? Katika miaka ya hivi karibuni, ili kuharakisha usambazaji wa utamaduni, nchi nyingi zinajitahidi kuvutia makampuni ya juu ya kimataifa ya filamu kuzisaidia kupiga filamu. Kwa makampuni hayo, hii sio tu inasaidia kuhakikisha ukweli wa utamaduni, lakini pia inaokoa gharama nyingi. Kwa mfano makampuni ya Hollywood, yakitengeneza filamu katika nchi zilizo na gharama ya chini ya wafanyikazi, yanaweza kuokoa asilimia 20-40 kwa gharama.
Sekta ya filamu ni moja ya alama za utamaduni wa Marekani. Lakini katika miaka ya karibuni, mvuto wa filamu za Marekani katika soko la dunia umepungua polepole. Hali hii inatokana na kupungua kwa sifa ya filamu hizo. Licha ya hayo, kuporomoka kwa heshima ya Marekani duniani pia kumeleta athari kubwa, ni jambo la kawaida kwamba filamu za Hollywood, kama wabebaji wa maadili ya Marekani, hazipendwi tena na watu. Lakini Trump amepuuza ukweli wa mambo, na ameamua kuchukua tena fimbo ya ushuru, ambayo haiwezekani kuwa njia ya kufufua filamu za Marekani.
Wakati Trump alipoamua kufunga mlango katika sekta ya filamu, habari zimekuja kwamba mauzo ya tiketi za filamu ya China Nezha 2 yamefikia Renminbi yuan bilioni 15.8, sawa na dola bilioni 2.2 katika soko la kimataifa. Filamu hiyo imeonyshwa katika nchi zaidi ya 50 duniani, na kuchukua nafasi ya 5 katika historia ya filamu duniani. Katika miaka ya hivi karibuni, filamu za China zimepata umaarufu kutokana na kufungua mlango na kushirikiana na nchi za nje.
Utengenezaji wa filamu Nezha 2 ulishirikisha makampuni mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Kampuni ya Industrial Light and Magic ya Marekani, Studio Ghibli ya Japani, na timu ya waandishi wa skrini ya Ufaransa. Zaidi ya hayo, filamu hiyo pia ilivutia uwekezaji wa mashirika mengi ya kimataifa, yakiwemo Sequoia Capital na Warner Bros.
Misimamo tofauti ya China na Marekani kuhusu maendeleo ya filamu inathibitisha kwamba ustawi haupatikani kutokana na vikwazo vya ushuru, bali unatokana na nia ya kufungua mlango na ushirikiano. Kwani, ni kwa kukumbatia nchi nyingine tu, ndipo unaweza kukumbatiwa na nchi nyingine.