Marekani Kupeleka Nyambizi Mbili Kukabiliana na Urusi

Marekani Kupeleka Nyambizi Mbili Kukabiliana na Urusi

Sun Zu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2022
Posts
758
Reaction score
2,106
Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba ameamuru nyambizi mbili za nyuklia za nchi hiyo zipelekwe kwenye maeneo mawili ya kimkakati kufuatia matamshi aliyoyataja kuwa ya "kijinga na uchochezi" yaliyotolewa na Rais wa zamani wa Urusi, Dmitry Medvedev. Hivi karibuni Medvedev alitishia uwezekano wa kutokea makabiliano ya kijeshi kati ya Urusi na Marekani baada ya Trump kuipa Urusi muda wa siku 10 hadi 12 pekee kusitisha vita nchini Ukraine au ikabiliwe na vikwazo. Trump hajasema ni wapi nyambizi hizo mbili zitapelekwa, lakini vyombo hivyo vya kivita vinavyozama chini ya bahari vina uwezo wa kufanya mashambulizi makubwa ya makombora ikiwemo yale ya nyuklia. Tupe mtizamo wako kuhusu taarifa hii.
 
Back
Top Bottom