Marekani kuondoa wanajeshi wake Syria

Marekani kuondoa wanajeshi wake Syria

Ila Trump hii sera yake ya America first Sasa inapoendea sio pazuri,unaondokaje Syria wakati una Urusi,una Iran una Hezbollah wamejizatiti na bado wanaendelea kujichimbia mizizi kule(Syria). INAHUZUNISHA!!!
Mkuu mbona USA yupo syria illegal? Russia yupo Miaka na miaka
 
sidhani Trump ni sawa na jiwe naamini anavyombo vya intelijensia vinamshauri hivyo nadhabi hili swala lilioangwa mda mrefu na sasa ndio wakati wa utekelezaji wake
 


Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatno kwamba wanajeshi wa Marekani wataanza kuondoshwa nchini Syria, kwavile wamefanikiwa kutimiza lengo lao la kulitokomeza kundi linalojiita Dola la Kiislam (IS) na sasa hawahitajiki tena nchini humo.
"Tumekuwa tukipambana kwa muda mrefu sana nchini Syria. Nimekuwa rais kwa zaidi ya miaka miwili. Tumejitahidi sana na tumelishinda kundi la IS. Tumewashinda na tumewashinda vibaya sana. Tumewapokonya ardhi waliokuwa wanidhibiti. Na sasa ni wakati wa wanajeshi wetu kurudi nyumbani," amesema Donald Trump wakati akitangaza uamuzi wake huo.
Uamuzi huo wa kuondoa kabisa wanajeshi wa Kimarekani nchini Syria, umethibitishwa pia na maafisa wa Marekani na unatarajiwa kutekelezwa katika miezi ijayo. Lakini kuondoka kwao huko kunaweza kukafanya vigumu kupambana na kundi hilo iwapo litapata tena nguvu.
Na Marekani pia itapoteza ushawishi wake katika eneo hilo, na kuhujumu juhudi zake za kidiplomasia za kutaka kumaliza vita vya Syria vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo vimeingia mwaka wake wa nane.
Maseneta wakosoa uamuzi wa Trump
Uamuzi huo wa Trump umekosolewa na Maseneta pamoja na baadhi ya wanachama wenzake wa chama cha Republican, ambao wanadai kwamba kuondoka kutazipa nguvu Urusi na Iran, ambazo zinamuunga mkono Rais wa Syria Bashar Assad. Maseneta hao wa Marekani ikiwa ni pamoja na wa chama cha Republican Jumatano usiku walimsisitizia Rais Donald Trump kutafakari upya uamuzi wake huo wa kuondoa majeshi ya Marekani kutoka Syria.

Wapiganaji wa kundi la SDF
Uamuzi huo pia unaweza kuliathiri kundi la muungano wa wanamgambo wa Kikurdi na Kiarabu unaojulikana kama SDF. Kundi hilo limekuwa mstari wa mbele katika kupambana na kundi la IS, lakini sasa linakabiliwa na kitisho kutoka Uturuki, kwa vile taifa hilo linatafakari kufanya mashambulizi nchini Syria.
Makamanda wa jeshi la Marekani waliopo Syria, ambao wamekuwa na uhusiano mzuri na viongozi wa kundi la SDF wameeleza wasiwasi wao juu ya uamuzi huo wa Trump na jinsi utakavyohatarisha vikosi vinavyoungwa mkono na Marekani.
Lakini Trump amesema kwake yeye operesheni ya Syria imemalizika, kwavile wanamgambo wa kundi la IS wameshapoteza maeneo waliokuwa wakiyadhibiti.
Maafisa wa Marekani wamesema wanajeshi wataanza kuondolewa Syria katika siku 60 hadi 100 zijazo na kwamba Wizara ya Mambo ya Nje itaanza kuondoa wafanyakazi wake kutoka Syria katika kipindi cha masaa 24.

Chanzo: DW
hii naona kama ni moto wa putin ndo unawatoa huko. Yaani kweli dunia inadanganywa. IS hiyo hiyo ndo inasapotiwa na USA, sasa eti wamewatoa. Na utaingiaje kwenye nchi ya mtu kupigana na watu ambao hawakuhusu? haya mapicha picha baadaye kitaeleweka tu.
 
Mmmh,US wanaondoka tu bila kuwa na Alternative plan?..Sidhani
 
sioni kama ni busara kuanza kuingiza haya masuala na uhasama.Wanajeshi wanafamilia zao marekani sasa kama IS hawapo warudi nyumbani tu.Halafu kitendo cha kuiingiza urusi pia ni upuuzi tu maana hakuna kitu kama hicho maana sion kwamba ni msingi upi unaotumia russia kumtisha US.Hayo ni maamuzi tu ya Trump basi.Na IS wakipewa nguvu basi majeshi yatarudi.
Naona us kuondoa majeshi saizi kunasababu zaidi ya moja kwa mtazamowangu.

1,Us wana kabiliwa na kitisho cha Russia ambao wana mpango wa kuweka mfumo wa ulinzi kwenye anga lote la syria.
Kwa hiyo us watashindwa kutumia ndege zao kufanya wanachotaka.

2,Ikiwa urusi wata wazuiya kuruka katika anga la syria manayake watatakiwa kuruka kwa nguvu nandio itakuwa kuingia vitani na urusi na kufanya syria uwanja wa mapambano.

3, Kama syria ikiwa uwanja wa mapambano kati ya Us na urusi then kuna haja ya kuangalia faida na hasara.

Cha kwanza us wangependa kuona wakiingia vitani na Russia wangetaka kuona Russia inapata direct effect nyumbani kwake.
Kwa hiyo kama ni kuingia kwenye vita na Russia nibora iwe kupitia Ukraine na sio syria.

Hasara kubwa ambayo wanaweza kuipata Us kwa kuingia vitani syria ni kuhatarisha maisha ya marafikizao/ Ndugu zao Israel.

Maana Irani na urusi wanaweza kuamua kuishambulia Israel kama sehemu ya mapigano ama kulipiza kisasi.

Kwahiyo naona Us wameamua kuchapa mwendo kistaarabu kabla hawaja lazimishwa ili kukwepa aibu.

Sababu nyingine nikuhofia kujiharibu kiuchumi kwakuwa wakiingia vitani china watawapiku kirahisisana.

Kwa hiyo ukiwauliza US wangependa kuzipiga na nani kati ya Urusi na china nadhani watapenda waanze kuzigonga na china ili kuvuruga uchumiwao.

Kwakuwa wanaweza kupigana nae wakiwa mbali na nyumbani sababu wana access ya kuwakaribia kupitia Japan, Korea kusini ama Taiwan na sehemu zingine.

Hataivyo wanaweza kuingia vitani na Urusi iwapo tu kutakuwa na ulazima mkubwa.
 
Tujali maisha ya ndugu zetu syria.Wamechoka na vita miaka 8.Ninyi mnaangalia matimu US,mara Urusi afu manasahau maisha ya raia wasio na hatia wa Syria.Mtu yeyote mwenye ubinadamu lazima asupport alichofanya Trumpa maana hata wakibaki bado Syria itaendelea kuwepo na choko zilizokuwepo hazipo.Mission complete.Warudi makwao.
Kwa mfano Baada ya M23 kumalizwq mbona wanajeshi wetu waliondolewa congo?saiz wamebaki wachache tu.
Tuwaache wasyria wajenge nchi yao.
 
Mattis anasepa
Sijajua kina Bolton na Haspel
 
SAFI SANA PUTIN KUISAMBARATISHA MAREKANI NA ULAYA [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapa nahisi kuna mchezo unachezwa.
Wasiojua Analysis ya haya mambo tayari wameshaanza kupuliza matarumbeta kushangilia. Kwenye haya mambo ni heri hawa jamaa wangeendelea kuwepo kuliko wakiondoka. Binafsi nahisi hivi sasa hali itakuwa mbaya zaidi. Syria huenda ikatawakiwa na mabwana wa kivita kama ilivyo Somalia. Muda wote wa zile harakati nahisi ndiyo Syria ilikua inamegwa kwa kuwaandaa hawa mabwana wa Kivita ili ikifika wakati muafaka wakabidhiwe vitendea kazi na kupewa maeneo ya kutawala.
Ngoja tuone yajayo.
 
Wasiojua Analysis ya haya mambo tayari wameshaanza kupuliza matarumbeta kushangilia. Kwenye haya mambo ni heri hawa jamaa wangeendelea kuwepo kuliko wakiondoka. Binafsi nahisi hivi sasa hali itakuwa mbaya zaidi. Syria huenda ikatawakiwa na mabwana wa kivita kama ilivyo Somalia. Muda wote wa zile harakati nahisi ndiyo Syria ilikua inamegwa kwa kuwaandaa hawa mabwana wa Kivita ili ikifika wakati muafaka wakabidhiwe vitendea kazi na ku9ewa maeneo ya kutawala.
Ngoja tuone yajayo.
Mkuu kwa nn unataka waendelee kuwepo?? Huoni kama watazidi kuuwa watu wasiokuwa na hatia ??
 
Erdogan akili zake anazijua mwenyewe ndo maana Putin anacheza nae kwa akili hakurupuki. Kuna kipindi unamkuta anasema Assad ni dikteta na atolewe madarakani Asubuhi akiamka anasema Assad abaki madarakani tena wanakaa meza Moja pamoja na Urusi na Iran kujadili.
Kiboko yake alikua ni Trump,erdogan alimpiga mikwara Trump,Trump akaamua kuongeza tarrifs kwenye Chuma na alumini toka Uturuki kwa zaidi ya 50%,fedha ya Uturuki ikaanza kuporomoka (hadi pale Qatar alipoamua kuja kuiokoa Uturuki) Erdogan akaamua akamwachia yule Pastor wa US alyekua akishikiliwa Uturuki ili yaishe.
Nakubaliana na wewe
Kiboko ya erdogan ni Trump kwa sababu wote hao ni watu wa kakurupuka[emoji23]
 
Back
Top Bottom