Marekani kuondoa wanajeshi wake Syria

Marekani kuondoa wanajeshi wake Syria

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatno kwamba wanajeshi wa Marekani wataanza kuondoshwa nchini Syria, kwavile wamefanikiwa kutimiza lengo lao la kulitokomeza kundi linalojiita Dola la Kiislam (IS) na sasa hawahitajiki tena nchini humo.
"Tumekuwa tukipambana kwa muda mrefu sana nchini Syria. Nimekuwa rais kwa zaidi ya miaka miwili. Tumejitahidi sana na tumelishinda kundi la IS. Tumewashinda na tumewashinda vibaya sana. Tumewapokonya ardhi waliokuwa wanidhibiti. Na sasa ni wakati wa wanajeshi wetu kurudi nyumbani," amesema Donald Trump wakati akitangaza uamuzi wake huo.
Uamuzi huo wa kuondoa kabisa wanajeshi wa Kimarekani nchini Syria, umethibitishwa pia na maafisa wa Marekani na unatarajiwa kutekelezwa katika miezi ijayo. Lakini kuondoka kwao huko kunaweza kukafanya vigumu kupambana na kundi hilo iwapo litapata tena nguvu.
Na Marekani pia itapoteza ushawishi wake katika eneo hilo, na kuhujumu juhudi zake za kidiplomasia za kutaka kumaliza vita vya Syria vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo vimeingia mwaka wake wa nane.
Maseneta wakosoa uamuzi wa Trump
Uamuzi huo wa Trump umekosolewa na Maseneta pamoja na baadhi ya wanachama wenzake wa chama cha Republican, ambao wanadai kwamba kuondoka kutazipa nguvu Urusi na Iran, ambazo zinamuunga mkono Rais wa Syria Bashar Assad. Maseneta hao wa Marekani ikiwa ni pamoja na wa chama cha Republican Jumatano usiku walimsisitizia Rais Donald Trump kutafakari upya uamuzi wake huo wa kuondoa majeshi ya Marekani kutoka Syria.

Wapiganaji wa kundi la SDF
Uamuzi huo pia unaweza kuliathiri kundi la muungano wa wanamgambo wa Kikurdi na Kiarabu unaojulikana kama SDF. Kundi hilo limekuwa mstari wa mbele katika kupambana na kundi la IS, lakini sasa linakabiliwa na kitisho kutoka Uturuki, kwa vile taifa hilo linatafakari kufanya mashambulizi nchini Syria.
Makamanda wa jeshi la Marekani waliopo Syria, ambao wamekuwa na uhusiano mzuri na viongozi wa kundi la SDF wameeleza wasiwasi wao juu ya uamuzi huo wa Trump na jinsi utakavyohatarisha vikosi vinavyoungwa mkono na Marekani.
Lakini Trump amesema kwake yeye operesheni ya Syria imemalizika, kwavile wanamgambo wa kundi la IS wameshapoteza maeneo waliokuwa wakiyadhibiti.
Maafisa wa Marekani wamesema wanajeshi wataanza kuondolewa Syria katika siku 60 hadi 100 zijazo na kwamba Wizara ya Mambo ya Nje itaanza kuondoa wafanyakazi wake kutoka Syria katika kipindi cha masaa 24.

Chanzo: DW
 
Naona us kuondoa majeshi saizi kunasababu zaidi ya moja kwa mtazamowangu.

1,Us wana kabiliwa na kitisho cha Russia ambao wana mpango wa kuweka mfumo wa ulinzi kwenye anga lote la syria.
Kwa hiyo us watashindwa kutumia ndege zao kufanya wanachotaka.

2,Ikiwa urusi wata wazuiya kuruka katika anga la syria manayake watatakiwa kuruka kwa nguvu nandio itakuwa kuingia vitani na urusi na kufanya syria uwanja wa mapambano.

3, Kama syria ikiwa uwanja wa mapambano kati ya Us na urusi then kuna haja ya kuangalia faida na hasara.

Cha kwanza us wangependa kuona wakiingia vitani na Russia wangetaka kuona Russia inapata direct effect nyumbani kwake.
Kwa hiyo kama ni kuingia kwenye vita na Russia nibora iwe kupitia Ukraine na sio syria.

Hasara kubwa ambayo wanaweza kuipata Us kwa kuingia vitani syria ni kuhatarisha maisha ya marafikizao/ Ndugu zao Israel.

Maana Irani na urusi wanaweza kuamua kuishambulia Israel kama sehemu ya mapigano ama kulipiza kisasi.

Kwahiyo naona Us wameamua kuchapa mwendo kistaarabu kabla hawaja lazimishwa ili kukwepa aibu.

Sababu nyingine nikuhofia kujiharibu kiuchumi kwakuwa wakiingia vitani china watawapiku kirahisisana.

Kwa hiyo ukiwauliza US wangependa kuzipiga na nani kati ya Urusi na china nadhani watapenda waanze kuzigonga na china ili kuvuruga uchumiwao.

Kwakuwa wanaweza kupigana nae wakiwa mbali na nyumbani sababu wana access ya kuwakaribia kupitia Japan, Korea kusini ama Taiwan na sehemu zingine.

Hataivyo wanaweza kuingia vitani na Urusi iwapo tu kutakuwa na ulazima mkubwa.
 
Mchezo ndo unaanza

Kajiondoa lkn huohuo Kaacha wapiganaji zaidi ya elfu arobain wenye mafunzo makali.

Kajiondoa, kulinda Uhusiano wake na Uturuki, kijeshi na kisiasa .

Kajiondoa, ili Kuharibu uhusiano wa kufoji ulokuwepo kati ya Urusi na uturuki.

Kajiondoa sababu. Urusi iliinyima israel ruksa ya kushambulia Iran syria... Kwa iyo ili urusi iwaondoe wairan na kuipa ruksa ya kuwapiga wairan,... Ilibidi waisrael wailazimishe marekan kujitoa Syria... Kupunguza vikwazo kwa warusi ( mfano huyu mmiliki wa kampuni la Aluminia ) kaondolewa vikwazo ...

Bado Urusi na Syria hawapaswi kupiga yowe kwa hii hatua
 
Naona us kuondoa majeshi saizi kunasababu zaidi ya moja kwa mtazamowangu.

1,Us wana kabiliwa na kitisho cha Russia ambao wana mpango wa kuweka mfumo wa ulinzi kwenye anga lote la syria.
Kwa hiyo us watashindwa kutumia ndege zao kufanya wanachotaka.

2,Ikiwa urusi wata wazuiya kuruka katika anga la syria manayake watatakiwa kuruka kwa nguvu nandio itakuwa kuingia vitani na urusi na kufanya syria uwanja wa mapambano.

3, Kama syria ikiwa uwanja wa mapambano kati ya Us na urusi then kuna haja ya kuangalia faida na hasara.

Cha kwanza us wangependa kuona wakiingia vitani na Russia wangetaka kuona Russia inapata direct effect nyumbani kwake.
Kwa hiyo kama ni kuingia kwenye vita na Russia nibora iwe kupitia Ukraine na sio syria.

Hasara kubwa ambayo wanaweza kuipata Us kwa kuingia vitani syria ni kuhatarisha maisha ya marafikizao/ Ndugu zao Israel.

Maana Irani na urusi wanaweza kuamua kuishambulia Israel kama sehemu ya mapigano ama kulipiza kisasi.

Kwahiyo naona Us wameamua kuchapa mwendo kistaarabu kabla hawaja lazimishwa ili kukwepa aibu.

Sababu nyingine nikuhofia kujiharibu kiuchumi kwakuwa wakiingia vitani china watawapiku kirahisisana.

Kwa hiyo ukiwauliza US wangependa kuzipiga na nani kati ya Urusi na china nadhani watapenda waanze kuzigonga na china ili kuvuruga uchumiwao.

Kwakuwa wanaweza kupigana nae wakiwa mbali na nyumbani sababu wana access ya kuwakaribia kupitia Japan, Korea kusini ama Taiwan na sehemu zingine.

Hataivyo wanaweza kuingia vitani na Urusi iwapo tu kutakuwa na ulazima mkubwa.
fact lkn pia wamewakwepa na waturuki coz uturuki wanaplan ya kuwafata wakurdi syria soon
 
Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu amekasirika sana kusikia US anaondoa Majeshi na operation zake Syria akisema huu ni Ushindi kwa Iran kwan Iran itajitawala sana na kuanzisha Hezbollah nyingine Syria tena mpakan na Israel...Hivyo Netanyahu kasema atavishambulia vikosi au majeshi yanayosimamiwa na Iran swali la kujiuliza kwann Israel isivishambulie hivi Sasa.....Viongozi wengi hasa waandamizi wa US wamekasirishwa na hatua ya Trump kuviondoa vikosi hivyo haraka bila ata kiwashirikisha lakin wajuzi wa Mambo wanasema wakati wa kampeni Trump alisisitiza kuviondoa vikosi hivyo km akishinda akisema US sio world policeman wa middle East na uchaguzi ni mwakani tu 2020 hivo anatimiza ahadi....Sababu nyingine ni Turkey kuendelea na misimamo yake isiyoyumba kwa wa Kurd ambao US amekua akishirikiana nao na Turkey wanawaona hao ni magaidi...Sababu ingine ni uimala wa Russia,Iran,Hezbollah,na majeshi ya Asad kuendelea kuyachukua maeneo mengi hivyo wangejikuta wanaanza mgogoro wa hao ambao wapo kiuhalali tofauti na US....Sababu nyingine ni Uchumi kwan nadhan wafadhili wa US alikua ni Qatar,UAE,Saudi Arabia kuendelea kutofautina hivyo kusitisha ufadhili...
 
Putin kakaba mpaka penalti [emoji38][emoji38]

Ushawishi wa Washington umedorora kwa kiwango cha lami huku ushawishi wa Moscow ukija juu kwa speed ya 4G

Marekani wakienda kuanzisha chokochoko zingine kama za Syria kupitia Ukraine, basi tutegemee Ukraine kuchukuliwa kibabe na Urusi

Kiuchumi China inamsumbua sana Marekani huku kijeshi Urusi ikiibuka kidedea,,, mbaya zaidi Marekani unajificha nyuma ya umoja wa Ulaya ikizikokota nchi zaidi 20 wakati mbabe wao Urusi anakuja yeye kama yeye

Yajayo yanafurahisha sana
 
fact lkn pia wamewakwepa na waturuki coz uturuki wanaplan ya kuwafata wakurdi syria soon
Ndio, na US hataki kuvurugana na uturuki bila sababu ya maana.
Kuna taarifa zinasema turkey wanakubaliana na US kuuziana silaha ikiwemo F-35 ili kuharibu mpango wa manunuzi ya S- 400 za urusi.

Na dili ya S- 400 kwenda turkey ikibuma basi tutaona kitukinginge kigumu kati ya urusi na Turkey.
 
sidhan kama erdogan ana jeuri kwa urusi
 
Back
Top Bottom