Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Balozi wa Marekani hapa nchini Alfonso Lenhardt amesema Serikali ya Marekani imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na kasi ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa yaliyofikiwa na Tanzania kiasi cha kuwa mfano wa kuigwa na serikali za nchini nyingine za Bara la Afrika na dunia kwa jumla.
Ameusifu mfumo wa demokrasia na utawala wa Serikali ya Tanzania, kwa kujali maslahi ya wananchi wake.
"Tanzania ina rasilimali muhimu kwa mfano ardhi yenye rutuba, hivyo kupitia ushirikiano wa kirafiki kati yetu, Marekani itahakikisha kuwa wananchi wote wanafaidika katika miradi ya maendeleo,".
Alisema msingi wa ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani ni wa kujivunia na kwamba ili uwe wa manufaa zaidi kwa wananchi, serikali zote mbili (kweli mbili au moja?)hazina budi kudumisha mshikamano kupitia uboreshaji wa huduma za maendeleo ya jamii.
Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, alisema katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufaika na rasilimali za taifa, Serikali ya CCM imejiwekea mikakati mbalimbali ya utekelezaji wa ilani ya Chama.
Alisema moja ya maeneo ambayo ilani hiyo imeyapa kipaumbele ni uboreshaji sekta za maendeleo ya jamii ikiwemo elimu. Kwa mujibu wa Chiligati, kwa sasa karibu kila kijiji hapa nchini, kina shule ya msingi na shule za sekondari katika kila kata.
My take
In reality tuseme ni maendeleo gani kiuchumi kijamii na kisiasa ambayo Marekani imeyaona hadi kusema nchi zingine zije kuiga kama huku si kutufanya wote mazezeta America is kidding us wanatuambia wakituchekea huku moyoni wakisema yaone haya majinga
Nafikiri tatizo data wanazopewa ni zile zilizotayarishwa na watu wa type ya kina Chiligati mfano anaposema kila kijiji kina shule wamarekani si wajinga wanajua kila kitu wanajua ubora wa shule zinazosemwa na type ya viongozi tulionao kwamba wakitaka chochote wanajichukulia ndiyo maana nasema tunafanywa mazezeta.