JANGA KUU LINALOINYEMELEA DUNIA KISIRISIRI.
Kwa muda mrefu sasa idadi ya wanaume inazidi kukinzana mbali na ile ya wanawake.Wanawake ni wengi kupindukia ukilinganisha na wanaume.
Watoto wanaozaliwa mahospitalini wameonesha tofauti kubwa kati ya wakike na wa kiume. Wa kiume wachache mara dufu ya wakike.
Tafiti zinaonesha kuwa mimba nyingi zinazoharibika ni za watoto wa kiume zaidi ya zile za wa Kike. Aidga vifo vingi vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano ni vya watoto wa kiume.
Katika nchi zenye ugomvi,mapigano na vita kubwa kubwa wanaokufa au kupata vilema vya kudumu wengi ni wanaume.
Wanaume wengi wenye umri wa utu uzima hufa wakiacha wanawake wakiendelea kuishi. Takwimu zinaonesha kuwa wajane ni wengi kushinda wagane!
Sayansi imetueleza jinsi ilivyorahisi kutungwa mimba ya mtoto wa Kike na ilivyo ngumu kwa upande wa watoto wa kiume.
WANAUME NI VIUMBE WALIOHATARINI KUTOWEKA DUNIANI.
Ongezeko hili litasababisha ongezeko la migogoro ya ndoa kotekote duniani.Hata msimamo wa makanisa wa Mke mmoja Mme mmoja utaingia kwenye mgogolo mkubwa na wawazi.
Wanawake sasa wanakuwa ndio wenye kuiendesha dunia. Ongezeko hili la wanawake ndiyo mwanzo wa mwisho wa ubabe wa wanaume kwao.
Tamaduni nyingi huenda zikageuzwa kabisa. Mfano katika jamii zetu ambalo watoto wanabeba Jina la baba na si la mama,sasa mambo yatageuka. Kama hatutagawana watoto basi huenda wote wakabeba Jina la mama.Duuuu,kweli Mungu wa ajabu!!!