Marekani imeshindwa uvumilivu North Korea

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,841
Rais wa Marekani Donald Trump anasema muda wa uvumilivu wa kimikakati kwa Korea Kaskazini umekamilika sasa.
Katika hotuba ya pamoja na rais wa Korea Kusini Moon Jae, kwenye ikulu ya White house, Trump amesema kwamba vitisho vya Korea Kaskazini vinafaa kupata majibu ya kijasiri.
Hata hivyo, Trump amesema ni muhimu kuwe na ushirikiano katika kugawana mzigo wa kuhakikisha usalama.
Rais wa Korea Kusini amesema kwamba taifa lake litaweka marekebisho ya kiuslama na kujenga msingi dhabiti wa kujikinga.
Rais Moon pia amesema ni muhimu kuendelea na majadiliano na viongozi wa Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini yamtaja Trump kwa mara ya kwanza
Kiongozi huyo wa Marekani amesema kuwa serikali yake sasa inafanya kazi na Korea Kusini pamoja na Japan wakiwemo washirika wengine duniani kuchukua hatua kadhaa za kidiplomasia, usalama na kiuchumi ili kuwalinda washirika wake pamoja na raia wa Marekani dhidi ya janga hilo kwa jina Korea Kaskazini.
 
Bado sidhani kabisa na siamini kama kutakuwepo na operesheni wa kijeshi dhidi ya North Korea kutoka Marekani.

Labda North Korea ifanye jambo lililo drastic sana.

Lakini si kwa huu upuuzi wa kurusha vikombora vyao baharini ambavyo wakati mwingine vinawafyatukia hapo hapo wao wenyewe.
 
Maneno tu hayo! Trump hana ubavu wa kuyaogelea maji marefu ya mzee wa kiduku kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake!
Kwanza katiba ya nchi yake inamfunga! Kwa mujibu wa katiba ya marekani ni marufuku kupiganisha vita katika ardhi ya marekani! Hivyo hawezi kuanzisha vita na taifa lenye uwezo wa kurusha kombora hadi marekani!
 
Back
Top Bottom