Marehemu Dkt. Mengi alikuwa na mdogo wake hospitalini kabla ya mauti kumfika - Kikwete

Jakaya kwa kujifanya anayajua ya familia HAJAMBO, kwenye msiba wa Ruge alituambia marehemu kaacha watoto wawili, kuja kusomwa historia watoto ni watano.. Mkwere bana hata akiwa na madaraka na elimu porojo haziachi...mdogo wake alienda na Regina wakati hali imeshakuwa mbaya sasa kuwepo kwake huko Kikwete anataka kutuambia nini labda?


Yupo close na hiyo familia way back , na Misiba yote kuanzia Mutie, mama Mercy na Mzee Mengi yote KJ alikua nao kuwapa faraja
 
Jakaya kwa kujifanya anayajua ya familia HAJAMBO, kwenye msiba wa Ruge alituambia marehemu kaacha watoto wawili, kuja kusomwa historia watoto ni watano.. Mkwere bana hata akiwa na madaraka na elimu porojo haziachi...mdogo wake alienda na Regina wakati hali imeshakuwa mbaya sasa kuwepo kwake huko Kikwete anataka kutuambia nini labda?
Kwa maelezo ya JK ni kama Mjane wa Marehemu hakuwepo hospital.
 
Nimemsikia Raisi Mstaafu Dkt Kikwete katika taarifa ya habari ITV akisema kuwa Marehemu Dkt Mengi alikuwa na mdogo wake (Mengi) hospitalini pamoja na wanafamilia wengine kabla ya kifo chake.
Hivyo akawataka watu wajihadhari na taarifa zinazozushwa kuhusu sababu za kifo hicho.

Nadhani kwa kauli hii ni vema kujizuia kuzungumzia au kuandika chochote kuhusu rumors za kifo hiki kusubiri taarifa ya wanafamilia kwa kuwa wao wana taarifa kamili.

Kufanya vinginevyo kunaweza kuwaumiza sana wana familia hasa kama kinachosemwa ni uongo.
Wana familia wanahiari ya kueleza sababu za kifo au kutoeleza !
 
Comment za huu uzi zinaonyesha ni jinsi gani watanzania walivyo na uwezo mdogo wa kufikiri a.k.a akili ndogo
 
Jakaya kwa kujifanya anayajua ya familia HAJAMBO, kwenye msiba wa Ruge alituambia marehemu kaacha watoto wawili, kuja kusomwa historia watoto ni watano.. Mkwere bana hata akiwa na madaraka na elimu porojo haziachi...mdogo wake alienda na Regina wakati hali imeshakuwa mbaya sasa kuwepo kwake huko Kikwete anataka kutuambia nini labda?
Vyovyote vile, mlalamikaji atabaki kuwa mwanafamilia au wanafamilia siyo Mange. Kwa mantiki hii Kikwete yuko sahihi 100%. Nami ninaamini hakuna mwanafamilia anayelalamika au atakayelalamika na msiba utaisha vizuri kama ilivyo misiba mingine.
 
Kikwete ni rais wa wapi? Ukweli ni ukweli tu, haujalishi umesemwa na nani. Kama Kikwete alishindwa kumjua aliyemteka Ulimboka tena akiwa rais, atajua kuhusu ya Mengi tena akiwa mstaafu?
Una hakika hakujua? Au kukaa kimya ndio kutokujua?
 
Kwa hiyo wewe na akili yako unamwamini huyu mpuuzi Mange kuliko JK Kikwete? watu sijui mumelishwa kasumba gani na huyo mwehu wenu

Who is JK? Kama hakujua pesa za escrow Ni za umma au sio za umma akiwa rais ndio atajua habari za Mengi?
 
umechukuli serious sana statement ya JK mpaka unachanganyikiwa

sio kweli JK hajui nini kinatokea, nini kimetokea na sio kuwa hajui mambo!.....

Kaongea kama mzee, kumlinda marehemu na familia yake

mtafute Rachel Temu, ndio ana uhakika

yaani unakuja na kurasa 100 eti JK hajui!!!!......

wewe na akili zako zote source yako ni Mange tu???....na unatamba kabisa hapa bila aibu kuwa unamwamini asilimia 100

Mkuu kwenye hilo suala la Mengi, Kikwete na Mange wote ni wapiga porojo tu. Simply sio wahusika, hivyo kila mtu anaweza kumuamini yoyote. Huyo Kikwete alipokuwa rais alikuwa anaongea uongo wa wazi, leo hii ni mstaafu nani ana muda wa kumuamini?
 
South Afrika ni Dubai?!..... Mzee Mengi amefia south Afrika!
usichezeee police ya dubai . ni wazuri sana na wako fasta kwa uchunguzi ya mauwaji na kesi za aina yoyote waulize shirika la ujasusi la israel mosad walipoenda watu 23 kumuua comander wa palestine alipokwenda dubai kufanya shopping hoteli aliyofikia mpalestina na wao walichukua vyumba hapo hapo na waliweza kumuuwa lakini kwa mda mchache waligundulika wauwaji na majina yao na sehemu wanapoishi na passport zao walizotumia za nchi tofauti
 
Bado watanzania tunasafari ndefu sana. Watu wanasema Mange habari zake nyingi zina ukweli zaidi ya 90%! Hawaoni kama wao ndio wanalazimisha zionekane za kweli.

Ni habari ngapi zilishatoka kwake baadae zikathibitishwa kuwa za kweli kwa kubalance pande zote?

Kwanini tunakimbilia kuamini uzushi uzushi badala ya kujishughulisha na mambo ya muhimu?

Let us assume anayoyasema kuhusu mzee wetu ni ya kweli, mimi na wewe yanatuhusu nini? Tuna nafasi gani ku force familia ifuate hisia zetu?

Mwisho wa yote watu wanasema kwamba familia ilifichwa kuhusu mzee kuumwa! Kwa hiyo wanaamini yule mzee hatembei na daktari hasa kwa hali tuliyomuonayo wakati wa msiba wa Ruge na Kibonde!

Mzee alikuwa anasaidiwa kukaa na kusimama kwa kushikiliwa na watu zaidi ya wawili halafu atembee bila usaidizi wa daktari?

Achilia mbali daktari, kwa hiyo yule mzee hana wasaidizi wengine?! Kama mkewe alificha taarifa kwa ndugu baada ya kuzidiwa, daktari na wasaidizi wake nao walificha? Kwamba Mkewe aliwatisha wasiseme au!? Na wao wakatishika ama!?

Watanzania tuachane na haya mambo ya kubebeshwa vitu na kuvibeba kama vilivyo! Tutumie akili tulizopewa na Mungu vizuri! Si kila jambo tunatakiwa kuamini kwa asilimia zote!

Walioko karibu na familia ya mzee wanakili kuwa tangu 2016 afya ya mzee haikuwa vizuri, sasa kwanini leo kifo chake kionekane kuwa ghafla? Sisi tulio nje ndo tunaona ghafla kwasababu sio lazima tujue yote yanayohusu familia husika. Kwenye msiba wa Ruge mzee alionekan dhahiri afya yake sio nzuri sana.

Na mwisho kabisa, hakuna nafsi ambayo haitaonja mauti! Mzee amejaaliwa kuishi miaka 77, si haba ni jambo la kumshukuru Mungu kwa maisha yake na namna alivyojitoa kwa wengine.

Kupitia yeye tujifunze, leo ukiondoka utaacha alama gani!?

Utakumbukwa kwa kuwa mueneza uzushi wa kwanza au mbeba kila uzushi unaoletwa? Na jamii yako inafaidika na nini na alama hiyo unayoiacha?
 
Sisi watanzania ni mazuzu sana, sasa unafikiri kama atakuwa ameuawa technically(kitaalam) kuna mwanafamilia atajua chanzo cha kifo eti kisa alikuwa na marehemu hospitalini??!
Wamefanya postmortam huko Dubai...amesema mwanasheria wa familia..tena full body
 
Back
Top Bottom