Sijui kuhusu wanawake, hilo watajibu wenyewe
Ila kikawaida marasta huwa concious na aware sana kuhusu maisha yao binafsi, ya jamii na dunia nzima. Wapo makini sana na vitu wanavyoulisha ubongo wao hivyo, si ajabu huyo unaemuona mchafu, ukiingia kwenye mazungumzo nae, unaweza usimuingie hata robo kwa vitu alivyojaza upstairs
Kingine ni watu peaceful sana na wanaoishi maisha halisi "culture". Hawafuati trend za dunia, wanafuata ukweli halisi na vitu vinavyowapa furaha. Sio makondoo wa media au propaganda za siasa, wao huwa na misimamo yao binafsi.. Sio wanafki, sio fakers.. 100%OG according kwa dunia yao ndio maana anaweza kuwa na muonekano wa bhangi na knowledge ya CEO comfortably.
Kwa hiyo kwa watu wenye exposure na njaa ya knowledge kuliko udaku kama wazungu, Marasta ni rahisi kuvutiwa ama kushawishika nao