Marando na watuhumiwa wa ufisadi

Viongozi wetu wanaogopa kuchangia hii sredi kuogopa kuonesha msimamo wao! Basi walau wahaidi "kuyafanyia kazi" maoni yetu yaishe!

Pamoja na kukatwa kodi zetu kiaina,mawakili wa serikali wanalipwa mishahara yao na kutetea wauwaji ambao kwa mazingira ya nje ya mahakama huonekana wanamakosa.

Sawa mpaka hapo tunakubaliana.

Vizuri

Hao mawakili wasiofungamana na chama chama chochote ni akina nani na wanapatikana wapi hapa Tanzania.

Chris Maina Peter ni mmoja wapo. Huyu sijawahi kumuona kwenye jukwaa lolote la kisiasa. Kuna jirani yangu wa zamani Darajani - Kapwete John..kaolewa siku hizi na sijui jina la mumewe. Kuna Agnes Sayi...huyu naye kaolewa sijui jina la mumewe. Wapo wa kutosha tu.

Sijui una maana gani na neno makada, lakini nimepitia listi ya viongozi wa Chadema na sijaliona jina la Marando.

Una kamusi hapo? Kama unayo angalia maana yake.

Sawa sawa hakuna miiko yoyote ya kitaaluma (ethics) aliyovunja Marando. Sana sana kaweka ushabiki pembeni kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na hapa Marando yafaa apewe sifa.

Hakuna aliyewakataza kumpa sifa. Na sisi tunaomuona yeye ni mnafiki tuna haki hiyo.

Swali ni je, ungependa kuona vibaka wakichomwa moto ?

Hapana.

Court of public opinion na implications zake kisiasa unaijua wewe?

NN ukishupalia kitu! Mbona ufisadi wa magamba mishipa haikutoki? Hivi bandugu FF = NN au? Hahahahaha!

Wewe ni chadema tawi gani na kadi namba ngapi Mkuu? Ilinikusaidie husiyo ya fahamu!

Unaposema achague mteja kwa kuangalia aina ya kosa analoshtakiwa nalo sijui unajenga hoja yako juu ya nini? unataka kusema kuna makosa ya jinai ambayo CDM inayaunga mkono na yapo mbayo CDM haiyaungi mkono!

Kama ikiwa CDM haiungi mkono makosa yote ya jinai kwanini husiseme kuwa wanachama wa CDM wasimtete mtu yeyote anayeshtakiwa na serikali mahakamani? kama ikiwa vyama vya siasa vitafanya ujinga huo vyote nani atamtetea nani? and then! nini kitafuata au CDM ikichuwa madaraka itapereka mswada wa sheria kuomba mawakili wote wasiruhusiwe kuwa wanachama wa vyama vya siasa? Hii hoja ya ajabu sana.

Kwanini husiseme kuwa watuhumiwa waiperekwe Mahakamani wafungwe moja kwa moja na polisi? Maana Wakili ni sehemu ya Mahakama na kazi ya Wakili si kusaidia mtuhumiwa hasifungwe bali ni kuisaidia mahakama itende haki na itoe hukumu kwa mujibu wa sheria za nchni bila upendeleo wowote.

Haki ya watanzania wanaoshtakiwa ni haki ya kikatiba chama chochote ambacho kinafikia kupingana na haki hizo hakifai mbele ya Jamii kwa ujumla wake maana huwezi kuubiri haki na wakati mwingine ukaipinga, unachotaka wewe kifanyike ndio kinyume na mataraji ya wengi, maana kuitaka CDM ipingane na haki za msingi za watanzania walizopewa kwa mujibu wa sheria.

Hoja yako bado ndugu yangu,

Hakuna aliyesema wanachama wa CHADEMA ambao ni mawakili wasitetee watuhumiwa wenye kesi za jinai...Hakuna mtu anayeleta hoja hiyo. Labda wewe ndiye unaianzisha.

Tatizo ni mwanachama wa CHADEMA, kada na kiongozi wa juu (Mabere Marando), ambaye amekuwa mstari wa mbeke kupinga ufisadi kiasi cha kuwataja mafisadi hadharani (naamini unakukumbuka kasheshe ya Jangwani mwaka jana) na halafu huyo asimame mahakamani kuwatetea wateja wanaokabiliwa na kesi za ufisadi. Hii haikubaliki kabisa hata kama hajavunja sheria yoyote au maadili ya kazi yake ya uwakili.

Wananchi wanajua kuwa mafisadi ni sawa na mumiani (blood suckers) na hawawezi kumwelewa mtu anayewatetea hata kama nyie wasomi mnamulewa.

Ila kama hamtaki kuwasikiliza wananchi wa kawaida basi msubiri siku ya siku watawaeleza kwa sauti ambayo mtaielewa hata kama hamtaipenda!!

Nimefuatilia mjadala na naona kuna mchanganyiko wa mambo ambayo yaweza kuwa hatuyaelewi au tunayatafsiri vibaya.
Kwanza nakubaliana na Kobello kuwa kazi ya wakili(stand to be corrected) ni kusimamia haki ili itendeke (Fair trial) hata kama mtuhumiwa amethibitika kutenda kosa ili mambo mengine ya kisheria yazingatiwe katika kutoa adhabu.

Mawakili ni weledi sana wa sheria na kama taaluma zingine wanongozwa na sheria, principles na ethics. Moja kati ya Ethics zao ni kulinda public interest iwe katika kikundi au mtu binafsi kwa kuhakikisha haki inatendeka kwa kila raia anayestahili bila kujali itikadi ya kisiasa ya wakili au mtuhumiwa kama wanavyofanya madaktari hospitali.

Profesa Sarungi mtaalamu wa upasuaji alikuwa mkuu wa mkoa wa Pwani, Mbunge mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM na kada muhimu. Kuna nyakati alilazimika kutumia taaluma yake katika hospitali ya tumbi pale kulipotokea matukio kama ya ajali, au kuhudumia majeruhi wanaotokana na uhalifu kama ujambazi, wizi, fumanizi n.k.

Sarungi hakufanya kazi kama kada wa chama bali mtaalamu anayelinda kiapo chake cha udaktari cha kuhudumia binadamu bila kuangalia jambo lolote bali uninadamu na utabibu kwa kutenda haki.
Court of public opinion ilimhukumu kama mtu, daktari na kiongozi anayejali na kuenzi taaluma yake kwa kuthamini utu.

Popote duniani mtuhumiwa bila kujali wajihi, hadhi au nafasi yake katika jamii analindwa na haki ya kisheria. Wauaji wa Albino ambao wengine hawamudu hata kununua mkate, bado wanahaki ya kuwekewa uwakili na cha kushangaza zaidi ni kuwa mawakili wao wanalipwa na serikali ambayo ni kodi yangu mimi na wewe. Kwa maneno mengine, tunalaani mauaji ya albino na wakati huo huo tunatoa pesa za kuwawekea mawakili.
Court of public opinion inapaswa kutusuta sisi tunaolipia gharama za kumuokoa muuaji au kabla ya kumlaumu wakili.

Tunapoiba pesa za halmashauri au wizara na kisha kuwaambia mawakili siri zetu na wao kututetea hata kama wanajua tumeiba au tumefanya ujambazi, court of public opinion inatupa haki kama ambavyo inapaswa kutoa haki kwa mtuhumiwa mwingine wa fumanizi au ufisadi.

Ni jambo gumu kuwa na mtu asiyefungamana na itikadi ya kisiasa hasa katika kada ya wasomi.
Wapo watakaosema hawafungamani kama ninavyoweza kusema lakini ukweli unabaki mioyoni mwao na wala hatupaswi kusadiki kauli zao.

Mfano, sheria inakataza viongozi wa majeshi kuwa washabiki wa vyama vya siasa. Mwaka jana tumeona kamanda mkubwa wa polisi aliyestaafu miezi 3 tu nakuchukua form za ubunge. Hivi huyu tunaweza kusadiki kuwa alikielewa chama chake katika miezi 3 tu hadi kufikia hatua ya kuchukua form za ubunge kama si kuwa alikuwa kada asiyesema? Sasa tutasemaje tuwe na mawakili neutral, kwa evidence gani.

Marando anapokuwa mahakamani anasimamia haki kama wakili na mtaalamu kwa mtuhumiwa na sio mhalifu na si kama ni mwakilishi wa Chama cha kisiasa kwa mantiki ile ile ambayo Profesa Sarungi anakuwa theatre akimshona nyuzi jambazi.

Profesa kwa wakati ule si mkuu wa mkoa au kada wa chama bali daktari aliyekula kiapo kutoa huduma ya haki kwa binadamu.
Ikifika hapo lazima tujiulize kwanini kuna double standard?
Why court of public opinion is not applicable across the board!

Kisiasa ni kweli hili jambo lina political ramifications hasa kwa nchi zenye wananchi ambao ufahamu wao una limit. Kibaya zaidi ni kuwa hata sisi tunaopaswa kuwaambia kuwa kuna politics na professionalism tunaelekea kuwashadidia waelewe tofauti.Je huku si kuendelea kuwapotosha!!
Tatizo lingine ni sisi kuchomeka siasa kwenye kila jambo hata yale ya kitaaluma na kitaalamu ndiyo maana hata mambo ya megawatts, resuscitation, economy, tumewaachia wao wapange na wasaini mikataba. Sio engineers, doctors au economists.

Tumeruhusu na kukubali wanasiasa kuchomeka siasa katika taaluma na sasa tuneshaingia huko haya ndiyo matokeo yake.

Tunadhima ya kuuambia umma wetu uliochanganywa na siasa za Nape Nnauye kuwa kuwa, alichosema Nape ni political mudsling and confusion, ukweli ni kuwa Marando kama professional hajakiuka Laws, regulations, principles au ethics kwa namna yoyote na kwamba court of public opionion imhukumu kwa kauli na matendo yake kisiasa katika chama chake bila kuchanganya na utaalamu wake kama vile court of public opinion ilivyomuelewa profesa Sarungi alipokuwa ana repea mifupa na kuzuia damu isivuje kwa majambazi.

Ni maoni yangu senti sumuni.

yah, umejibu sahihi kabisa

nimependa avatar yako

wewe jamaa .... hivi ukiwa kama daktari halafu mwizi akaletwa hospitalini ameumizwa vibaya je hautamtibu kwasababu ni mwizi ?
tofautisha kati ya daktari na mwanasheria; unapozungumzia daktari unazungumzia uhai wa mtu, lakini c dhani kama unapomtetea fisadi unaokoa uhai wake! kwamba usipomtetea atakufa! kilichompeleka huko marando ni njaa, sasa ili kuinusuru chadema inabidi achagua kati ya siasa au kuwatetea mafisadi! kinyume cha hapo chadema inabidi ifyate mkia kuzungumzia mafisadi, maana huwezi kukipinga kitu ambacho mwenyewe unakitetea huo utakuwa ni unafiki! yaani itakuwa ni sawa na kusema nyama ya kiti ni haramu lakini mchuzi wake unakunywa!!!!!!!!!!!

na mimi naomba nikuulize kaswali kadogo; hivi mh. marando anapokwenda kuwatetea hawa mafisadi anapoulizwa na hakimu kuwa watuhumiwa wake ni wezi, wameiba pesa za epa kwa mfano; huwa anajibu nn? ndio au hapana? yaani kwa niaba ya watuhumiwa marando huwa anakubali au huzikana tuhuma?

Ndiyo maana Marando alijigamba pale Jangwani kuwa anawajua mafisadi. Anawajua kwa sababu anawatetea!!

Chukulia wewe in lawyer mzuri sana, na kuna kibaka mmoja amembaka binti yako na kafikishwa mahakamani. Sasa anataka kukukodi umtetee. Je utamtetea?

Hapa napata shida kidogo kuelewa, Dr Slaa, anapambana kupiga vita ufisadi halafu ndani ya chama chake anatokea mtu anawatetea Mafisadi kisa eti Uwakili ni taaluma hana haki ya kuwatetea!
Kama kweli ana dhamira ya dhati angejitoa kwenye siasa aendelee na kazi yake ya kutetea Mafisadi kama kuna watu watahoji chochote

Chukulia wewe in lawyer mzuri sana, na kuna kibaka mmoja amembaka binti yako na kafikishwa mahakamani. Sasa anataka kukukodi umtetee. Je utamtetea?

Sawa kabisa mkuu,

Hata mimi niliwauliza hao watu wa sheria na maadili ya uwakili swali kama hilo.....Unaweza kumtetea mtu ambaye ana tuhuma za kumuua baba yako?????

Chukulia wewe in lawyer mzuri sana, na kuna kibaka mmoja amembaka binti yako na kafikishwa mahakamani. Sasa anataka kukukodi umtetee. Je utamtetea?

kamwe mshitaki hawezi kuwa mshitakiwa naturally (plaintiff as defendant ), hiyo haitakuwa kesi

kamwe mshitaki hawezi kuwa mshitakiwa naturally (plaintiff as defendant ), hiyo haitakuwa kesi

Mshitaki ni Jamhuri na sio wewe. Binti yako anaweza kuwa kabakwa chuoni.

hoja yako ni nzuri sana na ina tahadhali na mtazamo mkubwa sana wa mbele! ninachokiona hapa kuna wana chadema wamekua wavivu wa kufikiria sana! hawaoni hatari ya kuichafua chadema jukwani kupitia hili analolifanya marando! ni bahati mbaya sana wanachadema wameiweka akili yao kw aupande wa kishabiki kwa kila jambo! hili la marando linatia doa kwa chadema katika vita yake ya kupinga ufisadi! ni doa!

Sawa kabisa mkuu,

Hata mimi niliwauliza hao watu wa sheria na maadili ya uwakili swali kama hilo.....Unaweza kumtetea mtu ambaye ana tuhuma za kumuua baba yako?????
ni simple logic too! unahubiri la kupinga ufisadi kesho unaenda kisutu kuwatetea mafisadi!

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…