Marando na watuhumiwa wa ufisadi

Ni kweli, pia aelewe kuwa wale ni watuhumiwa si haki kuwabagua kwa utuhumiwa wao
hadi pale haki itakapojibainisha.
Marando na Dr Slaa wote ni CDM na kila siku wanasimama kwenye majukwaa ya siasa wanapinga Ufisadi.
Tukija kwenye suala la EPA Dr Slaa, anawatambua Mafisadi kina Jeetu Pater, Marando hawatambui?
Hii kweli sinema ya kihindi
 
Ni threat kwa CCM na mafisadi sio kwa wananchi hata kiongozi wa waasi Libya Mustafa Abdel Jalil alikuwa waziri wa sheria wakati wa Gaddafi.
 
Tutafute namna ya kumtetea Marando jamani,hv kusema wale ni watuhumiwa tu maana yake Marando anapigania kumprove wrong Dr slaa? Tuseme vidagaa or whatever lakini fisadi ni fisadi na hao tunawajua hivyo!
 
Mimi nilishagasema humu kuwa kisiasa afanyacho Marando hakitaeleweka hata kama hakuna makosa kwenye maadili ya fani yake. Ni heri achague moja tu...siasa ama aendelee na fani yake bila kujiingiza kwenye siasa.
 

Ni kweli hili suala la Marando linatakiwa kuangaliwa kwa undani zaidi na viongozi wa chama. Kwa upande mwingine linaathiri chama kusonga mbele. Wanaoijua issue ya Mahalu kwa kweli hawaamini mtu kama Marando kumtetea.Tunamwomba kabla ya kuchukua kesi aichunguze kwanza tunataka awe anawaadabisha hao mafisadi ili tabia hiyo ikome. Tanzania imeshatafunwa vya kutosha na ndio maana vijana tunateseka, hatuna ajira.
 
Zamani tulikuwa na majibu ktk kila swali na viongozi wetu walikuwa wanajibu kila hoja kwa ufasaha.tusirundike malalamiko akina Tumbo ndio kazi zao hizi!
 
Hivi Tundu Lissu akianza kuwatetea akina Rostam na mafisadi wenzie ataeleweka kweli?
 
Ni kweli lakini maadili ya uwakili yanasemaje? Tusipende kuhukumu pasipo kujua tunachokihukumu.

Mimi sijui hayo maadili ya uwakili kwa sababu mimi siyo wakali. Pia hakuna mtu anayelazimika kujua maadili ya kazi yangu. Hata hivyo kutojua maadili ya kazi mtu hakutunyimi haki ya kuona mambo katika mtazamo wa kawaida (hata kama mtazomo wetu unatokana na ujinga wetu). Na ni kutokana na mtazamo wetu, wengi wetu tunaamini kuwa Marando hana sababu ambayo anaweza kuitoa akatushawishi kwamba anaweza kuendelea kuwatetea mafisadi na wakati huo huo akaendelea kutuhubiria kuwa ufisadi ni mbaya...Wakati huo anakula na kusaza kwa sababu ya malipo ya uwakili wa kuwatetea mafidi ...It doesn't make sense at all!

Labda nikuulize...Unaweza kusimama kama wakili ukamtetea mteja anayetuhumiwa kumuua baba yako???
 
Unataka CDM wajifunze toka kwa wengine wepi CCM? au kutoka kwako ha ha ha teacher.
 
si kosa kutetea maana ya uwakili ni kutetetea au kurekebisha kwenye makosa, ndio maana kuna kushinda kesi na kushindwa , Marando aliwahi kusema kuwa kesi hizi za ufisadi zimeisaidia CDM kujua kwa mapana zaidi wizi wa maliza walalahoi(Watz) kwa hiyo naona tumuache na taruma yake tutajua mengi, wezi wengi wanatumwa na mafisadi papa wakigundulika wanawaachia msara fisadi dagaa, tusubiri la kagoda kama CCM haikuhusika!!!
 

Hapana mkuu,

Kwani Slaa kapata wapi taarifa? Kama ni kujua taarifa haina haja ya kuwatetea mafisadi. Ana njia nyingi sana za kupata taarifa ukingatia kuwa yeye (Marando) ni shushu mwenye uzoefu wa kutosha!!
 

Nakubaliana na wewe kabisa, ninachotaka kusema ni kwamba kila mtu ana mtazamo wake
katika jambo hili na sidhani kama ni dhambi kutofautiana maana mwisho wa siku ukweli
utadhihirika. Hapa hatuhukumu bali tunajaribu kuangalia possibilities zote kuhusiana na
kile ulichokiita uelewa mdogo wa wananchi...
 

Naweza endapo nadhani kuna jambo limefichika nyuma ya pazia kama vile mtuhumiwa kubambikiwa
mashtaka ambayo hakuhusika, nitafanya hivyo ili kuujua ukweli zaidi. Mbona imeshatokea hivyo Marekani
kwa wakili kumtetea mtuhumiwa aliyetuhumiwa kumuua mtoto wake, mwisho wa siku ukweli ukajulikana
kuwa hakuhusika bali alitolewa kafara na vigogo ili kulinda maslahi yao... tusiangalie jambo hili kwa upande mmoja tu
 
Marando kigeugeu na miongoni mwa mafisadi makubwa. Anang'ata na kupuliza, atachukiaje ufisadi halafu unatetea ufisadi wakati chama chake ambaye ni miongoni mwa vigogo wanajidai mapambano yao ni dhidi ya ufisadi? walewale wanakataa posho bungeni baada ya kulamba za miaka sita na kupewa mrabaha Barrick.
 
MARANDOO hakupaswa kuingilia hata kidogo kesi ya MAFISADI. jeetu ni fisadi mdogo?? MANJI je ni fisadi mdogo? Uwepo wa MANJI YANGA umepelekea yanga nao waitwe mafisadi(BISHA) Wapo wa TZ wengi mamilioni wenye kubambikiwa kesi akawasaidie hao kama alivyofanya LISSU ktk kesi ya kule SERENGETI NYAMUMWA. tena bule tutamchangia hela. Wale wazee wastaafu wa iliyokuwa jumuia ya Afrika mashariki wamekosa mtetezi mwenye nguvu MARANDO HUKUWAONA HAO BABU ZETU Tusijibu maswali magumu kwa majibu mepesi. LAKINI NANUKUU" UJINGA WA WAPIGA KURA NI MTAJI KWA WAGOMBEA(WANASIASA)
 
Mbona imeshatokea hivyo Marekani
kwa wakili kumtetea mtuhumiwa aliyetuhumiwa kumuua mtoto wake, mwisho wa siku ukweli ukajulikana
kuwa hakuhusika bali alitolewa kafara na vigogo ili kulinda maslahi yao... tusiangalie jambo hili kwa upande mmoja tu

Wapi Marekani imewahi kutokea hivyo? Na kama imewahi kutokea nina uhakika kabisa huo uamuzi ulikuwa ni controversial!
 
NAUNGA MKONO HOJA. Hao mafisadi dagaa wakiishinda kesi serikali na kuidai fidia je, hizo fedha sio za walipa kodi? Je MARANDO hawezi kulipwa kamisheni au gharama za kesi? ATAPOKEA??? njii hii bwana wajinga do waliwao. ukiwa mjinga lazima uliwe. NITAMSIFU SANA KAMA ATAFUNGUA KESI YA WANAFUNZI WALIOKOSA MKOPO MWAKA HUU(+14,000) DHIDI YA BODI YA MIKOPO.
 
MARANDO ANATAKA APROVE KWAMBA wale ni vijidagaa Wahusika WaPO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…