Marando: CHADEMA waliongea na Lowassa akiwa bado ndani ya CCM

Marando: CHADEMA waliongea na Lowassa akiwa bado ndani ya CCM

Chadema wanaendesha Siasa kama Vilabu vya Mpira. CCM ilikuwa na haki zote kumkata Lowassa kama kweli hii Habari ni kweli. Sasa hivi Lowassa ndo Kiongozi Mkuu wa UKAWA na ndie amewapiga Marufuku UKAWA wasimshambulie Zitto na Magazeti yote ya Mbowe yameufyata kwa Zitto tangu Tarehe 26 July
 
We mleta mada,,Malando ni nini?

Kama mods watakuwa wakweli na watalinda maadili yao watarudisha kile nilichoandika mm mwanzo na sio hili jina waliloleta baada ya kuedit...wawe makini na lugha hii inapunguza ubora wa mtoa mada kumbe ni wao wana edit kichwa cha somo na mada yenyewe. Waje wakiri na waedit vizuri hilo jina...please?
 
kumbe chadema hawakuwa na mgombea urais mpaka wanakwenda kuokota mafisadi.
 
kumbe chadema hawakuwa na mgombea urais mpaka wanakwenda kuokota mafisadi.

Kaa kimya km huna jipya,tafuta jipya uungwe mkono kuliko kubwbwaja,kwanza hili jukwaa linanikera sana kuhusu utumiaji wa picha za avater,yani lijitu linakurupuka linaweka picha ya mtu bila ridhaa yake,alafu kibaya zaidi unakuta ni gamba.
 
Katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, Mabere Marando amesema, yeye alianza kumshawishi Lowassa akiwa bado CCM, Alimfuata Dodoma. Amesema Katiba ya CHADEMA haina Sharti la Mwanachama kuwa na Umri gani ndani ya Chama ili agombe Urais kama ilivo kwa CCM.

CHADEMA unaweza ukajiunga leo kesho ukagombea. ndani ya CHADEMA ukiongea na watu nje ya chama ukishawishiwa kuhama chama ni Usaliti, lakini ukiwa unaongea na mtu aliye nje ya chama kumleta ndani ya chama sio Usaliti.

Hiyo inaleta hisia gani! Anakiri kwamba EL alisaliti chama chake ccm anatuaminisha nini? Je dhambi ya usaliti ataiacha?


Akiwa CCM fisadi akija Chademasafi.

Ukitoka Chadema kwenda vyama vingine msaliti, Ukitoka vyama vingine kuja Chadema mzalendo.

Zidumu fikra za Mwenyekiti.!
 
siasa za wendawazimu sidhani kama tunaziweza tuwaulize wananchi wa kusadikika
 
Hawa watu wanatuchezea na lugha za kisiasa....ukiwa upande huu utaitwa kamanda mzalendo mpiganaji n.k ukiwa upande wa pili utaitwa fisadi gamba n.k haijalishi umehamia au ni mkaazi wa kudumu, haijalishi una tuhuma au la...utabeba hizo sifa. Huo ni ulaghai. Mfumo wowote unajengwa na watu corrupt km waliopo ni wachafu hata waende wapi watakumbuka kufanya matendo yao machafu. Tupime integrit yao...
 
Lowassa alishajua mchezo mbaya wa familia kuhodhi mamlaka ya Chama..... Chama gani kinaongozwa na mke wa Rais na mtoto wa Rais?.... Majina ya mfukoni yalishajulikana miezi 3 iliyopita na Hata Mwandosya alisema mwezi wa 4 alipelekewa hayo majina.... Mbaya zaidi wengine walikuwa hata hawana mpango wa kuchukua fomu....
Ocampo 4 unapotosha mchana kweupeeee?
kwani Lowassa ile 50Bn ya mara ya kwanza alitaka kumpa nani ambaye alikodiwa ndege kwenda ipokea
hadi wakamtishia kumfukuza Dr Slaa
ni kwanini ZZK au Kabouru hamkuwataka wasogee jikoni
angalia tena vyama vinavyoendeshwa kiimla kwani Lowassa anaweza timuliwa siku yeyote
 
CHADEMA walikuwa wakipiga kelele kuwa Lowasa kaonewa kukatwa.Kumkata mtu ambaye ni CHADEMA ndani ya CCM ni sahihi kabisa.Tundu Lissu akiongea na sauti ya ujerumani idhaa ya kiswahili alisema kuwa walishakubaliana na Lowasa kuhusu yeye kuingia CHADEMA miezi mitatu kabla ya mchakato wa uraisi CCM.Kwa hiyo CCM alikuwa kajiegesha kama pandikizi la CHADEMA.CCM ikampiga chini huyo CHADEMA lowasa CHADEMA wakajifanya kupiga kelele kuwa kaonewa lakini wameanza kujisahau wanamwaga hadharani kila kitu.Lowasa ni mmoja wa wafadhili wakuu wa CHADEMA na ACT Wazalendo kile cha Zitto kabwe na ndie mwanzilishi wa UKAWA aliuanzisha kwa kutumia proxy ili aje autumie baadae.

Hata mpige Kelele wa Tanzania washaziba masikio kama mbwai na iwe mbwai hawadanganyiki tena, kila lililowapata walisema tukutane October sasa inafika, tulieni wananchi wafanye yao.
 
Mwl wa maswala ya siasa atoa changamoto kwamba ccm hawakukosea kumuondoa msaliti ndani ya chama chao....tazameni kwa kutumia akili yenye udadisi...acheni ushabiki tu munaua mwelekeo mzuri wa siasa

CCM wamemwondoa nani ndani ya chama?
 
Katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, Mabere Marando amesema, yeye alianza kumshawishi Lowassa akiwa bado CCM, Alimfuata Dodoma. Amesema Katiba ya CHADEMA haina Sharti la Mwanachama kuwa na Umri gani ndani ya Chama ili agombe Urais kama ilivo kwa CCM.

CHADEMA unaweza ukajiunga leo kesho ukagombea. Amesema ndani ya CHADEMA ukiongea na watu nje ya chama ukishawishiwa kuhama chama ni Usaliti, lakini ukiwa unaongea na mtu aliye nje ya chama kumleta ndani ya chama sio Usaliti.

Hiyo inaleta hisia gani! Anakiri kwamba EL alisaliti chama chake ccm anatuaminisha nini? Je dhambi ya usaliti ataiacha?


Acha ujuha mwaka huu mtaisoma namba Lumumba hampati usingizi!
 
Waliokuwa madiwani baada kushindwa kutetea nyazifa kwnye kura za maoni ccm wakimbilia chadema kupima upepo.
 
Ushauri wangu kwa Ukawa.
CCM ni mabingwa wa kuweka pingamizi dhidi ya wagombea.
Ukawa kupitia chama mojawapo wamsimamishe mgombea mwingine anayeoneka
kuwa namba mbili kwa nafasi ya urasi na hata kwa wabunge pia.Ikitokea
mmoja akashindwa kwenye pingamizi basi huyo mgombea mwingine abebe nafasi
ya UKAWA.Ikitokea wamepita wote basi waangalie upepepo wa wananchi
unakwenda kwa nani,sasa hapo mmoja amwachie mwezie.
Kwa mfano Dr. Slaa anaweza kuhamia CUF au NCCR kwama alivyofanya
MH.Duni wa CUF ili agombee huko kwa tahadhari. Ikitokea wote wamepita
bila pingamizi, basi waangalie ni yupi anakubalika kwa wananchi. Kutoka
hapo wanaweza kuamua nani aendelee kubeba Ukawa. Muungano wao una nguvu ya kushinda hila za pingamizi za CCM. Nafasi wanayo kubwa sana.
 
Dr benson bana ndo mwl wenu wa uchambuzi wa siasa ambaye ni kada wa ccm hii hatari.. ccm mtalia sana mwaka huu ukawa mbele kwa mbele kamwe haturudi nyuma..
 
Mwl wa maswala ya siasa atoa changamoto kwamba ccm hawakukosea kumuondoa msaliti ndani ya chama chao....tazameni kwa kutumia akili yenye udadisi...acheni ushabiki tu munaua mwelekeo mzuri wa siasa
Unazungumzia Mwl. yupi? huyo aliyekuwa na mihemko yaani anasema yeye alikuwa upande wa Lowasa wakati ule akiwa CCM lakini kwa sasa haoni kama wapinzania watafanikiwa kwani wamekosea halafu mwisho wa siku anasema yeye hana chama chochote anachokishabikia ebu tafakari kwa kina je huyo unayemuita Mwl. wa masuala ya siasa je anawafundisha nini wanafunzi huko vyuoni. nimemtazama kwa makini nimemuona ni mtu hasiye elewa nini anaongea na ni nini anachokisimamia kwani yupo kama mtu aliyelishwa maneno tu ya kuja kuongea katika kipindi husika.
 
Wanatafakari kwa kutumia utumbo mkubwa siyo ubongo ndio maana nyakati hawazisomi...
 
Back
Top Bottom