Marando: CHADEMA waliongea na Lowassa akiwa bado ndani ya CCM

Marando: CHADEMA waliongea na Lowassa akiwa bado ndani ya CCM

njeeseka

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
1,374
Reaction score
985
Katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, Mabere Marando amesema, yeye alianza kumshawishi Lowassa akiwa bado CCM, Alimfuata Dodoma. Amesema Katiba ya CHADEMA haina Sharti la Mwanachama kuwa na Umri gani ndani ya Chama ili agombe Urais kama ilivo kwa CCM.

CHADEMA unaweza ukajiunga leo kesho ukagombea. Amesema ndani ya CHADEMA ukiongea na watu nje ya chama ukishawishiwa kuhama chama ni Usaliti, lakini ukiwa unaongea na mtu aliye nje ya chama kumleta ndani ya chama sio Usaliti.

Hiyo inaleta hisia gani! Anakiri kwamba EL alisaliti chama chake ccm anatuaminisha nini? Je dhambi ya usaliti ataiacha?

 
Lowassa alishajua mchezo mbaya wa familia kuhodhi mamlaka ya Chama..... Chama gani kinaongozwa na mke wa Rais na mtoto wa Rais?.... Majina ya mfukoni yalishajulikana miezi 3 iliyopita na Hata Mwandosya alisema mwezi wa 4 alipelekewa hayo majina.... Mbaya zaidi wengine walikuwa hata hawana mpango wa kuchukua fomu....
 
Kumbe walikuwa hawana mgombea wa ukawa? Hivi marando anataka kutueleze maana yake nini kwa hii kauli? Wakati anaulizwa swali na mwandishi kuhusu sheria zikoje mtu ambaye yupo bado ndani ya chama na bado anafanya mawasiliano ya kuhamia chama kingine. Marando alikwepa kutoa jibu hadi alipokumbushwa tena kwamba amesema kwamba yey marando alishiriki mchakato wa kumleta el kabla ya kukatwa ccm ndipo akajibu ndio japo alisita kidogo. Katika sentensi hii ya marando km ina ukweli kuna jambo linaonekana nyuma ya pazia....tumia muda kuangalia
 
ushindi palepale....nimependa CUF tulivyobaki kitu kimoja. vigeugeu wachache hawakosekani safarini
 
we naye janga tu..yeye alikuwa anarejea chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) sasa unajiuliza swali la nini?
 
Du malando=marando?

katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, mabere malando amesema, yeye alianza kumshawishi lowassa akiwa bado ccm, alimfuata dodoma. Amesema katiba ya chadema haina sharti la mwanachama kuwa na umri gani ndani ya chama ili agombe urais kama ilivo kwa ccm.

Chadema unaweza ukajiunga leo kesho ukagombea. Amesema ndani ya chadema ukiongea na watu nje ya chama ukishawishiwa kuhama chama ni usaliti, lakini ukiwa unaongea na mtu aliye nje ya chama kumleta ndani ya chama sio usaliti.

Hiyo inaleta hisia gani! Anakiri kwamba el alisaliti chama chake ccm anatuaminisha nini? Je dhambi ya usaliti ataiacha?

 
muanzisha maada, malando ndio nini?? sasa kama wewe na usomi wako unakosea jina la mtu kiasi hiki, una akili kweli??

inaboa sana kuona unakosea jina la mtu na haushstuki kabisa
 
Marando kasema walianza nae mazungumzo wakati CCM wakiendelea na vikao vya uteuzi lakini hakusema alimfuata Dodoma yeye binafsi.Acha kupotosha.
 
Sawa WabeLOya, tumekusikia 🙂 . Ulimi hauna mfupa ingawa vidole vina mishipa sijui? Acha waliosoma Biology waseme zaidi.

muanzisha maada, malando ndio nini?? sasa kama wewe na usomi wako unakosea jina la mtu kiasi hiki, una akili kweli??

inaboa sana kuona unakosea jina la mtu na haushstuki kabisa
 


Hiyo inaleta hisia gani! Anakiri kwamba EL alisaliti chama chake ccm anatuaminisha nini?


CHADEMA walikuwa wakipiga kelele kuwa Lowasa kaonewa kukatwa.Kumkata mtu ambaye ni CHADEMA ndani ya CCM ni sahihi kabisa.Tundu Lissu akiongea na sauti ya ujerumani idhaa ya kiswahili alisema kuwa walishakubaliana na Lowasa kuhusu yeye kuingia CHADEMA miezi mitatu kabla ya mchakato wa uraisi CCM.Kwa hiyo CCM alikuwa kajiegesha kama pandikizi la CHADEMA.CCM ikampiga chini huyo CHADEMA lowasa CHADEMA wakajifanya kupiga kelele kuwa kaonewa lakini wameanza kujisahau wanamwaga hadharani kila kitu.Lowasa ni mmoja wa wafadhili wakuu wa CHADEMA na ACT Wazalendo kile cha Zitto kabwe na ndie mwanzilishi wa UKAWA aliuanzisha kwa kutumia proxy ili aje autumie baadae.
 
nimeamini cdm hawakuwa na mgombea uraisi ndio maana walimfuata lowasa
 
SIASA ina Sayansi yake ndo maana kuilewa inakua Ngumu kidogo.

Ni hivi lengo kuu la upinzani ni kushika dola au kua na Nguvu katika vyombo vikuu vya Maamuzi.
Sasa mnawezaje kuvipata hivi ndio Sayansi ya Siasa inaingia hapa, kama ifuatavyo :-

1.Kuunganisha Vyama vya Upinzani kupata Nguvu ya Pamoja.
Hii ni kanuni namba Moja na Kuu katika halakati za kushika Dola au kupata Nguvu ktk Vyombo vikuu vya Maamuzi kama ambavyo Vyama vinavyounda UKAWA vilivyofanya.

2. Kuvunja Nguvu ya chama Tawala (CCM)
Hii ni kanuni namba Mbili Kuu ambapo Umoja wa vyama Pinzani unavunja nguvu ya Chama Tawala kwa kila namna ili kupunguza na Kudhohofisha Nguvu ya Chama Tawala, mbinu kubwa hapa inajumuisha Kuchukua Watu Muhimu na Wenye Ushawishi katika Chama Tawala kama ilivyo kwa Lowassa.

3. Kupanga Mipango Madhubuti ya Kushika Dola na Kushika Vyombo Vikuu vya Maamuzi.
Hii ni kanuni namba Tatu kuu ambapo Umoja wa Vyama vya Upinzani pamoja na Vigogo waliowapata toka Chama Tawala wanaunda Mikakakti Madhubuti ya Ushindi wa pamoja.

Hizi ndizo KANUNI KUU ZA SIASA SAYANSI kutumiwa na Upinzani kufikia Malengo.
 
Katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, Mabere Marando amesema, yeye alianza kumshawishi Lowassa akiwa bado CCM, Alimfuata Dodoma. Amesema Katiba ya CHADEMA haina Sharti la Mwanachama kuwa na Umri gani ndani ya Chama ili agombe Urais kama ilivo kwa CCM.

CHADEMA unaweza ukajiunga leo kesho ukagombea. Amesema ndani ya CHADEMA ukiongea na watu nje ya chama ukishawishiwa kuhama chama ni Usaliti, lakini ukiwa unaongea na mtu aliye nje ya chama kumleta ndani ya chama sio Usaliti.

Hiyo inaleta hisia gani! Anakiri kwamba EL alisaliti chama chake ccm anatuaminisha nini? Je dhambi ya usaliti ataiacha?


Kasemea wapi haya? baa?
 
Mwl wa maswala ya siasa atoa changamoto kwamba ccm hawakukosea kumuondoa msaliti ndani ya chama chao....tazameni kwa kutumia akili yenye udadisi...acheni ushabiki tu munaua mwelekeo mzuri wa siasa
 
Back
Top Bottom