Kiukweli nimecheka!. Serikali tatu hazina maana ya marais watatu!. Rais atakuwa ni mmoja tuu, rais wa JMT. Serikali ya Tanzania Bara itaongozwa na Makamo wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania Bara!. Serikali ya Zanzibar, itaongozwa na Makamo wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu wa Zanzibar.
Naomba kuwahadhirisha hawa vitimbakwiri wapinga muungano wetu huu adhimu, uliotokana na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kamwe hautavunjika!, Utadumu daima dumu na sana sana utaendelea kuimarika hadi serikali moja ambao Zanzibar itakuwa ni Mkoa wenye wilaya mbili za Unguja na Pemba, rais wa Zanzibar atakuwa ndiye Mhe. Mkuu wa Mkoa!.
Pasco.
Pasco,
Pokea tu li like langu ngosha. Huo ndo Muungano tunao utaka. Sio dagaa kummeza kambale hapana. Swali la kizushi; Je bunge hili linaweza kutuletea hilo au wameenda kupokea posho lukuki na kudai Ipad tuuu.
Mawazo kama haya ndo yangetawala badala ya serekali 3, za nini nasi tu wamoja wenye nia moja? Tupeni serekali moja tuu ya muungano na Rais mmoja tu akisaidiwa na Waziri nkuu na wakuu wa mikoa. Vyeo vya Marais kama wa Tff wapi na wapi? Mnaogopa nini?